Habari.
Niwatakie mapumziko mema ya uhuru wa nchi yetu pendwa Tanganyika,
Turudi kwenye mada,nataka kujua kama kuna uhusiano wa akili (intelligence) mama na mtoto,yaani kama uwezo wa akili wa mama unaweza kua na madhara(effects/impacts) kwa mtoto atakae mzaa.
Kuna binti niko nae kama rafiki,uwezo wake wa darasani ulikua mdogo sana,akili ya darasani ni ndogo sana lakini ni mzuri sana kwa umbile na mwenendo/tabia..
Je anaweza akaja kuzaa watoto wenye akili ndogo darasani kama yeye au watakua tofauti?
Karibuni.
Yup!
Ndo maana ufaulu wa darasani kama kipimo cha uwezo wa akili ya mtu si sahihi.
Uhusiano uko mkubwa kati ya akili au watoto na.mama yao genetically. Na ndiyo maana zamani hasa koo za kichifu zilikuwa zinachunguza akili na behaviour ya kwa wajomba. Mimi binafsi kwenye ukoo wetu au familia yetu tuna akili ila hazishindi za ukweni kwangu kwa wachagga. Wanangu sikupata nao tabu ya tuition na walikuwa hawaendi. Na muda mwingi si kusoma sana bali pia kujifunza utundu wa kila kifaa na umeme. Kidato cha nne wote one single digit na vyuoni wote first class. Mmoja wazungu walimng'ang'ania.

Kuna watu hapa duniani ambao darasani hawakufanya vizuri na sasa wanakubalika kuwa ni baadhi ya majiniasi waliowahi kutokea hapa duniani.
Huwezi kuhoji uwezo wa kiakili wa Winston Churchill ambaye alifeli mara mbili entrance exam ya Royal Military College, huwezi kuhoji uwezo wa kiakili wa Benjamini Franklin, huwezi kuhoji uwezo wa kiakili wa Charles Darwin, hata Albert Einstein ambaye naye hakuwa mzuri darasani na ambaye alifeli entrance exam ya Polytechnic Institute ya Zurish hutathubutu kuhoji uwezo wa ubongo wake.
uwezekano upo watoto mara nying iq wanarithi kwa mama
ALBERT EINSTEIN haukupaswa kumtolea mfano kama huu kaka Jamaa ni GENIUS.
Hakufeli in such na ndio maana aliongoza kwenye physics na mathematics,na mbona alivoenda Argovian Cantonal School aliongoza.
Attachment ya cheti chake iyo hapo inaonyesha 1---6 na 6 no highest score
Kisayansi ndio...
Japo watu wanaweza kupinga...
Unajua kuna wanawake wana akili lakini hawakuwa na access na shule...
Hivyo usiseme mimi nina akili lakini mama yangu si msomi...
Nilisoma article nyingi tu zina prove kuwa akili ya mtoto inatoka kwa mama...
I see..! Kumbe!!
Kuna watu hapa duniani ambao darasani hawakufanya vizuri na sasa wanakubalika kuwa ni baadhi ya majiniasi waliowahi kutokea hapa duniani.
Huwezi kuhoji uwezo wa kiakili wa Winston Churchill ambaye alifeli mara mbili entrance exam ya Royal Military College, huwezi kuhoji uwezo wa kiakili wa Benjamini Franklin, huwezi kuhoji uwezo wa kiakili wa Charles Darwin, hata Albert Einstein ambaye naye hakuwa mzuri darasani na ambaye alifeli entrance exam ya Polytechnic Institute ya Zurish hutathubutu kuhoji uwezo wa ubongo wake.
Hakuna....
Hizo ni exceptions...na unajua plausible reason?
Watu wenye akili kupitiliza huwa hawako conventional...akiambiwa kulia yeye anasema kushoto...
Kwa hiyo wana mtazamo tofauti...na darasani ukiwa tofauti na anayetunga na kusahihisha lazima ufeli...
Ndio maana wanafunzi wengi wanamezea utofauti wao mpaka wamalize shule...
Hapo ndio kufeli kunaweza kukawa ni sababu ya akili zilizozodi badala ya ujinga...ila watu wa hivyo si wengi...