Je, kuna Mkazi yeyote yule wa Jimbo la Kawe aliyeanza kuzishuhudia ahadi lukuki za maendeleo za Mbunge Askofu Gwajima?

Je, kuna Mkazi yeyote yule wa Jimbo la Kawe aliyeanza kuzishuhudia ahadi lukuki za maendeleo za Mbunge Askofu Gwajima?

Huyu mh. Mbunge wa kawe watu wanamtafuta Kawe sokoni aliahidi ujenzi wa soko na barabara kuelekea kanisa la KKKT lakini wapi hata kupita kusalimia haonekani nadhani ataonekana tena 2025.

Watu wa Makonde Kwenye shule karibu nne wanamtafuta awaeleze ni kwanini Lami iliishia Shopperz tu ilihali nao ni walipakodi wazuri lakini lami haikuendelea mpaka makonde haonekani. Watu wamtafuta wamuulize ni kwanini Lami inaelekea kwa Lukuvi na Chibu dangote lakinj mitaa yenye mabepari ya kina Temu lami haikupigwa na ndio walipa kodi wakubwa haonekani

Ccm mlikosea sana kumsimika huyu mchunga kondoo wa bwana kwani jimbo lake watu wanamuulizia na barua,email wanamtumia mheshimiwa vipi vyuo vya uvuvi, miundombinu mbona kimya hata greda la manispaa lipite tuu lichonge barabara yeye kajichimbia Dar au dodoma . Mh mtume hata Metuselah aje aseme na wananchi wenyeviti wanafunga ofisi wanaogopa maswali magumu.
Huyu Mbunge Jiwe kabisa. Ukimpigia Simu hapokei.
 
Nikiwa kama Mmoja wa Wavuvi wa Ununio nimeshaandaa Siku nyingi sana Picha zangu 4 za Passport kwa ajili ya Pasi ya Kusafiria ili anikatie VIZA na Mbunge Askofu Gwajima atupeleke nchini Marekani kama alivyotuahidi na kutuhakikishia pia.

Askofu Gwajima USA unatupeleka lini?
Yuko busy Na maombi ya kumfufua Mwenda zake.
 
Kipande Cha barabara mita 200 hapo africana aliwahidi bodaboda na bajaji hajatekeleza sembuse kuwapeleka US....nilipanda bajaji njia Ina maandaki nikamuuliza bajaji hapa mmeshindwa kuzawazisha kweli kasema Gwajima aliwahidi wakati wa kuomba kura Hadi leo hawajamwona...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nikiwa kama Mmoja wa Wavuvi wa Ununio nimeshaandaa Siku nyingi sana Picha zangu 4 za Passport kwa ajili ya Pasi ya Kusafiria ili anikatie VIZA na Mbunge Askofu Gwajima atupeleke nchini Marekani kama alivyotuahidi na kutuhakikishia pia.

Askofu Gwajima USA unatupeleka lini?
Mbona tuna aibishana sasa,njoo inbox mkuu...
 
huyu mla kondoo hawezi timiza ahadi. Frola mwenyewe bhapati hata noti moja
 
Mimi nasubiri boat 🚣‍♀️ la uvuvi,usikute TRA wanamzingua Mama aingilie kati boat ziachiwe Sisi tupige kazi.

DR Askofu Rashid hoyeeeeee 🚁
 
Wakuu

Mheshimiwa wetu wa kawe ndugu Gwajima akumbushwe alituahidi kwenda marekani sisi vijana.

Sasa kura tulimpigia mbona toka aende bungeni yuko kimya?

Wengine tulishaaga na ndugu zetu kua mambo yameiva, na tukaanza na kujifunza kiingereza tena kama jamaa yangu zakaria yeye alinyoosha na nguo kabisa akaweka kwenye begi sasa mumukumbushe inakuaje safari hii ipo au haipo ili tuelewe jinsi ya kujipanga.
 
Back
Top Bottom