Je, kuna umuhimu kama taifa kufanya usaili kwa kada ya Afya na Ualimu ndo Uajiri?

Usaili wa siku moja unatosha kumpima mtu kuliko vyeti yake vya kitaaluma? kumbuka katoka form4, six, cheti au diploma, degree, je dk 30 za usahili zinatosha kweli kumpima mtu huyo??
Tabia inapimwa Kwa vyeti vya taaluma?
 
Kwangu mimi sio kitu cha ulazima sababu kwa mwalimu usaili wake sio wa mtu na mtu ila ni mwalimu mwenye na mwanafunzi wake je unazani watakaomfanyia mwalimu wa GEOGRAPHY au CHEMISTRY watakuwa watu wa professional wa ilo somo au hayo masomo? kama jibu ni ndio basi serikali inatumia gharama nyingi kupanga bajeti kwa kitu ambacho wanamnufaisha mtu mmoja na kufanya duplication of ajira kama mwalimu wa geo ana anaweza kuajiriwa utumishi na shuleni at the same time? na kama jibu ni hapa basi kufanyiwa interview na mtu ambae sio professional wa ilo somo basi sio kupata watu sahihi ila ni kupata mtu anahitajika na mtu na sio taasisi flani au serikali.
Pia usaili kwa mtu kwa kumuangalia kwenye dakika moja au tano na kumuuliza maswali matano sio kipimo sahihi sababu kuna siku za bad mood ya mtu na kuna siku sa mood nzuri sasa unaweza mkuta msailiwa ni mzuri in subject master but kulingana na siku husika akawa na bad mood huyu mtu unampoteza bila kujali wala nini, pia kuna issue ya location mazingira, time management hivi vitu huwa viinatoa wasaliwa kwenye mood sana, watu wanatangaza interview inaanza saa moja mnakaa interview inaaza saa 5 au saa sita hii tayari ishakutoa kweny mood pia location unapangiwa interview afu mazingira yale kumbe sio rafik kwako, in short mambo ni mengi sana.
Ushauri kama wanataka kupata walimu bora na sahihi basi hawa walimu wafanyie interview shuleni waone interaction ya mtoto na mwalimu husika, naamini kila kona kuna shule kwahiyo mwalimu aende shule yake jirani afanye usahili mambo yaishe.
 
Kusoma na kuwa na vyeti hakutoshi moja kwa moja kwenda kuajiriwa. Anayeajiriwa ni mtu na sio vyeti, vyeti ni viambatanisho tu kuthibitisha kuwa mhusika aliwahi kupitia mafunzo fulani na kufuzu. Vyeti vinaweza kutumika kama tiketi tu ya kuingia kwenye foleni ya kwenda kwenye usaili, lakini uwezo wako ndio utakupa ajira.
 
unaweza kuwa na hoja ila hoja yako ikalenga kama ukanamizajii mtu kasoma miaka minne au mitatu chuo afu waliomfundisha uliwaamini na kuwapa mandatory ya kumtarain huyo mtu leo hii utamkashifu vip mtu kuwa vyeti vyake havitoshi wakati wew ndo uliajiri watu wa kumtrain?? bora ungesema hivi interview ni muhimu sababu nafasi ni chache ili kuwapunguza nyia rahisi ni kufanya interview.
pia kaka mtu kasoma miaka mitatu haumini vyeti vyake je ndani ya dk 5 na maswali yako matano ndo utamuuumini ???
tujenge hoja sio kuja na majibu ulioyasikia mtaani huko bila kuyatafakirii kwa kina ?
 
Hakuna hata sababu ya msingi ya kufanya usaili tofauti na kukwepa lawama za majobless
Binafsi usaili nauunga mkono ila sio wa multiple choice ya dk 40 at least mahojiano ya mdomo na practical

Huwezi kupima umahili wa mtu kwa kutumia formative assessment huo ni uwongo
 
Binafsi usaili nauunga mkono ila sio wa multiple choice ya dk 40 at least mahojiano ya mdomo na practical

Huwezi kupima umahili wa mtu kwa kutumia formative assessment huo ni uwongo
yes formative assement et unamfanyia mwalimu na watu wa afya unasema unataka watu bora tuko serious kwelii??? au ndo kutaka taifa liwe la kitapelitapeli tu?? sababu kinachofata hapo ni rushwa na sio kufanya usaili
 
Mbona hizi kelele zimeanzia kwenu waalimu wakat tangu kitambo watu wa kada zngn walikuwa wanafanya usaili na hawajawahi kulalamika?
unajibu lakin utakuwa umetumia mihemko sana bila kuja na hoja mkuuu,, swali ni kwamba interview ya nurse mnaongea tu ndani ya dk tano unasema huyu nimepata muuguzi bora mkienda kupewa dawa za kichwa mkapewa za kifafa ndo mtaelewa usaili ulikuwa hauna maana yyte kwa hizi kada mbili
usaili wa afya ni very very intersive if serikali ikiamua kusema tunaka watu makini lakini sio wa kufanya mtiani wa multiple choice na oral kuulizwa 5 uestion only
mwalimu uwezi kumfanyia usaili chumbani kama mnatongozana mwalimu apelekwe darasani afanye maandalizi ya somo husika ndo utajua kweli huyu ni mwalimu au huyu kagushiiii
 
Mwajiri anataka kuthibitisha wewe mwenye vyeti una upeo na maarifa kiasi gani kufaa katika kazi zake.

Kwa kifupi sana, vyetu havitoshi kujieleza kuhusu upeo na maarifa aliyonayo mtu kwa wakati huu.
 
