Hapo ndipo mataifa ya kiafrika yanapokosa simuluzi zinazounganisha taifa.
Yaani umoja haupo kila kakikundi kiwe cha kiimani, kikabila na kikanda wana simulizi zao za umoja katika uchache wao.
Lini nchi itakuwa na simulizi ya kitaifa kama USA, RUSSIA, CHINA, JAPAN n.k kadhalika.
Moja ya stori ya umoja ingeletwa na makabrasha yanayoelezea Tanzania yenye makabila mengi, imani tofauti pia jamii zikiwemo za kisomali, kihindi, kijerumani, kigiriki ziliungana chini ya jemedari mkuu mwalimu Nyerere kwenda kumpiga, kumfukuza na kumtupa mvamizi nduli nyoka Iddi Amin Dada nje ya mipaka yetu .....
Tatizo stori hizi za ushujaa wa jamii yetu tunazifanya ni siri kubwa na maveterani kama jenerali David Musuguri, makamanda na maofisa, wapiganaji na mgambo wapo lakini hatuoni kuwa vita ya Kagera ni moja ya simulizi ya umoja wetu katika mchanganyiko wetu kama taifa.
Nchi kama USA ama Russia simulizi hizi za umoja kupitia kumshinda adui mvamizi hutumika ktk mitaala ya shule, tamthilia, movie, mahojiano katika media House n.k kuonesha jambo lililofanyika kwa umoja mfano vita dhidi ya mvamizi Hitler, Napoleon n.k
A national narrative rationalizes and is supported by the nation's identity
Waandishi nguli, wanahistoria, wakutubi, wataalamu wa makumbusho na mali kale, watayarishaji movie, chuo cha ulinzi wa Taifa NDC, wizara ya utamaduni, elimu n.k wanaweza kabisa kuandaa dokumentari ndefu ikiwa na star Jenerali David Musuguri lakini imelenga kubeba ujumbe kama jamii yote moja iliweza kipindi fulani kushinda mvamizi kutoka nje
View: https://m.youtube.com/watch?v=BveT5bVV9p4