Uchaguzi 2020 Je, kutokuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kunachangia kwa kiasi kikubwa kutokuwa na Uchaguzi usio Huru na wa Haki?

Uchaguzi 2020 Je, kutokuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kunachangia kwa kiasi kikubwa kutokuwa na Uchaguzi usio Huru na wa Haki?

Pascal unachekesha, eti Magu ametuhakikishia? Je unajua Magu naye ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM na huyo ndiye aliyeichagua hiyo tume? Je, najua wasimamizi wa uchaguzi wengi wao ni makada wa CCM

Na mwisho unajua vema anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo.
Nakubaliana na wewe jambo moja tu, ili tume iwe huru lazima iwe shirokishi na wajumbe wasiteuliwe na mgombea wa upande mmoja.

Hakuna fair play kwenye mechi ambayo timu inayoshiriki kocha wao ndiye anachagua marefa na kamisaa wa mchezo.
 
Tunapoelekea kipindi cha kampeni tuna tegemea hoja nzito haswa kutoka kwa wagombea wa upinzani kuhusu serikali ya awamu ya tano kushindwa kuweka mifumo ambayo ingewezesha tume huru ya uchaguzi kuwepo. Lazima tufahamu kwamba Tume Huru ya Uchaguzi ni shirika linalo jitegemea pamoja na kuwa na nguvu kazi isiyo na upendeleo wa aina yoyote kwa chama chochote na kwasababu hio ni kitu ambacho kingechukua muda mrefu ku andaa.

Vile vile kuwa na Tume Huru inge tulazimu kuwa na mchakato wa kupata katiba mpya kwanza, kitu ambacho kilizua mzozo mkubwa mara ya mwisho tulipo waweka washika dau wote kwenye meza. Tujaribu kadri ya uwezo wetu kuzuia hali ambayo ingeweza kujitokea ya serikali kujenga ghorofa kubwa la tume huru liki endeshwa na watu wale wale ambao wapo kwenye tume tuliyo nayo sasa hivi. Vile vile uchaguzi kwa mara ya kwanza na tume mpya ya uchaguzi ni kitu kinacholeta sinto fahamu kubwa na kinatu lazimu tuwe tume jiandaa kwa muda mrefu ku kabiliana na changa moto zozote.

Ni vyema pia kama tungeweza kuchambua faida na hasara zinazoweza kuhusishwa na kuwa na tume huru ya uchaguzi. Faida kubwa kuliko zote ni vyama vyote vya siasa vitakuwa na imani kwamba uchaguzi utakuwa wa huru na wa haki kwasababu uchaguzi utasimamiwa na watu wasio na upendeleo.

Kitu cha muhimu ambacho washika dau wote wanashindwa kutambua ni kwamba tume huru ya uchaguzi inge andaliwa na serikali hii hii ambayo inasemekana kuwa na mkono kwenye tume tuliyo nayo sasa hivi. Watakaofanya kazi kwenye tume huru ya uchaguzi bado wangechaguliwa na serikali na hamna chama chochote ambacho kingekuwa na wa wakilishi kwenye tume.

Muda sio rafiki kwa kila mtu na kwasababu hio ni muhimu kwa wahusika wa vyama vyote kurekebisha tofauti zao na tume iliyopo sasa hivi na kuangalia jinsi walivyo jiandaa kwa uchaguzi.

Kuwa na historia ya kufanya kazi kwa uadilifu, uwezo wa kufanya kazi vizuri na vyombo vya usalama vilivyopo na mahusiano mazuri na watanzania wote kwa ujumla ni vitu ambavyo vinachukua muda kujenga. Tume ya uchaguzi inazingatia maslahi ya wagombea wote
Hiyo tittle tuu imemaliza uzi wako wote inajieleza.
 
Wasalaam, ukweli ulio wazi ni kwamba tume ya uchaguzi ni dhaifu kwa sababu;
1. Viongozi wake wote ni makada watiifu na waaminifu wa ccm.
2. Viongozi wote wa NEC wameteuliwa na m/kiti wa ccm taifa ndugu magufuli.
3. Viongozi wote wa NEC wanawajibika kwa mwenyekiti wa ccm taifa.
4. Viongozi hawa wamepokea maelekezo maalum kuhakikisha wagombea wa ccm wanapita kwa njia za panya(wizi wa kura) na kutangazwa washindi.

Kwa tume hii ya uchaguzi dhaifu inayopendelea upande mmoja natabiri ccm itashinda kwa kishindo Oct 28.
 
Siku hizi hakuna anayeweza kukuchukulia serious hasa baada ya kwenda kugombea nafasi ya ubunge na kuambulia kura ya mjumbe mmoja mlevi.

Wewe hujui Magufuli ni Double Standard, anasema maendeleo hayana chama na wakati huohuo anawashangaa wananchi wanaowapigia kura wapinzani.!! What is that.

Ccm kwa jinsi walivyochokwa na watu hawawezi kuacha kuiba kura na wasipoiba lazima watashindwa tu. That's for sure.
 
NEC siyo huru kutokana na sababu zifuatazo mkuu:-
1. Uteuzi wa wajumbe wa tume siyo wa wazi( open & transparent) kwa sababu huwa hawatangazwi gazetini wala vyombo vingine.
2. Hakuna sheria inayozungumzia jinsi ya kupata tume huru. katiba inaeleza tume inauundwa na watu gani(composition) na siyo namna ya kuwateua/uteuzi wa wakumbe(Manner of appointment). Hapa panaondoa uhuru wa tume(NEC). Chini ya katiba wajumbe wote huchaguliwa na mtu ambaye ni mgombea katika uchaguzi. Hapa huwa ni kinyume na haki asilia(rule of natural justice hasa katika "biasness".)
 
Back
Top Bottom