Dr Count Capone
JF-Expert Member
- Feb 7, 2017
- 1,878
- 3,263
mtu chake wa kupuliza kayaman zitto junior GENTAMYCINE Count Capone hili la uwepo wa jamii ambayo ni inbreeding depression huko Rwanda mnalifahamu ?
Suala la inbreeding depression miongoni mwa waHutu, waTutsi na waTwa sijawahi kutana na ushahidi wa kuthibitisha kuwa hilo linafanyika ktk kiwango cha kuathiri jamii nzima.
Sidhani kama madai ya kusema 90% ya Warwanda wanafanana na PK ni sahihi.
Na ni kwa sababu ni kuwa Watutsi wana sifa ya Urefu, pua nyembamba mchongoko, vichwa vidogo na rangi ya ngozi kuwa nyeupe kama ya WaEthiopia au WaEritrea huku waHutu wakiwa ni wengi wao wafupi, Pua za kibantu (nimeshindwa kueleza vizuri ila tazama pua za waLuba wa Kongo), na wana rangi nyeusi kabisa.
Japokuwa kutokana na muingiliano wa muda mrefu baina ya watu hawa sifa hizo kwa kiasi fulani huenda zikaonekana kwa watu wa makabila yote ya Rwanda, ila zinabaki kuwa miongoni mwa sifa pambanuzi.
Kitakwimu inakadiriwa kuwa 85% ya watu huko Rwanda ni Wahutu, 14% ni Watutsi na Twa ni 1%. PK mwenyewe akiwa Mtutsi na sifa zake kama nilivyoonesha hapo juu hafanani na mHutu aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana.