Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5?

Duniani ukweli hufichwa, ukajulikana na watu wachache sana,Uongo ndiyo imekuwa ikilishwa jamii siku zote, sijui ni kwa nini?
Nakuelewa sana.
Ndio maana hata mawaziri ambao ni watumishi kwa msingi wanawajibika kwa umma, viapo vyao huwa ni "sitatoa siri za baraza..."
Maana yake kuna siri. Nataka kuamini siri (uficho) ndani yake kuna mema na mabaya bila shaka.

Ndio namna ya kuendesha serikali duniani.

Huyu anaejadiliwa hapa, alikiri kuna makaburi akiyafukua pindi amekalia kiti like, 'pasingetosha'. Akafunika kombe akalisongesha 😅.
 
The darkest day ever in tz
 
Lakini pia kupata nafasi ya kuweka mipango ili mama asichukue nafasi km katiba inavyotaka.

Basi mkuu wa majeshi wakati huo akaingilia Kati na mama anatangaza habari ile usiku akiwa tanga , halafu wakamrekodi na kuituma Dar Tbc na nyumba nyingine za habari.

Ilikuwa surprise fulani. Mipango ilikuwa mama asiapishwe kuchukua nafasi.
 
Uzi wako umerudisha Apostle Mayala
 
Wapi Tanga ndio alitumwa namba 2 , ila Tanga si ndio kwao yule Mzee wa wazuri awafi eti ee? Kina je wapi yule
 
Paskali unatuzuga, usijidai hujui.
 
Mkuu wewe kihistoria siyo mtu wa kushangaa.
Kuelekea siku za mwisho za jamaa yetu, the air was thick with gossips za mustakabali wake both kiafya na kiutawala.
Wajuvi walikuwa wanasema alikuwa na hali mbaya kiutawala, he made too many powerful enemies.
Watu huwa wanajidanganya kuwa ukiwa top man you are in control by 100%.
Far from the truth.
Clue iko hapa, jamaa alipata ulinzi usio wa kawaida, hadi surveillance helicopter ya wajeda.

Tunakumbuka ni kama alihamia kijijini kwao ambako mgeni yeyote anayeingia kijijini, unaweza kummonitor kiurahisi.
Mpaka leo haieleweki i kilichomtoa pangoni kijijini kwake, na ka drive all the way hadi Dar, akisimama katika miji mikubwa kusema hili na lile.
Wakati huo hakuwa mgojwa.
Tatizoilikuwa ziara ya Dar iliyoishia Kituo kikuu cha mabasi kule Kimara.
Mpaka wakati huo alikuwa yuko safi, lakini pale ndio jamaa akaanza kukohoa.
Hakuonekana hadharani tena hadi mama alivyotangaza akiwa kwa wagoshi.
Hata hivyo wajuvi wanasema mitambo ya pace maker ilikohoa tarehe 9/3/2021 na walijaribu kurevive bila mafanikio, hatujui ukweli ni upi.

Kwa kifupi tumepata somo kubwa, hata ukiwa na madaraka makubwa kiasi gani, dont make too many enemies.
Kama mbwa koko, wakiwa wengi wanaweza kumlaza simba.
 
Nakazia kwa uchungu.
 
Eti wanasema nilikuwa simpendi Makande, Wakati juzi kati kanipa kiwanja nkajenge kilingeni kwake geita.KAULI HII ILINICHANGANYA NA NIMEITUNZA.
 
Conspiracy theory.
 
Fasihi simulizi ni ukoko, kwangua!
Mimi napita tu Kaka Pascal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…