Mkuu huyo jamaa sio kuwa haelewi ila analeta ligi za kada na kujimwambafai na kujiona kada yake ni bora kuliko za wengine analeta ushabiki na sio kujadili kwa hoja
 
Utumishi shikilieni hapo hapo, hakuna kada kuajiriwa bila usaili.

Kwan kada ya ualimu na afya wana u-special upi mpaka wasifanye usaili wakati kada zingine zinafanya usaili?

Utumishi shikilieni hapo hapo, msiachie hata kidogo.
Inaonekana una msongo wa mawazo chuki na kukukosa Ajira, hii mada haitaji mihemko hata kidogo labda nikuambie tu baada ya hili zoezi hakutakuwa na usaili tena ni sehemu ya majaribio tu Kuona ni namna gani sahihi ya kuweza kutafuta watu kuajiri ..

Sasa wewe na depression zako usiharibu mada acha watu watoe mitazamo watu wachukue maoni kila mada nakuona unashabikia sana haya mambo tafuta kazi na nalaiti nikijua jina lako siwezi kuruhusu kijana kama wewe mwenye mihemko hizi kupata kazi
 
Mwajiri anataka kuthibitisha wewe mwenye vyeti una upeo na maarifa kiasi gani kufaa katika kazi zake.

Kwa kifupi sana, vyetu havitoshi kujieleza kuhusu upeo na maarifa aliyonayo mtu kwa wakati huu.
Shida sio assessment, shida ni aina gani ya assessment tipo choice halijawahi ku assess umahili wa mtu kwenye kutibu mgonjwa wala kufundisha mwanafunzi
 
Upo sahihi katika hili.. Idadi kubwa ha wahitimu na uchache wa nafasi za Ajira

Hawezi Athiri muhitimu wa muda mrefu mfano 2015 na muhitimu wa 2023

Au wote ni sawa wakishindanishwa katika mitihani hiyo?
 
Ndugu yangu, fahamu tu kusoma na kupata vyeti ni jambo moja, na kuajiriwa ni jambo lingine tofauti kabisa.
Huwezi kumlazimisha muajiri amuajiri mtu mwenye vyeti tu wakati malengo ya muajiri yako zaidi au nje ya vyeti.

Narudia tena kuandika hapa, cheti ni uthibitisho kuwa ulipita mafunzo na kufuzu, usaili ni kipimo cha muajiri kuona kama unakidhi na kutosha kufanya kazi zake.
 

Msingi wa usaili unabaki ule ule tu kukwepa lawama za kwanini vijana/raia hawana ajira?
 
Naitwa Emmanuel Issac Mbaga, haya nenda ukabane
 
Sasa Kama ni kukidhi, si Kuna kipindi Cha matazamio??
 
Shida sio assessment, shida ni aina gani ya assessment tipo choice halijawahi ku assess umahili wa mtu kwenye kutibu mgonjwa wala kufundisha mwanafunzi
Hiyo ni hoja nyingine, tofauti na hii.
Hapa tunazungumzia kama kuna ulazima wa usaili ili kuajiriwa na sio usaili upi unafaa.
 
Shida sio assessment, shida ni aina gani ya assessment tipo choice halijawahi ku assess umahili wa mtu kwenye kutibu mgonjwa wala kufundisha mwanafunzi
Mimi nilitegemea mfano kada za Afya wangefanyia Usaili kwa Mgonjwa maana ndiyo kazi yake ya kila siku..

Au mwalimu angeenda kutanishwa na wanafunzi..


Kama ni kweli hoja Ilikua ni usaili kwanini wanatumja njia hii ya maswali tu?

Ukiangalia kwa uharaka zoezi hili.. ni kuwa watu wanapaswa waanze kuingia kwenye vituo vya kazi kabla ya mwezi wa 9 haujaisha yaani mwezi wa 10 mwanzoni wawe wameshafika na kuchukua barua zao..

Hivyo wameona urahisi ni kutumia maswali hayo waanze kupunguza watu ikiwa wengi watafaulu sana written/ computer wachukua hata wenye scores ya 70 kuendelea itategemea na ufaulu ..

Mimi nadhani usaili huu haukulenga Moja kwa Moja kumpima.mtu anajua nini ila umelenga kupunguza Idadi kubwa ya watu ili wapate wachache kwa ajili ya kwenda kwenye oral


Kijana kasoma miaka 3 au 5
Kakutana na wagonjwa amefanya mitihani amefaulu miaka yote ameenda kufanya mtihani wa board/ council za taaluma aliyosomea amefaulu na amepewa leseni bado tena unampima ili iweje? Unampima nini? unampima ubora wake kwa maswali? Hiyo leseni kapewa vipi? Kwamba hamziamini hizo board? Na vipi hayo maswali mnayouliza akikosa mnamnyanganya leseni? Mtasema hana ujuzi?

Kama ni usaili kwanini msiwapeleke wakakutanishwa na wagonjwa. ?

Nakama ni waalimu kwanini wasikutanishwe na wanafunzi.?

Hapa utagundua ni Muda.. Wana muda mchache na wafanyakazi wanahitajika kazini.
Mkifata utaaratibu wa usaili hili zoezi lingetumia miezi hata 2 au 3.

Ila wameamua kufanya assessment kwa njia ambayo haukubaliki na wanataaluma wa afya na ualimu

Tatizo la kuchanganya siasa na taaluma

Na nawasikitikia sana wasimamizi wa haya mambo sio wataalumu wa Afya hivyo hawajui ni namna gani wanainajisi Taaluma Hizi za Afya.


Afya ni tofauti na kada zingine kabisa
 
Bloom's taxonomy of education unaielewa vyema??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…