Je, kwanini vilabu vingi vya pombe za kienyeji hupenda kupiga nyimbo za zamani hasa zenye asili ya Kongo?

Je, kwanini vilabu vingi vya pombe za kienyeji hupenda kupiga nyimbo za zamani hasa zenye asili ya Kongo?

Wengi wao niwazee wakati waujana wao hizo ndizo zilikuwa nyimbo pendwa kwao kama leo tu! Nyakati hizo labda walikuwa napesa ama wapendwa wao sasa hivi hawapo tena na pesa hakuna tena . Wanatumia mda huo kujifariji na kukumbuka moments zao huko nyuma huwa nifuraha kwao. Alisikika mlevi mmoja akisema
 
Ni Kama utamaduni vile katika vilabu vya pombe za kienyeji utakuta nyimbo nyingi Kama siyo zote huwa Ni zile za ki Kongo Tena za zamani Sana zile za kina Pepe kale, Kanda bongoman n.k hii Ina uhusiano gani na vilabu vya pombe za kienyeji?

Maana karibu maeneo yote yenye hivyo vilabu nyimbo Ni hizo tu. Au Ni nyimbo zinapendwa na walevi?
Uzi tayari.
Ya walevi, waachie walevi.
 
Bar nyingi zinazopiga muziki wa wakubwa ndizo zinazouza, vijana wengi hawana hela
 
Duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuh!!!!!!!
Unaweka bongo fleva ni mzee gani atakuja hapo? nyimbo zimejaa matusi matupu na wala haijulikani unachezaje, wasanii wa sasa bila mganga hawazindui Album, nyimbo hazina kitu
 
Ukizaliwa wewe ni kijana

Ukose kazi taabu zote utazipata.....

Ukienda ukiona mtu wa kwenu...

Ukitoka wanaanza masimango;

Huyu kijana kazi gani anataka.....

Kupeleka ndege au kupeleka gari!
 
Hata walevi wa kileo huwaambii kitu zikipigwa nyimbo toka congo za leo hiii......MayDay mayday
 
Soukous ina amsha amsha halafu bonge la throwback kwa watumia pombe hizo ukizingatia huwa watu wazima zaidi.

Evelyne ya Aurlus Mabele au Laisser Passer (Matchatcha) ya Diblo Dibala huwezi zikosa.
 
Inaezekana zile nyimbo walskiza wajanj wa zaman sehem za stareh ambapo ndo vilabuni na mara nying huko huenda wazee au watu walochoka kimaisha
kwani siku hizi kuna muziki? hata wewe unaweza kuimba lolote, bila kufuta sheria za uimbaji
 
Back
Top Bottom