Emb elezea kwa ufupi time dilation mkuu, ukute ndo nachotafuta!
Kwa mujibu wa kanuni za Relativity kama zilivyoelezewa awali kabisa na Albert Einstein, upitaji wa muda ni kitu kinachotegemea vitu kadhaa.
1. Unategemea velocity (special relativity)
2. Unategemea gravity (general relativity)
3. Unategemea frame of reference
1. Velocity
Ukiwa na mapacha Kulwa na Doto wamezaliwa siku moja, Doto akabaki duniani halafu Kulwa akapanda spaceship kwenda nyota iliyopo kwenye mfumo wa Alpha Centauri, Proxima Centauri 4.246 kwa average velocity ya 90% the speed of light (in theory, practically we do not have the technology to reach this speed), kwa kika unit 1 of tine on board the observer on earth will count 2 and a quarter units.
Kwa Doto ataona Kulwa katumia miaka 4.71 kufika Proxima Centauri, kwa Kulwa mwenyewe ataona katumia miaka 2.06.
Kwenda na kurudi Doto ataona Kulwa katumia miaka 9.42 na Kulwa ataona katumia miaka 4.12.
Yani kama Kulwa na Doto wote watakuwa na miaka 20 kabla ya kutenganishwa, wakati Kulwa anarudi, atakuwa na miaka 24.12 wakati Doto atakuwa na miaka 29.42. Kutakuwa na tofauti ya miaka 5.3 katika umri wa watu mapacha waliozaliwa siku moja, tofauti itakayokuwa imesababishwa na time dilation.
2. Passage ya time ukiwa karibu na kitu chenye gravity kubwa inakuwa slower than ukuwa mbali nacho. Ukipanda juu kabisa kwenye jengo la Burj Khalifa time ina flow slower than pale chini, by a very tiny fraction. Kwa sababu pale chini ni karibu zaidi na gravity ya dunia kuliko juu. Gravity ina slow down the passage ya time.
3. Frame of reference. Kwa mtu aliye kwenye spaceship Kulwa, na mtu aliyeachwa dunianiDoto. Mtu aliyekaa juu Burj Khalifa na mtu aliyekaa chini, wote wataona muda unaenda sawa, tofauti itaonekana ukiwalinganisha hawa wstu walio katika frames of references tofauti.