Je, kwa hii kauli ya Papa, ameruhusu au amekataza ushoga??

Je, kwa hii kauli ya Papa, ameruhusu au amekataza ushoga??

Hivi karibuni Vatikani imeidhinisha wanaume mashoga kuwa mapadre iwapo wanaume hao watakuwa hashiriki tendo la ndoa.

Ingawa kanisa hilo halikuwahi kukataza wapenzi wa jinsia moja kuwa mapadri, mwaka 2016 Vaticn ilikataza wanaume wenye tabia kama hizo kuwa viongozi au mapadri

=====================================================
The Vatican has given the green light for gay men to become priests - as long as they remain celibate.

In an unexpected adjustment to practice in the Catholic Church, the new guidelines from Italian bishops will allow gay men to enter

Although the Vatican had not explicitly prohibited gay men from entering the priesthood in the past, an instruction from 2016 barred men who have "deep-seated homosexual tendencies".

The new guidelines, approved by Italian bishops, say seminary directors should consider a priestly candidate's sexual preferences, but only as one aspect of their personality.

"When referring to homosexual tendencies in the formation process, it is also appropriate not to reduce the discernment to this aspect alone, but … to understand its meaning within the whole framework of the young person's personality," the guidelines say.

Pope Francis, who has been pontiff since 2013, has been viewed by some as having taken a more welcoming approach towards the LGBTQ+ community.

This has included allowing priests to bless same-sex couples on a case-by-case basis - but the admittance of gay men into the priesthood has remained a taboo subject

Source: Sky News
Dini nyingine zimekuja kuleta laana tu duniani sasa shoga awe kiongozi si mtafungishwa ndoa za wanaume kwa wanaume ma kanisani🤔
 
Mashoga ni binadamu kama ulivyo wewe, kubali kataa ninyi nyote ni wa Mungu na anawapenda na kuwapa yaliyo sawa.
Jua likiwaka lenu nyote, mvua ikinyesha yenu wote, pumzi kawapa wote.

Utawahukumu hapa lakini wakitubu na kumrudia Muumba atawasamehe na kuwasafisha.

Yesu alikuja duniani kwa ajili ya watu wa namna hiyo, wapeni nafasi, kaeni karibu nao kama Yesu alivyofanya kukaa na wadhambi.
Kichaa akiwa wa jirani haisimbui,omba asiwe mtu wa karibu yako haya maneno utarudi kuyafuta.
 
Kichaa akiwa wa jirani haisimbui,omba asiwe mtu wa karibu yako haya maneno utarudi kuyafuta.
Maneno gani ya kufutwa hapo??
Akiwa wa karibu yako utamuua au utamsaidia aache kama nilivyoandika??
Wengi wenu hamna maamuzi juu ya hilo suala.
 
.
Ungeacha papara na kusoma ujumbe wangu vizuri ungenielewa. Wapi nimeonesha chuki? Vipi na wale wanaosema mashoga wauwawe, kati ya hao na mimi ninaesema waombewe nani anatangaza chuki?
.
Acha stereotyping...jifunze kujiamini mzee sio kila hoja inayotolewa ikiwa tofauti na mawazo yako basi watu wanakuchukia.
Ushaanza mihemko.
 
Kama Yesu Kristo angeliweza kuwakubali ni nani wa kuwakataa?watu hufikiria kuwa pengine watu kama hawa wangestahili kuuawa wasiwepo kabisa duniani(sitetei ushoga).lakini tukiwa kama wakristo tunapaswa kuwaombea watu wote wanaotenda dhambi ili Mungu awarehemu .Wewe unayewazungumza vibaya mashoga bado unazini,ni mwizi,unacheat na wake za watu,muuaji,mshirikina na wote kimsingi mnakuwa na destiny moja na mashoga.Tukiwa kama wakristo tunalo jukumu kubwa la kuwaongoza wengine kwenye njia ya kweli na kuwapenda kwa dhati.
 
Mashoga ni binadamu kama ulivyo wewe, kubali kataa ninyi nyote ni wa Mungu na anawapenda na kuwapa yaliyo sawa.
Jua likiwaka lenu nyote, mvua ikinyesha yenu wote, pumzi kawapa wote.

Utawahukumu hapa lakini wakitubu na kumrudia Muumba atawasamehe na kuwasafisha.

Yesu alikuja duniani kwa ajili ya watu wa namna hiyo, wapeni nafasi, kaeni karibu nao kama Yesu alivyofanya kukaa na wadhambi.
Kutubu hakuendi hivyo,yaani we ufanye kosa kimakusudi na wajua kabisa ni chukizo kubwa mbele ya muumba,kisa tu eti nitatubu na yataisha!!, Na je ukikutwa na mauti kabla ya kutubu,utajibu nini siku ya mwisho,usipende kurahisisha mambo mazito kuwa mepesi!!
 
Kwahiyo unatubu kwa kosa ambalo umefanya na hujui kua ni kosa??
Sasa utatubu vipi ilhali kila kosa unalojua ni kosa hulifanyi?? Au ninyi ndio wale mnaitwa watakatifu sijui wenye kheri ??
 
Back
Top Bottom