Je, kuna wakati akili zetu huwaza ujinga?

Je, kuna wakati akili zetu huwaza ujinga?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Kuna nyakati nyingi ambazo akili zetu huwaza mambo ya kijinga au yasiyo na mantiki, na hata kutufanya tuyandike au tuyazungumze

Hali hii ni ya kawaida kibiolojia na kisaikolojia, lakini pia hugusa sana maisha yetu ya kiroho na kihisia.
Ubongo wetu unapokosa utulivu wa ndani, unakuwa kama chombo kilichopoteza uelekeo katikati ya dhoruba.

Hali hii mara nyingi ni ishara ya vita vya kiroho vinavyoendelea ndani ya nafsi zetu au matokeo ya mshtuko mkubwa wa moyo unaotokana na mahusiano.Kiroho...!

Akili inapowaza mambo ya kijinga, mara nyingi inakuwa imepoteza ulinzi wa amani ya kimungu na kuruhusu mishale ya hofu, mashaka, na majaribu kupenya.

Hali hii inakuwa mbaya zaidi pale mtu anapopitia msongo mkubwa wa mapenzi, ambapo moyo unakuwa umejeruhiwa kwa usaliti, kukataliwa, au upweke.
Maumivu ya mapenzi yanapovuruga mfumo wa fahamu, ubongo huishiwa nguvu na kuanza kuzalisha mawazo ya hovyo na ya kufikirika! ambayo huishia kwenye maandishi ya majuto au ujumbe wa usiku wa manane unaoonekana wa kijinga asubuhi inayofuata.

Unapokuwa na kiu ya kiroho huku ukisumbuliwa na majeraha ya moyo, akili inakosa kichujio cha ukweli na kuanza kuona mambo yasiyokuwepo.

Sasa ili kuiponya akili na kuepuka kuandika mambo yanayoweza kukuaibisha au kukuumiza zaidi, ni lazima utafute utulivu wa kiroho kupitia sala, kutafakari, na kujisamehe mwenyewe.

Unapohisi dhoruba stress za maisha au mapenzi zimejaa kifuani, weka simu mbali na usiruhusu vidole vyako kuandika maumivu yako katika hali ya hasira au kukata tamaa.

Linda nafsi yako kwa kukubali kuwa maisha ni safari yenye milima na mabonde, na mpe Mungu nafasi ya kuganga donda la moyo wako ili akili yako irudi kwenye mstari wa nuru, hekima, na amani ya kudumu.

Nimemaliza Mimi✍🏿👌🏿
Surrealism ♥️.jpeg
 
1.Mlevi

Kwanini mkuu
Haifai kugombana na mlevi kwa sababu pombe huvuruga uwezo wake wa kufikiri na kudhibiti hisia, hali inayomfanya ashindwe kutumia mantiki na kupandisha hasira za ghafla zinazoweza kugeuka kuwa vurugu za hatari.
Kutokana na hali hiyo, mbinu salama zaidi ni kukaa kimya, kuepuka mabishano, na kuondoka eneo hilo ili kuzuia madhara yasiyo ya lazima.
655ec7f5-c71c-4ce4-b060-6da05472367b.jpeg
 
Haifai kugombana na mlevi kwa sababu pombe huvuruga uwezo wake wa kufikiri na kudhibiti hisia, hali inayomfanya ashindwe kutumia mantiki na kupandisha hasira za ghafla zinazoweza kugeuka kuwa vurugu za hatari.
Kutokana na hali hiyo, mbinu salama zaidi ni kukaa kimya, kuepuka mabishano, na kuondoka eneo hilo ili kuzuia madhara yasiyo ya lazima.View attachment 3597979
Umenena vema mkuu huyo ni mimi kabisa

Sema huyu fala mshamba anapenda kunijibu bila sababu Nitakuja kumfanya mchemsho wa kutolea hangover
 
Ni kweli kabisa na ndio maana kwenye mithali 4:23 Tuliambiwa tulinde mioyo yetu....
Sema Kuna muda akili zetu zinakuwa kama zimevurugwa kutokana na childhood Traumas +Hard knocking life pamoja na chaos zinazoletwa na utandawazi.... n.k Hakika usipokuwa makini ndio pale unajikuta unapata suicidal thoughts .
 
Wanasema an idle brain is a carpentry of a devil...! Mara nyingi ni vena kuziepusha bongo zetu kuangukia kuwa karakana za shetani
 
Wanasema an idle brain is a carpentry of a devil...! Mara nyingi ni vena kuziepusha bongo zetu kuangukia kuwa karakana za shetani
Kweli kabisa... Na ndio maana jamii za Asia kama china, Japan, Mongolia n.k. Meditation ni sehemu ya tamaduni zao kwa ajili ya kufanya Cleansing kwenye nafsi zao.
 
mjamzito,kwa nini?
Si vizuri kugombana na mwanamke mjamzito kwa sababu mabishano na ugomvi humsababishia msongo mkubwa wa mawazo (stress), ambao huachilia homoni za cortisol na adrenaline zinazoweza kudhuru afya yake na ya mtoto aliye tumboni. Kipindi cha ujauzito kinahitaji utulivu mkubwa wa akili na mwili ili kuhakikisha mtoto anakua vizuri
 
Hii nasikia unaweza kumsababishia miscarriage
 
Kweli kabisa... Na ndio maana jamii za Asia kama china, Japan, Mongolia n.k. Meditation ni sehemu ya tamaduni zao kwa ajili ya kunifanyia Cleansing kwenye nafsi zao.
Wengine hujiliwaza na mmea..lakini...Ina madhara ya mbeleni

Bangi ina kemikali inayoitwa THC (Tetrahydrocannabinol). Inapoingia mwilini, THC huchochea ubongo kuachilia homoni ya dopamine kwa kiwango kikubwa, hali inayomfanya mtumiaji kuhisi raha iliyopitiliza, mwili kulegea, na kusahau matatizo kwa muda. Huu ndio "utulivu wa uongo" unaowadanganya wengi.
5b304283-6ad3-4d32-a3f0-30d8a76c6a9e.jpeg
 
Back
Top Bottom