Uchaguzi 2020 Je, lengo la watawala kukifanya chama cha NCCR Mageuzi kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya mwaka 2020 litafanikiwa?

BAK
Hawa watawala wetu wamegeuza uchaguzi kuwa matakwa yao binafsi, badala ya kuheshimu matakwa ya sanduku la kura lililo huru
CHADEMA na wapinzani wa dhati msilalamike tu. Mdai tume huru ya uchaguzi la sivyo itakula kwenu. Learn from Burundi. The opposition was a mass mover but are losing.
 
Kama unaongelea wananchi wa multiple accounts wa jf na tweeter ni sawa hao wabunge wawili waweza patikana, lakini kama ni kule field wajidanganya, wananchi wanaona myafanyayo, usaliti dhidi ya Taifa na matusi, dhihaka dhidi ya mkuu wa nchi hata kwa mambo yanayopaswa kutuunganisha havitawaacha salama, mkipata mbunge mmoja mshukuru Mungu.
 

Mkuu hili jambo halitaki tochi, lipo tena mchana kweupe ata huyo Mbatia hivi makaribuni kama alijitoa fahamu na kuusema vibaya UKAWA lakini pia akatishia kwamba atatoa siri nyingi za UKAWA ni kama vile na yeye ametolewa fahamu ni upande ule ili kutimiza adhma na malengo ya upande ule ndio mana ukifuatili siku za hivi karibuni mkuu alimsifu sana Mbatia na kusema "Mbatia ni Kiongozi wa upinzani pekee anayejitambua" na alimpongeza sana.

Kwa ufupi ni kwamba chama hichi cha NCCR mageuzi ambacho sasa kinajengwa kwa nguvu zote kuwa chama kikuu cha upinzani hakitakuwa na tofauti na kile chama cha TLP cha bwana Mrema ambacho nacho hivi karibu mapema kabisa wameshampitisha mgombea wake wa urais na kusema atakuwa Mkuu aliyepo sasa mdarakani. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa miaka yote., Mimi niliwahi kuhudhuria kampenzi za Mrema miaka fulani ya uchaguzi hapo nyuma wakati wa JK alikuwa akisema waziwazi kura za rais zipigwe upande wa CCM.

Sasa na hii NCCR mageuzi nacho kitakuwa chama cha upinzani bandia kama ambavyo kitakavyokuwa chama cha Bwana yule ambavyo vimepewa meno na nguvu ni upande ule.

Sasa suala la kufanikiwa na kutofanikiwa hapa ni kitendawili, Hatujuwi ni nguvu gani itatumika uchaguzi ukija lakini kuna hofu kubwa ni vigumu kwa mbunge aliye bungeni kuacha ubunge kwa chama Makini kama Chadema ambacho kishakuwa na muelekeo angalau kuchukua madaraka siku 1 na kuamua kwenda NCCR lazima kuna jambo zito nyuma ya pazia.

Chamsingi Chadema walione hili muda bado upo na waje na njia mbadala naamini wanachama wao wapo hai hawajafa na wanayaona haya yote, wabunge siju madiwani na viongozi waliotoka ni wachumia tumbo tu, Wanachama wakukipigia kura chama ndio raslimi ya kuiheshimu siku zote katika chama cha siasa.

Hili jambo halitaki tochi, Kule Zanzibar wako Imara sana na siasa za Zanzibar ni rahisi sana watu siku zote hutaka kujua Maalim Seif yuko upande gani basi wao woooote haihitaji hata dakika 1 humfuata wote kwa wakati mmoja, zile herufu 3 za neno CUF zilizokufa hazina maana yeyote wala athari yeyote, saiv kila mtu ni ACT na utashangaa watu haikuchukua ata wiki 1 kila mtu ana sare za ACT watu waliochukua fomu kugombea uongozi ndani ya ACT kwa kule zanzibar ni utitiri mkubwa wengine mpaka kukosa nafasi ni kama vile ilivyokuw CUF ya awali.

