Je kuna miracle money? Je ni nani ameshawahi kupata miracle money?

Je kuna miracle money? Je ni nani ameshawahi kupata miracle money?

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Miracle money ni hela unayoipata kwa njia ya ajabu kabisa ambayo hukuitarajia.

Siku za hivi karibuni kuna wakuu wa dini wamejitokeza wakosema eti wana uwezo wa kukuombea ukapata miracle money.

Nijuavyo mimi, miracle money huombewi na mtu yeyote, ila unaomba wewe mwenyewe, na huipati hadi uwe na agano.

Miracle money inakuja sio kwa ajili ya kulia bata na kufanyia zinaa. Miracle money unapata ili kutimiza mission ya Mungu kama kusaidia yatima, wajane, wagonjwa na wahitaji mbalimbali.

Ukosha fanya kwa uaminifu hiyo mission kile kinachobaki ndio cha kwako.

Ukisikia mkuu wa dini anakwambia anakuombea upate miracle money, jiulizae maswali mengi.
 
20230406_100449.jpg
 
Wajinga,Wavivu,Wagojwa ndiyo huwa wapigwaji na hawa manabii wa Uongo,

Kwanza Mwenyezi Mungu akimpenda mja wake lazima ampe mitihani ya umaskini maradhi na mengineyo,ukisimama katika imani yako madhubuti utakuwa umefaulu.

Ayubu aliugua,akafiwa na watoto zake,mifugo yake ikafa,lakini hakufikiria miujiza.

Musa alimkimbia firauni akatembea ya miguu kutoka Misri mpaka palestini kwa siku 11,aliishiwa chakula mpaka wakala majani kama mboga,Viatu vilichanika akatembea pekupeku mpaka miguu ikapasuka

Mtume Muhamad (S.A.W)alitengwa na makureshi wa makka hakuna kuuza wala kununua akawekwe kwenye bonde Yeye na familia yake wakaishiwa chakula wakabaki kula majani ya miti wewe nani?

Hawa mitume kazi yao ni kuwapiga waumini hawana tofauti na matapeli
 
Jamaa kuingia chumbani akakuta bonge la chatu kitandani, akatoka speed, akaomba mizimu yake kwa dhati. Kurudi ndani akakuta kitanda kumejaa wekundu wa msimbazi. Kazi ni kuhesabu, mpaka akachoka, sasa hivi ni tajiri kati ya matajiri.
Imetokea wapi hii?
 
Back
Top Bottom