Napinga hilo na haifai kumwita ana pepo la uzinzi! Kuna tukio moja nililishughulikia lililonishawishi pengine ni salama vijana kukutana angalau mara moja kabla ya ndoa kujiridhisha kila mmoja yupo sawa.
Ilikuwa hivi; Binti alikutana na kijana tangu akiwa kidato cha pili na kujikuta wakiwa wachumba. Kijana alimshawishi mwenzie akajitambulishe rasmi kama mchumba kwa ahadi wataoana pindi Binti atakapomaliza shule. Wazazi walimkubalia kijana na kijana alikuwa akimimina zawadi nzito nzito kwa Binti na wazazi, na ilifika wakati walikuwa wakiruhusiwa kutoka wote na kusafiri hadi Arusha, Tanga na Mwanza. Binti anasema kila walipofanya romance na Binti kupandisha mzuka kijana alimsihi atulie kwani ipo siku atachoka mwenyewe.
Alopofaulu kwenda F5 Binti alikuwa anataka kuacha kuendelea na masomo ili aolewe kwanza lakini kijana alimsisitizia amalizie kidato cha sita na hata shahada kwani hakuwa na haraka. Alimnunulia Baba mkwe gari pick up kama zawadi kwa Binti kufanya vizuri kimasomo.
Uhusiano sasa ulikuwa karibu zaidi Binti akienda kukaa kwa mchumbawe hadi wiki nzima au zaidi lakini kila alipombembeleza mwenzie wafanye alikataa katakata akidai wakifanya watachokana na anaweza badili mawazo! Binti alilipeleka shauri kwa mama na kukaripiwa vikali kwamba yule ndiye mchumba sahihi maana hataki kumchezea!
Matokeo ya kidato cha sita hayakuwa mazuri sana kwa hiyo ilibidi waoane licha ya kijana kupiga kifua angemsomesha kwa gharama. Binti alikataa katakata kwa hiyo ilibidi ndoa ifungwe.
Kijana alianza kuonyesha mambo yamemshinda kuanzia wakiwa kwenye honeymoon, ambapo aliendelea kusisitiza eti kule ni sehemu ya kufanya tafakari ya maisha yao kiroho!
Kuona hivyo Binti alidai warudi nyumbani na mambo yalikuwa kama siku zote, kijana akihangaika na kumwingiza madole na kumyonya ulimi bila ya tendo. Binti alivumilia hadi mwaka ambapo mwaka wa pili alipata mchepuko na kuhakikisha anapata mimba potelea mbali litakalotokea, ajabu kijana alifurahi sana kwa mkewe kupata mimba, akaita marafiki na kufanya kijisherehe! Mtoto alizaliwa akifanana sana na mama na kijana aliwapenda mno mtoto na mama. Mtoto alipofika miaka mitatu mama alihitaji mtoto tena, alimhimiza mwenzie akatibiwe na haikupita nafuu licha ya kwenda hadi India! Mama atapata mimba ya mchepuko mwingine ambao kijana alikubali kama kwanza. Mtoto wa pili alipofika miaka mitatu mama aliamua kuweka mambo hadharani ambapo baada ya mvutano mkali kanisa liliibatilisha ndoa na kuitengua lakini kijana alibaki na watoto wake!