DOKEZO Je,kuna money laundering kwenye timu zetu? Baadhi ya timu zina matumizi ya kufuru kuliko mapato

DOKEZO Je,kuna money laundering kwenye timu zetu? Baadhi ya timu zina matumizi ya kufuru kuliko mapato

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 kuna bendi moja iliitwa Mviko Sound ,ilikuwa ikimilikiwa na mmoja wa wanafamilia yetu

Kufikia mwaka 2004 bendi ikafa,huyu ndugu yangu akasema ni bora kuwa na wanawaje kumi kuliko kumiliki bendi.

Wanawake kumi unaweza kuwatumia kama nguvu kazi au hata wakakuzalia watoto,sasa dume sima linaomba hela ya saloon kunipodoa masaa saba kazi yake kwenye bendi ni kutajataja tu majina ya mapedejezee wa mjini,mwisho wa mwezi anataka mshahara wake wakati kiingilio kwenye onesho hakizidi 5000,bendi ina wanamuziki zaidi ya 20.

Turudi kwenye mpira wetu,hakuna timu hata moja inayotengeneza faida kwa msimu,timu inasajili mchezaji kwa milioni 500, mshahara wake milioni 20 kwa mwezi,msimu mzima ana goli mbili,watamtumia mpaka msimu ambao atamaliza bila goli na kwenda timu ndogo bure baada ya msimu kuisha,no value for monet on that playet.

Gate collection ya maana ni Simba na Yanga,baada ya makato yote timu huambulia kama milioni 300 ambayo haitoshi hata kumsajili mchezaji mmoja wa maana

Mechi ya Namungo na Kagera Sugar msimu uliopita iliingiza laki saba,baada ya makato timu ikaambulia laki mbili,haitoshi hata mafuta ya gari iliyowaoeleka.

Tv rights,udhamini wa NBC na wadhamini wengine,malipo ya vilabu vinavyofanya vizuri kimataifa,,nk havikidhi hata nusu ya gharama, kuendesha timu ni gharama sana,cha ajabu kuna timu mikoani eti zinaporana wachezaji na makocha toka vimabu vikubwa vitatu vya Dar es Salaam, wanatoa wapi hela

Ukiondoa Dewji na Bakhresa wafadhili wakubwa hao wengine biashara zao sio kubwa kihivyo

Tusidanganyane mpira haulipi kihivyo
 
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 kuna bendi moja iliitwa Mviko Sound ,ilikuwa ikimilikiwa na mmoja wa wanafamilia yetu
Kufikia mwaka 2004 bendi ikafa,huyu ndugu...
Tanzania inawezekana kuna money laundering mpaka Ikulu.

Wewe unafikiri zile milioni mia saba kwa timu, mia moja hamsini kwa kanisa hili, mia moja hamsini kwa kanisa lile, mia moja kwa msikiti, anazotoa rais bila kufanyiwa auditing zote ni za walipa kodi?

Wakati huo huo mnasikia watoa rushwa wakubwa wa dunia kina Adani na DP World wanakutana na rais na kupewa deals Tanzania?

Hapo hata kama hujui kusoma picha huoni?
 
Kabisa, CAG alisema kuna A/C Ikulu haikaguliwi. Hiyo nahisi ndiyo inayotapanya huku 700m, kule na huko n.k.

Tukija vilabu lazima kuna kitu, hata hiyo kutakatisha pesa huenda ipo. Na watakatishaji pesa, hupenda sehemu kama mpira, muziki n.k akili kumkichwa.
 
Hata Al Ahly ukiangalia mapato yao na matumizi hayaendani, na sio hao tu hata ulaya ipo hivyo
Unaweza kuwa sahihi kwa sababu jitu kama Abramovic kipindi kile cha Chelsea utajiri aliokuwa nao Chelsea wadingeweza kumfirisi.
Azam FC hata wafanyeje hawawezi kumfirisi Mzee Bakhresa ila sasa kuna vitimu uchwara na wafadhili uchwara wanatunishiana misuli na mzee Bakhresa
 
Tanzania inawezekana kuna money laundering mpaka Ikulu.

Wewe unafikiri zile milioni mia saba kwa timu, mia moja hamsini kwa kanisa hili, mia moja hamsini kwa kanisa lile, mia moja kwa msikiti, anazotoa rais bila kufanyiwa auditing zote ni za walipa kodi?

Wakati huo huo mnasikia watoa rushwa wakubwa wa dunia kina Adani na DP World wanakutana na rais na kupewa deals Tanzania?

Hapo hata kama hujui kusoma picha huoni?
Kweli kabisa mkuu
 
Kabisa, CAG alisema kuna A/C Ikulu haikaguliwi. Hiyo nahisi ndiyo inayotapanya huku 700m, kule na huko n.k.

Tukija vilabu lazima kuna kitu, hata hiyo kutakatisha pesa huenda ipo. Na watakatishaji pesa, hupenda sehemu kama mpira, muziki n.k akili kumkichwa.
Viongozi wengi wa vilabu vya soka Tanzania ni watu wa Usalama wa Taifa wenye ajenda kubwa sana zaidi ya michezo.

Na hawa huwa hawagusiki hata wakifanya money laundering.
 
Sekta ya michezo na burudani iliongoza kuingizia mapato serikali kwenye budget iliyopita
Huenda hela IPO au hoja Yako ikawa na mashiko
Kuna timu kubwa mwaka jana,Rais waje akisema kwenye mkutano mkuu kuwa walikuwa na nakishi ya milioni nyingi sana
 
Back
Top Bottom