Je kuna uwezekano wa mtu kuchukuliwa msukule na kurudishwa?

Uwezekano wa kurudi upo, ila muwahi kabla hajakatwa ulimi, Kuna wataalam walio na uwezo huo, mtaalamu moja wapo yupo Sengerema( Buchosa) maeneo ya Nyehunge,anaweza kukurudishia mtu wako.
Naweza kupata mawasiliano nae
 
Inasemekana ukiwahi anarudi,
Nimewahi kuona manzi wa chaliangu mmoja mwaka 2004 dodoma (chang'ombe) alirudi na alieleza alikokua na aliokuwa nao,akamtaja huyo bibi aliyekuwa ajiwahifadhi na kwa hasira kali walizokuwa nazo raia wakamfuta yule ajuza
Naweza pata mawasiliano yao mkuu
 
Kijana unabishana na wataaalam sasa endelea kubisha nikugeuze chura robo usivuke..

Mchawi anaye chukua mtu kuwa msukule ni mmoja tu na sio kikundi na ili akutoe pale nyuma ya mlango au popote ulipo ni lazima asimame jua linapo zamia na afanye ishara ya kumuita mtu wake Mpaka pale huyo mtu atakapo mfikia..

Na huondoka nae kwa kumbeba mgongoni au kwa kumshika mkono.. na huyo mtu anakuwa anaona watu lakn haelewi ni nini kinaendelea.

Sasa bisha tena nije kukuchukua msukule 😀
 
Njoo unichukue😂😂..mi mwenyewe mzito..waulize Kilimanjaro mtu akipewa UFUMWA INATAKIWA aweje....back to your suggestion...kuchukua msukule hawi mchawi Mmoja..mmiliki ni Mmoja ila kikosi kazi cha usaidizi huwa ni nyomi...na wachawi pia waoga wakiua wanasikilizia kama mtamaliza msiba..mkimaliza ndio wanaokata ulimi ishara ya kuwa mmekubali ndugu yenu ameenda
 
Naweza pata mawasiliano yao mkuu
Kwa sasa sina mawasiliano yake maana ni kitambo kidogo,ila kama mna hakika kapotea kimazingara ukitafuta wataalam hasa kigoma huko ndiko inaaminika wako wa uhakika unafanikiwa
 
Wenyeji wa MAGU MWANZA,GAIRO MOROGORO watakuja kutuelezea kwa kina.
 
100% truly.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…