Benjamin ana rafiki wa kike, lakini hahisi kuwa bado ni uhusiano wa kutosha, na amechagua kungoja!
Hiyo ilipaswa kuwa mwisho wake, lakini Katy Perry anamuita ili ambusu. Benjamin anasita ila anakubali kumbusu Katy Perry shavuni. Mara paaap! Katy Perry anageuka na kumbusu Benjamin mdomoni bila kujali msimamo wa Benjamin kuwa hataki ku-kiss nje ya mahusiano! Majaji wengine wanafurahia kitendo hiko ila Benjamin anaonekana kutopendezwa na tukio hilo.
Kutokuelewa au kuheshimu mipaka ya watu ni jambo lisilofaa kwa jamii ya leo. Kucheka juu yake, haswa ikiwa ni kitu kinachotokea kwa mwanaume, hufanya iwe mbaya zaidi. Unyanyasaji wa kijinsia sio tatizo linapotokea kwa wanawake tu, ni tatizo linapotokea kwa wanaume pia!