Je, kwanini ni ngumu kwa Nyoka kuwa ng'ata watoto wadogo?

Je, kwanini ni ngumu kwa Nyoka kuwa ng'ata watoto wadogo?

Mwaka 2000 wanafamilia tulipatwa na hofu mara baada ya kumuona mdogo wetu aliyekuwa na umri wa miaka 2 akimshika kobra('Nyamwilu' kwa kihehe),kisha kumvuta mkia huku akisema "Mama inzagala yigenda" kwa tafsiri ya Kiswahili kisicho fasaha ni "Mama kuni inatembea".
Babu yetu akatuambia msimsogelee hawezi kumdhuru. Na mwishowe yule nyoka aliishia kumnusa tu na kutokomea porini.
Hata kwetu ilikuwa hivo hivo.. sema dogo alisema mama kuni inaingia shimoni
 
Sio kweli inategemea kama mtoto atamshambulia nyoka, sikuzote nyoka mashambulizi yake ni kwa adui na mawindo ya chakula haijalishi ni nani.

Nyoka anaweza kushambulia yoyote yule hana formula kwamba ni mtoto au mtu mzima inategemea na aina ya nyoka, mazingira, na vitisho vya mtu kwa nyoka.

Asante sana
Safi sana
 
Kuna clips nyingi Mitandaoni huonyesha watoto wadogo wakichezea kiumbe hatari .....aka Mr snake iwe koboko au wengine mara nyingi watoto wanakuwa unharmed na hao Nyoka Je sababu

Haya ni baadhi ya majibu yasiyo rasmi
"Nyoka anakudhuru kwa harufu unayoitoa unaposhikwa woga ambayo yeye anajua tayari huyu ni adui mbona amestuka sasa mtoto hatoi hiyo harufu maana hakuna yoga ndani yake wakati huo anaona ni rafiki wa kucheza nae[emoji54] eeeeh sina uhakika sana"
Je kisayansi hii Ina maanisha nn???View attachment 3375969

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Mtoto akimuona mnyama au mdudu humchukulia kama rafiki hawazi kumdhuru vivyo hivyo kwa mnyama pia hawezi kumdhuru kiumbe ambacho hakina habari (hata mtu mzima akiwa amelala hawezi kung'atwa) ila mtu mzima lazima aogope na awaze kumdhuru vivyo hivyo mnyama lazima ajihami kwa kung'ata au kushambulia.
 
Mtoto mdogo ambaye hajaota meno hang'atwi na nyoka.

Niliwahi kumkuta mdogo wangu anayenifuata akiwa anacheza na nyoka na nyoka yule hakumdhuru,wakati huo alikuwa bado hajaota meno.
Hata mama mjamzito
 
Hizo ni hekaya tu. Nyoka wanaua watoto kama kawaida.

Kinachopelekea nyoka kukushambulia ni pale anapohisi wewe ni hatari kwake.

Kwahiyo kama mtoto mdogo ataonekana kuwa tishio kwa nyoka, basi nyoka huyo atashamshambulia.

Kwa mfano akimshika mkia na kumvuta wakati nyoka anajaribu kuchoropoka na kukimbia, nyoka huyo atageuka na kumshambulia mtoto.
 
Hizo ni hekaya tu. Nyoka wanaua watoto kama kawaida.

Kinachopelekea nyoka kukushambulia ni pale anapohisi wewe ni hatari kwake.

Kwahiyo kama mtoto mdogo ataonekana kuwa tishio kwa nyoka, basi nyoka huyo atashamshambulia.

Kwa mfano akimshika mkia na kumvuta wakati nyoka anajaribu kuchoropoka na kukimbia basi nyoka atageuka na kumshambulia mtoto.
Kwann nyoka anakimbia ukimshika mkia
 
Ulikua unazidisha uchokozi wako,lkn pia inategemea na jinsi mnavyomtunza huyo paka.
Mfano,paka hapewi chakula nyumbani kwa madai kwamba anajitafutia,hapo huyo hafugwi,bali anazengea tu kwa hiyo hakuna kuzoeana.
Kwetu wanyama huwa tunawaangalia vizuri tu. Sema kitu nilichokuwa nafanya ni kumshtukiza kama amekaa sehemu kalala nakwenda na kumshika huku nipiga kelele ''puuuuu''. Au kwa bahati mbaya nakanyaga mkia wake wakati anakula.
 
Kuhusu harufu ni sahihi kabisa, kitaalam inaitwa adrenaline hormone. Hio huzalishwa nyingi pale mtu unapotaharuki wakati wa kukabili changamoto ya papohapo.

Ndimi mbili anazotoa nje nyoka ndizo hu-sense hio harufu na taarifa hiyo kutafsiriwa na 'Jacob's organ' iliyo sehemu ya juu ndani ya kinywa chake. Hapo hutafsiriwa kama hatari na nyoka kuchukua hatua ya ku-bite kama mbinu ya kujilinda.

Kuhusu maamuzi ya nyoka kung'ata sio kipaumbele chake , ni kweli kabisa. Nyoka kuamua kung'ata ni maamuzi ya mwisho kabisa baada ya jitihada zote za kumuepuka adui/subject zimegonga mwamba. Kwanini?

Kwasababu sumu ya nyoka ni pure protein, hii humuitaji kula mawindo yenye protein zaidi kitu ambacho humghalimu na kuchukua muda mrefu.
Sumu yake inamsaidia zaidi katika mawindo japo anaitumia pia kujilinda.

La ziada,

Gently handling.
Jinsi mtoto anavomshika nyoka na reaction za mtoto ni gently/friendly zaidi hivyo ukijumlisha na utulivu wa kiwango Cha hormones basi nyoka anafeel safety sense.

Angalizo,

Nyoka wengi hawana sumu na wachache pekee ndio wenye sumu. Katika hao wachache wenye sumu tuna black mamba/koboko. Huyu Huwa anaitafuta shari mwenyewe, hasubiri upite karibu yake au umkanyage ndio ashambulie.

Ndani ya 20mita Hadi 50mita (social distance) kuzunguka eneo lake akihisi uwepo wa kitu chochote anachoweza tafsiri kama threat/tishio basi yeye huanza msako.
Ana Sumu Kali na ndani na nusu saa bila msaada wa haraka kupoteza maisha ni njenje.

Ushauri.

Ikitokea umegongwa na nyoka au ndugu yako, jitahidi kukalili muonekano wake ikiwezekana muue kusaidia utambuzi wa aina ya sumu na tiba yake.
 
Mwaka 2000 wanafamilia tulipatwa na hofu mara baada ya kumuona mdogo wetu aliyekuwa na umri wa miaka 2 akimshika kobra('Nyamwilu' kwa kihehe),kisha kumvuta mkia huku akisema "Mama inzagala yigenda" kwa tafsiri ya Kiswahili kisicho fasaha ni "Mama kuni inatembea".
Babu yetu akatuambia msimsogelee hawezi kumdhuru. Na mwishowe yule nyoka aliishia kumnusa tu na kutokomea porini.
Duuuuh bila shaka Hali ilikuwa tete

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Nyoka angekuwa na uwezo wa kumgonga/kumdhuru mtoto aliyeko tumboni angemdhuru.
Nashangaa mnavyodanganyana kuwa nyoka ni rafiki wa watoto.

Monetary doctor
 
Back
Top Bottom