Je mafanikio ni uchaguzi maalum kutoka kwa "higher power"?

Fafanua zaidi mkuu.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
1% ya billionaires walichotushinda ni kupigania talent zao walizipewa na muumba (eg wasanii, wacheza mpira etc) na pia passion zao walizozaliwa nazo, eg Jeff Bezos, Elon musk, bill gates etc. Kuna wengine pia wa level za kati na chini ambao wamefanikiwa sana kutokana na kupigania passion na talent zao bila kukata tamaa.
Sisi mfumo wetu wa shule umetufanya tusitambue tuliumbwa na uwezo gani, so tunaishia kuwaza ajira tu.
Conclusion, ukijua Mungu alikuumba uwe nani hapa duniani utafanikiwa tu. Most of us hatujui, ndio shida inaanzia hapo.
 

Mkuu historia ya maisha ya mtu yeyote aliyefanikiwa huonekana kama vile ipo “very special”..... yaani hufanywa kuwa ni jambo ambalo binadamu wengine woooote tumeshindwa kufanya kasoro wao tu

Sipo hapa kupuuzia juhudi zao kuwa pale..... NOPE

Kinacho wafanya kuwa na mafanikio makubwa kinaweza kutengenezewa kila aina ya dhana kulingana na mtazamo na imani ya mtu

Wapo watakao sema ni Mungu ndio amepanga
Wapo wanao amini kuna secret code
Wapo wanao amini ni juhudi na bahati nk

Wewe unaamini Mungu katuumba kwa kusudi fulani hivyo unatakiwa kulijua kusudi hilo na ujibidiishe basi hapo utakuwa miongoni mwa hao 1% ya matajiri........ Lakini kuna watu wanakua mabilionea kwa kuua watu, kuandaa na kucheza porn, kuiba oline, kuchochea vita wauze silahaa, matapeli nk nk

Jambo lolote ukiisha ingiza imani za Mungu huwa linapoteza mantiki

Hakuna mtu yeyote aliyeumbiwa kusudi lolote lile

Kwa mujibu wa Nature.... only few will make it to the top, wengine ni wawezeshaji tu

Tukazane ili nafasi ikitokea unapita nayo
 
Sehemu kubwa ya utajiri ni kutokana na bahati na juhudi kiasi.
 
Thanks mkuu

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Thanks mkuu

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Sehemu kubwa ya utajiri ni kutokana na bahati na juhudi kiasi.
Labda tujue kwanza utajiri ni nini! Bahati haifanyi kazi kwenye economic dynamics! Kwamba nchi masikini hazina bahati na juhudi kiasi? Nope, kila kitu kinapangwa/ kimepangwa kwa mfumo wa hali ya juu na wachache. Mfano: USA inaongoza kwa madeni, lakini deni lake sio kama nchi za Kiafrika. Wao deni lao hawadaiwi na yeyote, ni fake, wanaweza kuprint dollars muda wowote. While deni la nchi za tatu, lazima lilipwe kwa dola, ambayo watakupangia riba, na utaipataje hiyo dolari. Huwezi kuiprint. Watakwambia zalisha hiki au kile, uuze kwetu. Kile wanachkipenda. Then watakishusha bei, uendelee kuhenya na deni na rundo la umasikini.
Halafu wanakuletea misaada na nadharia lukuki za uchumi, ambazo hazikusogezi popote. Utajiri haupo bila wengine.
 
Thanks mkuu

So wealth creates wealth.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Hapa hakika mimi nnabaki kua mpenzi msomaji tu,maarifa juu ya maarifa namawazo juu ya mawazo.hongereni kwa michango mizuri.
 
Watu ambao hawajamjua Mungu, utajiri na mali, ni umasikini.

Watu ambao hawajamjua Mungu, hawajui fedha, na hawajui mali, ni za nani.

Haiwezekani, mtu ambaye hajamjua Mungu akawa tajiri, na akawa na mali.

Inawezekana, mtu akapata na mali, na akapata utajiri, kwa udanganyifu na njia zisizo haki. Huu ni umasikini.

Utajiri na mali, ni "Baraka" na "Zawadi" kutoka kwa Mungu. Sasa baraka maana yake ni nini, na zawadi maana yake nini.

Kuwa tajiri, na kuwa na mali: Kunataka kwanza kabisa "Hekima", kama kitu kinachotangilia vingine vyote. Sasa, hekima maana yake ni nini; na, ili mtu uwe na hekima unatakiwa uweje; au ufanyeje.

Pili, "Unayatazamaje mambo", ndio akili. Sio tu, kuhusu kuwa na ufahamu wa kawaida wa mambo, bali ni kuhusu kuwa na uewelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu. Je, unao uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu?
 
Sasa kama unahela unatafanya kazi gani tena tunafanya kazi ili tuendelee kuishi vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…