Chadema wakae walione hili na waje na njia mbadala zaidi, kiukweli kunahitaji mbinu yakinifu na mipango kabambe ili hili lengo lao lisifanikiwe. Wakibweteka na kulichukua as usually aisee ni anguko kubwa kwa Chadema lakini kwa siasa zenye upinzani kule Bara zitakuwa ndio mwisho wake.
 
Mbona ni rahisi sana kukifanya chm cha nccr kuwa chama kikuu bila hata kubadilisha mioyo ya watu? Subiri utaona kazi ya tume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni ishara tosha kwamba CDM ndo chama bora cha upinzani maana wameshindwa kukinunua,hata mbinu chafu hazizai matunda tarajiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila uchaguzi mkuu unapokaribia...

Tunaona ufadhili wa ajabu ajabu... wa kufuja na kuteketeza pesa bila sababu za msingi...



Cc: mahondaw
 
N Nimeona Ado Shaibu alichokiandika......

Eti Magu ameahidi kuwa atakayeshinda uchaguzi Zanzibar atatangazwa...........

Hivi kweli huyo Ado Shaibu anamuamini Magu kuwa alichoongea, ndicho atakachokitekeleza?
 
Kwamba hayajawahi kuwa mabaya japo yanatofautiana?
Ni kweli ukifanya comparison ni kuwa angalau wakati huo matokeo angalau hata kama atashinda mpinzani na ikatokea mpinzani huyo "akakomaa" alikuwa akitangazwa mshindi..................

Jambo ambalo limekuwa tofauti sana katika utawala huu was awamu ya tano, ambapo mtendaji wa serikali kumtangaza mpinzani kuwa ameshinda uchaguzi, ni sawasawa na kujifukuzisha kazi!
 
Kuna mifano?
Wewe umesahau kauli ya Jiwe alipokuwa akiwahutubia wakurugenzi na kuwaambia kuwa........

Ninakupa gari ya fahari ya kutembelea, nyumba nzuri ya kuishi na msahahara mnono, halafu nisikie umemtangaza mpinzani kuwa ameshinda kwenye eneo lako........

Sasa Mkuu wa nchi anatamka maneno ya aina hiyo, bado unategemea kuwepo uchaguzi ulio huru na haki kweli??
 
Aliwahi kusema pia 2020 kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki! Kama suala ni kusema...
 
Aliwahi kusema pia 2020 kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki! Kama suala ni kusema...
Anaongea hivyo ili kuwafurahisha jumuia ya kimataifa.....

Ili asikose mikopo ya WB na IMF
 
Hayo maswali majibu anayo mwenye SACCOSS,kuisema CCM ni kuionea,CCM haikati mishahara ya wabunge wa Chadema ili iende kwa mwenye SACCOSS ,CCM haikukaa kwenye kikao hewa cha kuwafukuza uanachama wabunge waliogoma kwenda lockdown jijini Dar Es Salaam,tatizo badala ya kuangalia vibanzi vyenu kwenye macho yenu mnaangalia upande wapili,pale unapotegemea washauri wakuu wa SACCOSS ni akina Halima na shoga wake Bulaya,Lema, Mchungaji(?) Msigwa matokeoyake ndio hayo,jiulize akina Baregu na Safari wako wapi.
 
Bahati mbaya watanzania wengi ni mambumbu. Wanapelekeshwa kama mang'ombe.

Sent using Fly in any Weather.

wewe ni mtanzania au?unapata wapi ujasiri wa kuwaita ndugu zako mlionyonya titi moja la mama yenu ambaye ni tanzania kuwa ni wapumbavu?
 
Na Chadema wanaichukia CCM kwa kuwa ni chama imara na kina madhara kwa malengo yao!
CHADEMA wanaichukia CCM kwa kuwa ina madhara kwa wananchi na malengo ya watanzania,na ni chama imara kwa ufisadi na kwa kuwabeba mafisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…