Je, kwanini ni ngumu kwa Nyoka kuwa ng'ata watoto wadogo?

Je, kwanini ni ngumu kwa Nyoka kuwa ng'ata watoto wadogo?

Kihusu ushari wa koboko nakubaliana na wewe. Lakini huwa hashambulii kila wakati.
Nakumbuka mwaka 2017, nilikuwa na mzee tukielekea mashambani, basi mimi sina hili wala lile; nikashangaa mzee kanizuia kwa mkono pasi na kusema chochote. Akaniashiria niangalie mbele na nisigeuke. Bonge la joka la kijivu na kichwa chake kidogo, urefu wake ni kama mita 3 au 4 hivi kilichochongoka! lilikuwa limeinua nusu ya kiwiliwili chake likifanya scanning kwenye nyuso zetu. Lilipoona tumetulia likashusha kiwiliwili chake na kuondoka kwa kasi ya ajabu mithili ya risasi. Huyo kule uheheni tunamuita Nyamuhandu, ninyi wazungu mnamuita black mamba.
Rest in peace mzee, uliniokoa siku ile.
Hongereni, ni jambo la kumshukuru Mungu .

Mzee wako aliapply kanuni ya kiusalama nyikani/porini. R I P.

Ipo hivo ndiomana tunasahuriwa ukihisi ubaridi wa ghafla sehemu fulani ya mwili basi usikurupuke, kaza. Huyo ni nyoka ataondoka na kama umelala basi inahitaji moyo na uvumilivu kidogo maana nae anapenda joto.

Kujitingisha kwa namna yeyote inampa go ahead ya kukubite.

Hii kanuni inashauliwa hata kwa jamii nyingine za wanyama wa mwitu japo si wakati wote itakuhakikishia usalama wako. Namaanisha kusimamia still.

Lakini umepata picha halisi yakwamba mliinga ndani ya social distance yake ndio maana akafanya search. Hakuibuka bahati mbaya na alichokuwa anajiridhisha pale ni kwamba wewe ni kiumbe hai au ni kitu mathalani mti. Pale hapimi dhamira yenu hapana.

Ni kweli pia huyu black mamba anauwezo wa kusimamia hadi usawa wa nusu Hadi robo tatu ya urefu wake.

Safi umepata uzoefu wa kuvutia japo ni hatari.
 
Mwaka 2000 wanafamilia tulipatwa na hofu mara baada ya kumuona mdogo wetu aliyekuwa na umri wa miaka 2 akimshika kobra('Nyamwilu' kwa kihehe),kisha kumvuta mkia huku akisema "Mama inzagala yigenda" kwa tafsiri ya Kiswahili kisicho fasaha ni "Mama kuni inatembea".
Babu yetu akatuambia msimsogelee hawezi kumdhuru. Na mwishowe yule nyoka aliishia kumnusa tu na kutokomea porini.
😄😄😄😄 Kuni inatembea ebwanaee hii Aina TOFAUTI na Yale mavifuu yanatembea.


Ilikuwaje? Dogo katika kucheza cheza ikabidi aanze kuokota vifuuu Ebwana eh katika process si akaokota na makobe SASA ila anatua mzigo akaona mengine ya move NI kasikia mjomba mavifuu yanatembea mbona nilichoka
 
Watoto wana utukufu = Nuru
Watu wazima = Ushetani.

Tangu lini nuru na giza vikachangamana?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
A baby is born good (pure) but is getting defiled by the environment (people around it) in the course of it's life.
 
Kuna clips nyingi Mitandaoni huonesha watoto wadogo wakichezea kiumbe hatari aka Mr snake iwe koboko au wengine mara nyingi watoto wanakuwa unharmed na hao Nyoka. Je, sababu ni nini?

Haya ni baadhi ya majibu yasiyo rasmi

Nyoka anakudhuru kwa harufu unayoitoa unaposhikwa woga ambayo yeye anajua tayari huyu ni adui mbona amestuka sasa mtoto hatoi hiyo harufu maana hakuna yoga ndani yake wakati huo anaona ni rafiki wa kucheza nae

Eeeeh sina uhakika sana!!

Je kisayansi hii Ina maanisha nini?

View attachment 3375969
Watoto ni malaika hawana dhambi
 
Ufahamu walionao watoto ni tofauti na ufahamu alionao mtu mkubwa.

Mtoto anajua kila kitu ni chema, wakati wakubwa wanajua kuna mema na mabaya.

Mtoto akiona nyoka ata-react kama rafiki yake... Wakati mkubwa abamuona nyoka kama adui yake.
Nyoka ana-respond kulingana na ulivyokuja.
Daaah kumbe

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Kihusu ushari wa koboko nakubaliana na wewe. Lakini huwa hashambulii kila wakati.
Nakumbuka mwaka 2017, nilikuwa na mzee tukielekea mashambani, basi mimi sina hili wala lile; nikashangaa mzee kanizuia kwa mkono pasi na kusema chochote. Akaniashiria niangalie mbele na nisigeuke. Bonge la joka la kijivu na kichwa chake kidogo, urefu wake ni kama mita 3 au 4 hivi kilichochongoka! lilikuwa limeinua nusu ya kiwiliwili chake likifanya scanning kwenye nyuso zetu. Lilipoona tumetulia likashusha kiwiliwili chake na kuondoka kwa kasi ya ajabu mithili ya risasi. Huyo kule uheheni tunamuita Nyamuhandu, ninyi wazungu mnamuita black mamba.
Rest in peace mzee, uliniokoa siku ile.
Haukuonyesha umwamba???[emoji23]

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom