kikoozi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2015
- 2,184
- 3,221
Habarini ndugu zangu, poleni na majukumua ya hapa na pale, niende moja kwa moja kwenye mada ya andiko hili
nipo na mpenzi wangu, ni mwaka wa 4 sasa na nimepanga kama mungu akijaalia nimuoe mwakani mwishoni, uyu binti nampenda sana sana na tumepitia ups and down za hapa na pale ila kwa ili naomba niwashirikishe kidogo.
Nili note baadhi ya mabadiliko ya hapa na pale katika communication kati yangu mimi na yeye, baada ya kumuuliza kama kuna shida akadai kuwa hakuna shida yeyote (niliona amebadilika tofauti na nilivyo mzoea ndio maana nilimuuliza), akawa ni mgumu sana wa kunitafuta kwa simu mpaka nimuanze mimi (ni kitu kilichoanza ghafla tu maana kwa kawaida lazima tutafutane kila siku asubuhi na jioni kabla ya kulala),
Baada ya kuona mwenzangu amebadilika hayupo sawa sawa na nikimuuliza anadai yupo sawa tu hakuna tatizo lolote na upande wa communication naona kama mimi ndio natumia nguvu nyingi sana kumtafuta wakati mwanzoni haikuwa ivyo kwa upande wangu nikaamua kuchukua maamuzi kama ifuatavyo, "nikajiwekea msimamo wa kutomtafuta tena, kama anaona namfaa basi atanitafuta yeye"-----msimamo huu niliauanza jumatano ya week hii inayoisha leo
Note: kiukweli nampenda sana, ata huo msimamo nimeuweka kwa kujikaza sana sana.
Alihamisi asubuhi alitafuta yeye kwa salamu tu whatsup......nami nilimuhitikia vizuri na kumjibu kama vile hakijatokea kitu
Ijumaa pia alinitafuta tena.......tunasalimiana tu ila sio kwa maongezi malefu (conversation ndefu za sms kama kipindi cha mwanzo)
Jumamos ya jana hakunitafuta, nami sikumtafuta kabisaa siku nzima
Leo jumapili hakunitafuta na mimi pia sijamtafuta mpaka muda huu
kwa upande wangu nahisi upweke wa ghafla tu umenijia, natamani kumtafuta ila nahisi kama amenidhalau,
moyo unanishawishi nimtafute ila akili inagoma kabisa.
naomba waungwana, waliovuka iki kiunzi maana kama kumpenda nampenda na nahisi msimamo nilioweka unaniumiza mimi ebu nisaidieni mawazo yenu wakuu.
huu msimao ni tiba au ni kuchochea moto.?