Uchaguzi 2020 Je, kutokuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kunachangia kwa kiasi kikubwa kutokuwa na Uchaguzi usio Huru na wa Haki?

Uchaguzi 2020 Je, kutokuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kunachangia kwa kiasi kikubwa kutokuwa na Uchaguzi usio Huru na wa Haki?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
372
Reaction score
310
Tunapoelekea kipindi cha kampeni tuna tegemea hoja nzito haswa kutoka kwa wagombea wa upinzani kuhusu serikali ya awamu ya tano kushindwa kuweka mifumo ambayo ingewezesha tume huru ya uchaguzi kuwepo. Lazima tufahamu kwamba Tume Huru ya Uchaguzi ni shirika linalo jitegemea pamoja na kuwa na nguvu kazi isiyo na upendeleo wa aina yoyote kwa chama chochote na kwasababu hio ni kitu ambacho kingechukua muda mrefu ku andaa.

Vile vile kuwa na Tume Huru inge tulazimu kuwa na mchakato wa kupata katiba mpya kwanza, kitu ambacho kilizua mzozo mkubwa mara ya mwisho tulipo waweka washika dau wote kwenye meza. Tujaribu kadri ya uwezo wetu kuzuia hali ambayo ingeweza kujitokea ya serikali kujenga ghorofa kubwa la tume huru liki endeshwa na watu wale wale ambao wapo kwenye tume tuliyo nayo sasa hivi. Vile vile uchaguzi kwa mara ya kwanza na tume mpya ya uchaguzi ni kitu kinacholeta sinto fahamu kubwa na kinatu lazimu tuwe tume jiandaa kwa muda mrefu ku kabiliana na changa moto zozote.

Ni vyema pia kama tungeweza kuchambua faida na hasara zinazoweza kuhusishwa na kuwa na tume huru ya uchaguzi. Faida kubwa kuliko zote ni vyama vyote vya siasa vitakuwa na imani kwamba uchaguzi utakuwa wa huru na wa haki kwasababu uchaguzi utasimamiwa na watu wasio na upendeleo.

Kitu cha muhimu ambacho washika dau wote wanashindwa kutambua ni kwamba tume huru ya uchaguzi inge andaliwa na serikali hii hii ambayo inasemekana kuwa na mkono kwenye tume tuliyo nayo sasa hivi. Watakaofanya kazi kwenye tume huru ya uchaguzi bado wangechaguliwa na serikali na hamna chama chochote ambacho kingekuwa na wa wakilishi kwenye tume.

Muda sio rafiki kwa kila mtu na kwasababu hio ni muhimu kwa wahusika wa vyama vyote kurekebisha tofauti zao na tume iliyopo sasa hivi na kuangalia jinsi walivyo jiandaa kwa uchaguzi.

Kuwa na historia ya kufanya kazi kwa uadilifu, uwezo wa kufanya kazi vizuri na vyombo vya usalama vilivyopo na mahusiano mazuri na watanzania wote kwa ujumla ni vitu ambavyo vinachukua muda kujenga. Tume ya uchaguzi inazingatia maslahi ya wagombea wote
 
Ndio nina fahamu. Tofauti ya tume huru na tume tuliyo nayo sasa hivi ni kwamba tuna imani kuwa tume huru ina uwezo wa ku simamia uchaguzi kwa ufasaha zaidi na bila upendeleo
Kwahiyo hichi ulichoandika hapa ndiyo uelewa wako kuhusu TUME HURU YA UCHAGUZI ???
 
Naomba uni julishe tofauti kati ya tume huru ya uchaguzi na tume isiyo huru
Mimi nataka kujifunza kwako wewe mtaalamu halafu naona umeelezea kwa kifupi sana.
Hivi waliotaka kuwepo na Tume huru ya Uchaguzi nini hasa yalikuwa mapendekezo yao ??
Wanataka hiyo tume ya uchaguzi iwe ya namna gani na ya muundo upi ??
Hivi sehemu nyingine duniani tume huru zimesaidia kwenye chaguzi zao ??
 
