DOKEZO Je,kuna money laundering kwenye timu zetu? Baadhi ya timu zina matumizi ya kufuru kuliko mapato

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ngoja nikupe elimu ya kitaa.

Iko hivi, watu wana pesa chafu, wanaiingiza kwenye timu ya mpira, pesa inatumika kusajili wachezaji na benchi la ufundi. Wanatengeneza rekodi fake ya mapato, kuanzia viingilio hadi udhamini. Mianya yote ya taarifa husika inazibwa. Pesa inazunguka inawarudia wahuni ikiwa saaafi.

Senti mbili zangu.
 
hata hujaeleweka mfano ww unazo bilion moja ukaiingiza kwenye timu ya mpira zikasajili na kulipa mishajara wachezaji maana yake bilioni imeishia mifukoni mwa wengine kihalali...sasa ishu ni kwako ww uliyetoa hiyo bilion kwa lengo utakatishe pesa iwe safi kisha uje kuitumia kwenye mzunguko halali lakini ulikozifanyia manuva hazikurudi zimetumika..pia umesema pesa hiyo inazunguka inawarudia wahuni kivp wakati ishatumiwa kwa kusajili na kulipa mishahara ya wachezaji na makocha ina maana hao waliolipwa wanamrudishia mtakatishaji pesa yake.! mm naona hii money laundering wengi wetu hatujui undani wake ila tunafata mkumbo tu kishabiki hatuna maelezo yaliyonyooka eti mtu atakatishe pesa alafu isirudi kwake
 
ni dunia nzima

soka kuna namna, we piga hesabu tu hata kwa team za ulaya utaona
 
Kama haujaelewa omba ufafanuliwe ila usikaze hilo fuvu. Nimeshakwambia kuna rekodi feki za mapato zinatengenezwa na hapo ndiyo pesa inapowarudia wahusika ikiwa safi. Kuwa mjanja kdg basi.

Ili kujustify mapato yanayoripotiwa, lazima na gharama nazo ziwe zimeshiba, ndio tunachokiona kwa baadhi ya hivi vilabu.
 
Nafikiri kumiliki timu ya mpira ni biashara kama zingine, hiyo pesa ya kuwalipa mishahara na usajili inarudi kwenye makusanyo ya viingilio , kuwauza wachezaji , pesa za wazamini pamoja na malipo kutokana na kuchukua vikombe mbalimbali pamoja na kushiri mashindano ya kimataifa (cafcl).
Pesa inayopatikana huko hua inarudi Kwa mabosi.
 
ok, ila mkuu unachukulia utakatishaji pesa kama kitu rahisi sana hata kama ukitengeneza rekodi feki za mapato je,unaongeza namba au unapunguza..hapo utaingia kwenye kesi ya ukwepaji kodi TRA na sidhani kama timu zetu zinaigiza mapato ya maana kiasi cha watakatishaji kurudisha pesa zao maana matumizi ya timu zetu ni makubwa kuliko mapato wanayoingiza ukija kutoa gharama za timu hamna hela ya maana inayobaki wengine wana hasi kabisa.! usisahau kuna kuna kitengo cha kuzuia fedha haramu za utakatishaji -FIU na ukileta mbinu za kitoto kwenye kutakatisha pesa unadakwa mapema so lazima njia iwe ndefu kidogo kuruka viunzi ila hizi njia fupi zilizotajwa humu tunadanganyana tu
 
Wewe kweli kichwa kigumu. Naona umemiss sehemu niliyosema "mianya yote ya taarifa inazibwa", umeelewaje kauli hiyo? Unadhani anayefanya inshu hizi ni mtu hohehahe?
 
Imagine wanataka kumpa mkataba kocha Gamondi???
Ile ni yanga B...ni kama mwanachama mwenye ushawishi mkubwa yanga a, kaamua kua na yanga b ..sababu, yawezekana kupambana na simba na vilabu vingine vnavyokuja kwa kasi
 
Kwa marungu haya ya Trump zitaanza kufa mda si mrefu
Ukiona miradi iliyoaanza imesimama ghafla ujue ni Trump effects
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…