Fuatilia siasa za nchi mbalimbali Duniani, RAIS wa nchi anapokuwa katika miaka ya uongozi ambayo siyo ya uchaguzi uwezi kusikia kusifu na kumwabudu Kama ilivyo Tanzania
Hali inayoendelea nchini Kwetu inafanya baadhi ya Watu kuhoji labda wanaosema Wana imani na RAIS hawana Imani naye Bali wanachowaza kutumpaka mafuta Ili wateuliwe Tena na Tena. Wengi wa wanaokesha wakiimba Wana imani na Mhe. RAIS ni wale Watu ambao siyo wabunifu, siyo wachapa kazi, siyo viongozi wenye ueledi wala uwezo wakutenda Bali ni wale Watu wa bla bla.
Kitendo Cha Watu wasioweza kufikiri kukesha kusifu kunamfanya RAIS aonekane kama labda ameanza kampeni nje ya muda au Bado anao wapinzani wengi ambao hata kama watadhibitiwa ndani ya chama chake Bado Wana nguvu kubwa ya kumwkwamisha wakiowemo waombaji Hawa.
Kama Mhe. RAIS anataka kugombea 2025 ni lazima kuanzia Sasa aweke mbele Watu waliopo serious, apange safu ya Watu serious, afanye tathimini ya Hawa wanaomsifu je lengo lao ni madaraka au ni kweli wanazungumza kutoka moyoni, ajiuize mtangulizi wake si alisifiwa? Je Leo waliomsifu wapo naye kiroho?
Kiongozi Makini Kwa Karne ya dot com na utandawazi lazima awekeze Kufanya kazi na Watu productive katika Kila sekta kujiimarisha kupitia huduma Kwa Umma. Watu wanaipiga makofi Bungeni kuanzia hotuba inaanza Hadi inaisha si Watu wakuwaaminj Kwa sababu hata huko majimboni bila dola hakuna ushindi kwao. Mhe. RAIS change strategy, biashara ya kusifiwa imepitwa na wakati, piga marudfuku