Sifahamu mapendekezo yao ya muundo wa tume ila ninacho fahamu ni kwamba serikali inaweza ikasikiliza mapendekezo ya kila mtu ila maamuzi ya mwisho yatabaki kwa serikali. Vyama vya siasa haviwezi kuruhusiwa kuchagua wanao simamia uchaguzi
 
Kwahiyo umeamua kuwashauri ilhali hufahamu fika kwamba wao wanataka nini ???
 
Hebu acha kuandika UJINGA!!! Marehemu Mkapa angekuwa anaamini kwamba hii tume ni huru kulikuwa na sababu gani ya yeye kutaka kuwepo kwa tume huru?

1596596115156.jpeg

Nime washauri kutokana na uelewa wangu. Kama na wewe una mchango, changia kama wana JF wengine
Wala hujakosea kutoa mchango wako ndugu yangu, lakini nadhani ingekuwa ni busara zaidi kama ungesikiliza upande wa pili unataka nini kisha ukaja kutoa ushauri kama huu hapa jukwaani. Tume Huru ni swala nyeti ambalo linaweza kuathiri mustakabali wa vitukuu vyako, hivyo tuwe makini sana tunapoamua kuchangia mada nzito kama hizi. Haya ndiyo maoni yangu kwako mkuu. Uwe na siku njema!
 
Hebu acha kuandika UJINGA!!! Marehemu Mkapa angekuwa anaamini kwamba hii tume ni huru kulikuwa na sababu gani ya yeye kutaka kuwepo kwa tume huru?
Naamini kuna umuhimu wa kuwa na tume huru ila leo ni tarehe 5 mwezi wa 8 mwaka 2020. Una mapendekezo gani?. Na hata baada ya uchaguzi kuna tofauti gani kati ya tume huru na tume isiyo huru?
 
Mapendekezo yangu na ya Watanzania wengi kuwe na UWAZI wa kuhesabu kura na pia zihesabiwe hadharani.

1596596313914.jpeg

Naamini kuna umuhimu wa kuwa na tume huru ila leo ni tarehe 5 mwezi wa 8 mwaka 2020. Una mapendekezo gani?. Na hata baada ya uchaguzi kuna tofauti gani kati ya tume huru na tume isiyo huru?
 
Attachments

  • D56B8664-50D1-4BCB-A640-5B8B6FC438C5.jpeg
    D56B8664-50D1-4BCB-A640-5B8B6FC438C5.jpeg
    62.9 KB · Views: 1
Wala hujakosea kutoa mchango wako ndugu yangu, lakini nadhani ingekuwa ni busara zaidi kama ungesikiliza upande wa pili unataka nini kisha ukaja kutoa ushauri kama huu hapa jukwaani. Tume Huru ni swala nyeti ambalo linaweza kuathiri mustakabali wa vitukuu vyako, hivyo tuwe makini sana tunapoamua kuchangia mada nzito kama hizi. Haya ndiyo maoni yangu kwako mkuu. Uwe na siku njema!
Nina elewa kwamba itafikia kipindi ambacho ita tulazimu kuwa na tume huru ila kwa sasa hivi ni muhimu kufahamu mapendekezo ya washikadau wengine ni yapi na tume huru zingine duniani zina fanya kazi ki vipi?
 
Sasa hili wewe kama msomi ndiyo inabidi ukalifanyie utafiti wako binafsi!
 
Uchaguzi "huru na wa haki" ni Uchaguzi wa namna gani?

Kwa mujibu wa maelezo yako,
Tunawezaje kuuhakikisha uhuru wa tume ambayo msingi wake ni kiongozi ambaye naye ni miongoni mwa wagombea katika chama kinachoshiriki huo Uchaguzi?
 
Je lazima kuwe na mabadiliko ya katiba ili tume huru iundwe?. Hilo lita chukua muda gani?. Nani ana husika katika ku andaa tume huru? Orodhesha tofauti kati ya tume huru na tume tuliyo nayo sasa hivi
 
Back
Top Bottom