Je, kuna ukweli kuwa waafrika weusi tumelaaniwa? (World cup rant)

Usije kurogwa kuamini timu za wamatumbi hata siku Moja. Africa timu ni moja tu- Morocco.

Wazo la gattuso kupunguza matimu ya Africa sio baya. Lifanyiwe kazi kuliko kujaza matimu yanayogawa utamu tu.
Wamatumbi hahaha min -me mmefikiwa

Wasipunguze bwana, tuko wengi mno.
 
Kuna mwandishi alisema wachezaji weusi hawawezi kukupa concentration kwa zaidi ya dakika 60. Watu wakamjia juu nadhan huko aliko anapata nguvu ya kusimamia kauli yake. South Africa, congo, ivory coast na senegal wamekufa ugonjwa mmoja.
Kuna mmoja alisema huko IG na watu walimshambulia vibaya mnoo ila saiz anatrend tu. Issue ni kama dakika za mwisho wanaanza kuparalys wanakuwa mazombie mizimu inasema yakishinda haya kuna watu hawata lala😁
 
Uko sahihi kabisa mkuu,
Hatutaki ushirikiano, na makocha wazawa huwa na kujikweza flani hivi, si unakumbuka mgunda alivyo tambaga just because kashind mechi 3 mfulurizo
 
Kocha kapata vigoli vyake viwili anamtoa Pape Gueye ambaye alikuwa amesettle vizuri Katikati tena mapema Tu anaingiza Lamine Camara ambaye mechi zile za mwisho alizoanza alikuwa Yuko vibaya kwenye composure, dogo hata dakika moja haijapita kala njano haha...
 
Kwani hao wakina dembele ni waafrica?

Mtu kazaliwa Brazil na Paris unawaitaje ni waafrica. Au kwako wewe mtu kuwa mweusi ndio muafrica
 
Wewe hauko sawa kabisa

Yaani unasema uwekezaji miaka hii? Angalia vikosi vya Senegal, ivory coast, angalia timu zinavyo battle na timu za Ulaya na mpira unadunda vizuri tuu

Mkuu hicho sio kigezo kabisa, unakumbuka Ghana ya 2010 Je kipindi hicho si ndo ilikua bado kabisa?
 
Jana Senegal kafanya mambo ya kichoko sana.. 2 goals ahead, unakuja kusawazishiwa ndani ya dakika 10 za mwisho haraka haraka.

Kuwa muafrika ni laana
 
Jana Senegal kafanya mambo ya kichoko sana.. 2 goals ahead, unakuja kusawazishiwa ndani ya dakika 10 za mwisho haraka haraka.

Kuwa muafrika ni laana
Hata Mm najiuliza team iliyo chukua afcon yenye wachezaji classic kabisa? So insane!
 
Yaani mpira tu mchezo wa fun ndo urelate na laana kweli....labda usemee siasa mpira usche ni sport ile acha uwanja uamue ...mbona china hawajacheza
Sio kimpira tu hadi maisha halisi, we are doomed to be loosers.. Angalia maendeleo yalivyo stagnant, angalia jinsi tunavyo kuwa exploited, angalia uongozi...
 
Sahihi, ni mentality
 
Hata Mm najiuliza team iliyo chukua afcon yenye wachezaji classic kabisa? So insane!
Team ni Morocco tu, haya mengine yanaendeshwa na mihemko. Huwezi kushindwa kuzuia dakika 10 za mwisho na unaongoza mbili.

Wanashindwa kujua huo ndio muda hatarishi zaidi kwao sababu mpinzani anafanya kila analoweza ili arudishe magoli, badala ya kuongeza compactness, nyie ndio mnarelax..

Nimekwazika sana aisee
 
Kwani hao wakina dembele ni waafrica?

Mtu kazaliwa Brazil na Paris unawaitaje ni waafrica. Au kwako wewe mtu kuwa mweusi ndio muafrica
Kwamba Dembele ni mzungu? Ng'olo Kante ni Mzungu? Au wana uraia wa huko walipo?

Kwa tafsiri yako, Bongo zozo ni Muafrika? Kweli tuna safari ndefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…