Uchaguzi 2020 Je, lengo la watawala kukifanya chama cha NCCR Mageuzi kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya mwaka 2020 litafanikiwa?


Mpinzani na mgomvi mkuu wa CCM ni yeyote yule anayeitwa CHAMA KIKUU CHA UPINZANI. Hata mkiwa marafiki leo lakini kesho ukipata hadhi hiyo wewe ni adui yake.

Hivyo CCM kamwe haitaki NCCR kuwa chama kikuu cha upinzani. Inachohitaji hiki chama tawala ni kumpa nguvu Mbatia ili:
  • Asikubali kuungana na vyama vya upinzani katka uchaguzi 2020.
  • Kwa maana hiyo atagawa kura za wapinzani na kuwaangusha wabunge wa upinzani.
  • Kuwarahisishia wagombea wa CCM wabunge/Rais kuwa na msaada toka NCCR Kihoja kwani kinawanachama wengi toka CDM.
Aidha chama tawala kina mkakati wa kuwashawishi wagombea wa NCCR kuwekwa maeneo yale ambayo CHADEMA wana strong hola kama Mbeya (hususan ktk kumuondoa Sugu), Kilimanjaro, Mara, Iringa (analengwa Msigwa) n.k. Kwa hili nafikiri watafanikiwa, sijui CHADEMA watakuwa wamejipangaje.

Kwa kuwalipa Fadhila hao NCCR, chama tawala kitawazawadia wabunge kati ya 5 mpaka 7. Hii haitoshi kuwa chama kikuu cha upinzani.
 
nccr ni kama kaingizwa choo cha kike, haitawezekana ccm kugawa fungu nccr mageuzi wakati yenyewe tu saiv inahaha kwamba oktoba itakuaje! chadema wana mtaji wa rasilimali watu nchi nzima je mbatia na kundi lake watajaa kibaba?
 
Watakifanyaje wakati Ni matakwa ya watawala?,kama siyo watawala kinachoendelea leo nccr unakiona?
Ni mwananchi gani mpumbavu kiasi cha kuchagua wasaliti wa Taifa? nani haoni wanayoyafanya CHADEMA na Zitto kila uchao kumtukana na kumdhihaki mkuu wa nchi? nani haoni wanavyolichonganisha Taifa kwa wadau na wahisani wa maendeleo? ni mwendawazimu tu ndo atasubiri aambiwe na Rais kwamba hao hawafai ndo achukue hatua, wananchi tunaona na tushaamua, wakipata walau mbunge mmoja October washukuru.
 
Ni historia inajaribu kujirudia kumbuka NCCR ndio kilikuwa chama kikuu cha upinzani mwanzo kabisa wa siasa za vyama vingi mwaka 1995. Ukweli ni kwamba ccm wanacheza na kitu wasichokijua, CDM imejikita sana nchi nzima na hawawezi kuiua CDM kupitia NCCR na hatima ya yote vyama hivi vitakuwa kitu kimoja na kuipigilia ccm msumari wa mwisho.
 
nccr ni kama kaingizwa choo cha kike, haitawezekana ccm kugawa fungu nccr mageuzi wakati yenyewe tu saiv inahaha kwamba oktoba itakuaje! chadema wana mtaji wa rasilimali watu nchi nzima je mbatia na kundi lake watajaa kibaba?
Hahahahaha...hao watu wako nje ya nchi ma multiple accounts tweeter na jamiiforums, kule field CHADEMA haina mtu mkuu, watu walishatembea kitambo hata kabla ya Lowassa kurejea CCM, October sio mbali mtafurahi na macho yenu, hakuna wa kuunga mkono wasaliti wa Taifa.
 
Nimezunguka baadhi ya maeneo wakurugenzi wengi wamewekwa wa toka nyumbani, inahitajika nguvu ya ziada sana.Wakifutilia vizuri watagundua hiki nilicho andika

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
fazili
Wanachofanya CCM ni sawasawa na mtu anayekimbiza kivuli chake, akiamini kuwa ipo siku atakikuta![/QUOTE]
 
fazili
Wanachofanya CCM ni sawasawa na mtu anayekimbiza kivuli chake, akiamini kuwa ipo siku atakikuta!
[/QUOTE]
Hahaha...mko desperate kishenzi, kwa hiyo CHADEMA watakuwa kitu kimoja na wasaliti walonunuliwa?
 
Je unaipenda Chadema au unaishabikia tu chadema kwa sababu unaichukia ccm?
 
Ukitia akili kichwani utaelewa tu. Anuita ni mdudu gani?

Waulize bavicha mbona ghafla wanamuogopa jamaa na kumuita msaliti ghafla? Muulize BAK kwa nini anuita mbatia msaliti ghafla!
 
Imenikumbusha wakati Pan Afrika inaundwa kuingoa Yanga nguvu za pesa zilitumika sana lakini wananchi walishinda hivyohivyo nccr itashindwa
 
CCM wanapenda vyama dhaifu kwa kuwa havina madhara kwao, na wanapambana na vyama vya kweli ambavyo ni tishio kwa CCM ili wavisambaratishe.

Hata NCCR wenyewe wakifikia kiwango cha kuwatishio kwa CCM, nao hawatafika mbali kibao cha kuwasambaratisha kitawageukia.
 
Bila kuwa na tume huru ya uchaguzi na tukiendelea na tume hii hii, basi aslimia 100 ya lengo la watawala litafanikiwa.
 
Reference yetu iwe Local Gv election. Uhuni wa wazi ulipfanyika.

Kwa mantiki hiyo wamejiandaa kwa uhuni mwingne wa mchana kweupe.

Watakachofanya ni sawa na LGE, watawakata majina, watakao baki watapigwa rafu kwenye kampeni, watakao himili watapigwa rafu kwenye uchaguzi, watakaohimili hawatotangazwa, maeneo ambayo wananchi watapinga...watapigwa na wengne kupotea.

Watawatangaza wabunge wasiozid wawili au hata sifuri kabisa. Hawanaga aibu wale.

Uchaguzi huu 2020 wananchi wasipokataa uhuni wa CCM, hakuna mbunge wa CDM atarudi bungeni.

Ni dhahiri sasa ACT wameungana na CCM ndo maana uumeona Ado Shaibu alichoandika leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…