Kuhusu harufu ni sahihi kabisa, kitaalam inaitwa adrenaline hormone. Hio huzalishwa nyingi pale mtu unapotaharuki wakati wa kukabili changamoto ya papohapo.
Ndimi mbili anazotoa nje nyoka ndizo hu-sense hio harufu na taarifa hiyo kutafsiriwa na 'Jacob's organ' iliyo sehemu ya juu ndani ya kinywa chake. Hapo hutafsiriwa kama hatari na nyoka kuchukua hatua ya ku-bite kama mbinu ya kujilinda.
Kuhusu maamuzi ya nyoka kung'ata sio kipaumbele chake , ni kweli kabisa. Nyoka kuamua kung'ata ni maamuzi ya mwisho kabisa baada ya jitihada zote za kumuepuka adui/subject zimegonga mwamba. Kwanini?
Kwasababu sumu ya nyoka ni pure protein, hii humuitaji kula mawindo yenye protein zaidi kitu ambacho humghalimu na kuchukua muda mrefu.
Sumu yake inamsaidia zaidi katika mawindo japo anaitumia pia kujilinda.
La ziada,
Gently handling.
Jinsi mtoto anavomshika nyoka na reaction za mtoto ni gently/friendly zaidi hivyo ukijumlisha na utulivu wa kiwango Cha hormones basi nyoka anafeel safety sense.
Angalizo,
Nyoka wengi hawana sumu na wachache pekee ndio wenye sumu. Katika hao wachache wenye sumu tuna black mamba/koboko. Huyu Huwa anaitafuta shari mwenyewe, hasubiri upite karibu yake au umkanyage ndio ashambulie.
Ndani ya 20mita Hadi 50mita (social distance) kuzunguka eneo lake akihisi uwepo wa kitu chochote anachoweza tafsiri kama threat/tishio basi yeye huanza msako.
Ana Sumu Kali na ndani na nusu saa bila msaada wa haraka kupoteza maisha ni njenje.
Ushauri.
Ikitokea umegongwa na nyoka au ndugu yako, jitahidi kukalili muonekano wake ikiwezekana muue kusaidia utambuzi wa aina ya sumu na tiba yake.