DOKEZO Je,kuna money laundering kwenye timu zetu? Baadhi ya timu zina matumizi ya kufuru kuliko mapato

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna timu kubwa mwaka jana,Rais waje akisema kwenye mkutano mkuu kuwa walikuwa na nakishi ya milioni nyingi sana
Michezo Ina hela sana hasa hizi team zikienda kimataifa sema ndio bado hatujaangalia hili jambo kwa jicho la pekee ila michezo imeitajirisha Uingereza na Spain kwa mda mrefu sana
 
Football clubs ni Money Laundry schemes.

Hapa Tanzania ukiondoa vilabu vya wanachama na Azam zingine zote ni mipango ya kutakatisha fedha.
 
Inasikitisha sana, nchi kwa hatuheshimu Sheria na uoga wa kufanya uhalifu haupo tena.
 
Hakuna Biashara nzuri kama mpira kwa sasa,, hao Singida Big Star msimu huu wamemuuza mchezaji wao Benjamin Tanimu kwenda Ulaya kwa zaidi ya billion 2,, hakuna cha utakatishaji pesa wala nini ni hesabu tu na ku-take risk ya kile unachowekeza,, mchawi mtaji,,
 
Wanadanganya,Azam,Simba na Yanga hawajawahi kuuza mchezaji hata bilioni moja kwa miaka ya karibuni,sembuse Singida
 
Michezo Ina hela sana hasa hizi team zikienda kimataifa sema ndio bado hatujaangalia hili jambo kwa jicho la pekee ila michezo imeitajirisha Uingereza na Spain kwa mda mrefu sana
Ni kweli ila Simba na Yanga wanajitahidi ila hicho kiasi wanachopata kimataifa ni usajili wa wachezaji wawili au watatu tu wa kimataifa
 
inamaama ni mm tu sijaelewa kuhusu money laundering maana nyie mnasema wanatakatisha pesa ambazo hazina maelezo zimepatikanaje au zimetoka chanzo haramu lakini mm nijuavyo ukitakatisha pesa basi lazima hio hela irudi tena kwako baada ya kuwa safi sasa kwa mifano iliyotolewa humu mara kanisa mil.150, msikiti mil.100, stars mil.700 hizi utasemaje za money laundering waliopewa wanazitumia kujengea na wachezaji wa stars wamegawana huo mpunga wala hazijarudi kwa aliezitoa ili afaidike nazo tena hio eti hizo pesa zinatakatishwa kivp hasa ikiwa hela hazirudi tena mikononi kwa mwenye nazo ..sasa hawa wanaopiga kelele ooh hio utakatishaji pesa hivi wanajua maana yake hasa au wanafata mkumbo tu...wanaojua watusaidie hii money laundering ikoje
 
Njia za kurudisha hizo pesa kwao haziwezi kuwekwa wazi,si rahisi kuzijua,oesa ya halali inauma kuitapanya nkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…