Je, kwanini vilabu vingi vya pombe za kienyeji hupenda kupiga nyimbo za zamani hasa zenye asili ya Kongo?

Ni research tu isiyo rasmi mkuu Yani utasema kule wapo ulimwengu wao maana Ni nyimbo za kitambo sana
Unataka wasikilize nyimbo za watoto wa 2000 za akina Diamond inama inuka nichomeke inazama yote??

Kwenye vile vilabu wapo watu wazima lazima wasikilize nyimbo zilizotrend wakati wao wako na pesa na nguvu za kutosha.
 
Zamami nyimbo za Congo zilitawala, hata muziki wa Bongo umeathirika sana na mziki wa congo.
 
Mama yangu alipika hizi pombe, naziheshimu. Na kweli miziki ya vilabuni ni rhumba za zamani sio za kina fally ipupa
 
Mimi nimeenda kijijini kumenishinda wale wazee wa jika langu wengi wamesharudisha namba.

Vijana wamechoka kwa kunywa gongo.

unaweza ukatembea barabarani km 2 au 3 usikutane na mtu yoyote hata mbwa.
 
Unataka wasikilize nyimbo za watoto wa 2000 za akina Diamond inama inuka nichomeke inazama yote??

Kwenye vila vilabu wapo watu wazima lazima wasikilize nyimbo zilizotrend wakati wao wako na pesa na nguvu za kutosha.
Kwa hiyo ndo mnazipenda sana
 
Inaezekana zile nyimbo walskiza wajanj wa zaman sehem za stareh ambapo ndo vilabuni na mara nying huko huenda wazee au watu walochoka kimaisha
Walochoka kimaisha πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Mimi nimeenda kijijini kumenishinda wale wazee wa jika langu wengi wamesharudisha namba.

Vijana wamechoka kwa kunywa gongo.

unaweza ukatembea barabarani km 2 au 3 usikutane na mtu yoyote hata mbwa.
Aisee hatari sana, na kilabuni ulipita pita ukawakosa, au ndio gongo imewasepesha
 
Zina vibe lake ukute kimama chembamba kina kilemba na chupa lake la wanzuki mkononi kinacheza bhuyagayaga huku kinabambiwavna mlevi mbaba anamkoti mchafu na mzula usio na rangi maalum...ndio starehe yao hiyo
Uje mahakamani kesho πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Au sio, kimpumu, ulanzi, mtindo + gongo
 
Tukiwa tunachamba koo huku tukiupa mwili pole, hatuwezi kusikiliza kwaya ama singeli mkuu...😊
 
Zamani ipi unaiongelea? Binagsi naingia kwenye kilabu kinachopendelea miziki yenye kukumbusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…