Habari za Sabato!
Harakati na siasa ni kama mchezo wa Draft au wale wakulungwa wanacheza Chess games.
Mtu yeyote anayejua kucheza Draft kikamilifu basi harakati na siasa hazitamsumbua.
Kwenye Chess au Draft watu wengi huziona Kete.
Lakini sisi wabobevu hatuishui kuziona Kete kama kete.
Bali tunaona zaidi ya kete; tunaona
a) Kete
b) Njia zitakazopita kete.
c) mfumo utakaitumika..
Siasa nazo zipo hivyohivyo. Watu ndio Kete. Kwenye kete katika Draft au Chess kuna aina ya za kete ingawaje kete yoyote inapofanikiwa kufika mstari wa mwisho wa mpinzani wake hugeuka Mfalme/king.
Kuna King, malkia, farasi, kuhani na askari. Huo ni mchezo wa Chess.na kila kete inakazi na nguvu yake.
Sasa mlisema hamtaki kuchoshwa.
MO29 ilifanikiwa kwa asilimia 20% kutokana na muunganiko wa Team JPM na Chadema na kundi dogo la wanaharakati.
Tumesikia 7/7 yametangazwa mengine.
Lakini katika ubao wa Draft/Chess nikitazama kuna kete zisioni. Zimerudi nyuma au kuangushwa au kupunwa.
Team jpm ni kama imerudi nyuma. Au tunasema wapo inactive. Hii inafanya hamasa ya 7/7 kuwa chini.
Hata hivyo naona serikali kuna wakati inacheza au kusogeza kete za wanaoandaa 7/7 kwa kuisema sema kwani hiyo inaongeza awareness,kutoa taarifa kwa ambao hawakuwa wanajua au sio wafuatiliaji.
Katika Chess kuna kanuni isemayo unaruhusiwa kuangalia kete za mwenzako lakini ni mwiko kuzicheza.
Mimi sina jipya. Nimemaliza.
Nimetoka church hapa Mbezi Mwisho, sabato ilikuwa nzuri.
TaikonMaster
Kwa sasa Mbezi luis, Dar es salaam