Je, kuna Mkazi yeyote yule wa Jimbo la Kawe aliyeanza kuzishuhudia ahadi lukuki za maendeleo za Mbunge Askofu Gwajima?

Huyu Mbunge Jiwe kabisa. Ukimpigia Simu hapokei.
 
Yuko busy Na maombi ya kumfufua Mwenda zake.
 
Kipande Cha barabara mita 200 hapo africana aliwahidi bodaboda na bajaji hajatekeleza sembuse kuwapeleka US....nilipanda bajaji njia Ina maandaki nikamuuliza bajaji hapa mmeshindwa kuzawazisha kweli kasema Gwajima aliwahidi wakati wa kuomba kura Hadi leo hawajamwona...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mbona tuna aibishana sasa,njoo inbox mkuu...
 
huyu mla kondoo hawezi timiza ahadi. Frola mwenyewe bhapati hata noti moja
 
Mimi nasubiri boat πŸš£β€β™€οΈ la uvuvi,usikute TRA wanamzingua Mama aingilie kati boat ziachiwe Sisi tupige kazi.

DR Askofu Rashid hoyeeeeee 🚁
 
Wakuu

Mheshimiwa wetu wa kawe ndugu Gwajima akumbushwe alituahidi kwenda marekani sisi vijana.

Sasa kura tulimpigia mbona toka aende bungeni yuko kimya?

Wengine tulishaaga na ndugu zetu kua mambo yameiva, na tukaanza na kujifunza kiingereza tena kama jamaa yangu zakaria yeye alinyoosha na nguo kabisa akaweka kwenye begi sasa mumukumbushe inakuaje safari hii ipo au haipo ili tuelewe jinsi ya kujipanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…