Je, kwanini ni ngumu kwa Nyoka kuwa ng'ata watoto wadogo?

Hapana, si kweli kwamba nyoka ni rafiki wa watoto au kwamba hawadhuru watoto. Kisayansi:

✅ Ukweli wa Kisayansi:
  • Nyoka wengi ni waoga na hukimbia binadamu, lakini si rafiki wa watoto wala watu.
  • Baadhi ya nyoka wana sumu kali (kama cobra, puff adder, black mamba), na wanaweza kumdhuru au hata kumuua mtoto ikiwa watashtuliwa au kuhisi tishio.
  • Watoto wako kwenye hatari zaidi kwa sababu miili yao ni midogo, hivyo hata kiasi kidogo cha sumu kinaweza kuwa hatari zaidi kwao kuliko watu wazima.
  • Nyoka wasio na sumu bado wanaweza kung’ata kwa kujilinda, wakisababisha maambukizi au maumivu makali.

🧠 Chanzo cha imani potofu:
Hii imani inaweza kuwa sehemu ya hadithi za kitamaduni, simulizi au imani za kienyeji, lakini haithibitishwi na utafiti wa kisayansi.

🔴 Hitimisho:
Nyoka si rafiki wa watoto — ni muhimu kuwafundisha watoto kujiepusha na nyoka na kutoa taarifa kwa watu wazima wakiona nyoka, badala ya kuwakaribia.

Ungependa maelezo ya jinsi ya kujikinga na nyoka kwa watoto?
 
Japo case za watoto kung'atwa na nyoka ni 2/10

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23]

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Ufahamu walionao watoto ni tofauti na ufahamu alionao mtu mkubwa.

Mtoto anajua kila kitu ni chema, wakati wakubwa wanajua kuna mema na mabaya.

Mtoto akiona nyoka ata-react kama rafiki yake... Wakati mkubwa abamuona nyoka kama adui yake.
Nyoka ana-respond kulingana na ulivyokuja.
 
Kihusu ushari wa koboko nakubaliana na wewe. Lakini huwa hashambulii kila wakati.
Nakumbuka mwaka 2017, nilikuwa na mzee tukielekea mashambani, basi mimi sina hili wala lile; nikashangaa mzee kanizuia kwa mkono pasi na kusema chochote. Akaniashiria niangalie mbele na nisigeuke. Bonge la joka la kijivu na kichwa chake kidogo, urefu wake ni kama mita 3 au 4 hivi kilichochongoka! lilikuwa limeinua nusu ya kiwiliwili chake likifanya scanning kwenye nyuso zetu. Lilipoona tumetulia likashusha kiwiliwili chake na kuondoka kwa kasi ya ajabu mithili ya risasi. Huyo kule uheheni tunamuita Nyamuhandu, ninyi wazungu mnamuita black mamba.
Rest in peace mzee, uliniokoa siku ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…