Uchaguzi 2020 Je, kutokuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kunachangia kwa kiasi kikubwa kutokuwa na Uchaguzi usio Huru na wa Haki?

Pascal unachekesha, eti Magu ametuhakikishia? Je unajua Magu naye ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM na huyo ndiye aliyeichagua hiyo tume? Je, najua wasimamizi wa uchaguzi wengi wao ni makada wa CCM

Na mwisho unajua vema anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo.
Nakubaliana na wewe jambo moja tu, ili tume iwe huru lazima iwe shirokishi na wajumbe wasiteuliwe na mgombea wa upande mmoja.

Hakuna fair play kwenye mechi ambayo timu inayoshiriki kocha wao ndiye anachagua marefa na kamisaa wa mchezo.
 
Hiyo tittle tuu imemaliza uzi wako wote inajieleza.
 
Wasalaam, ukweli ulio wazi ni kwamba tume ya uchaguzi ni dhaifu kwa sababu;
1. Viongozi wake wote ni makada watiifu na waaminifu wa ccm.
2. Viongozi wote wa NEC wameteuliwa na m/kiti wa ccm taifa ndugu magufuli.
3. Viongozi wote wa NEC wanawajibika kwa mwenyekiti wa ccm taifa.
4. Viongozi hawa wamepokea maelekezo maalum kuhakikisha wagombea wa ccm wanapita kwa njia za panya(wizi wa kura) na kutangazwa washindi.

Kwa tume hii ya uchaguzi dhaifu inayopendelea upande mmoja natabiri ccm itashinda kwa kishindo Oct 28.
 
Siku hizi hakuna anayeweza kukuchukulia serious hasa baada ya kwenda kugombea nafasi ya ubunge na kuambulia kura ya mjumbe mmoja mlevi.

Wewe hujui Magufuli ni Double Standard, anasema maendeleo hayana chama na wakati huohuo anawashangaa wananchi wanaowapigia kura wapinzani.!! What is that.

Ccm kwa jinsi walivyochokwa na watu hawawezi kuacha kuiba kura na wasipoiba lazima watashindwa tu. That's for sure.
 
NEC siyo huru kutokana na sababu zifuatazo mkuu:-
1. Uteuzi wa wajumbe wa tume siyo wa wazi( open & transparent) kwa sababu huwa hawatangazwi gazetini wala vyombo vingine.
2. Hakuna sheria inayozungumzia jinsi ya kupata tume huru. katiba inaeleza tume inauundwa na watu gani(composition) na siyo namna ya kuwateua/uteuzi wa wakumbe(Manner of appointment). Hapa panaondoa uhuru wa tume(NEC). Chini ya katiba wajumbe wote huchaguliwa na mtu ambaye ni mgombea katika uchaguzi. Hapa huwa ni kinyume na haki asilia(rule of natural justice hasa katika "biasness".)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…