Je, Magufuli amemfunika Nyerere kwa waombolezaji kwa sababu ya mtandao au ni kweli?

Dunia nzima idadi ya watu haizidi bilioni 7.5 ukisema msiba wa JPM umefuatiliwa na watu bilion 3.9 maana yake zaidi ya nusu ya watu waliopo duniani wanafuatilia tukio hili

Hapa napata mashaka kidogo kwanza kauli yenyewe umetoka mdomoni kwa Kassim Majaliwa alietundanganya mbashara tena kwenye nyumba ya ibaada

"Mh Rais ni mzima yupo ikulu anapiga kazi nimeongea nae leo asubuhi amesema niwafikishie salamu"

Kumbe Rais wetu alikuwa mgonjwa (Apumzike kwa amani) hata kwa hili la bilioni 3.9 mmmmh!

Watu bilion 3.9 ni zaidi ya watu wote kabisa waliopo bara la Afrika yaani maana yake watu wote kabisa Afrika sio wazeee , watoto yaaan woteee walitizama tukio [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Baada ya kujua unachouliza ndiyo iwe nini?

Mnapoelekea mtakufuru...huyo ni binadamu kama binadamu wengine,na amekufa kama walivyokufa wengine na sisis tupo njia kuelekea alipoelekea Magu.

Amepambana kadiri alivyoweza embu muacheni jaman.

Hizi sasa siasa za kipumbavu maana hata ukijua haitomsaidia kwa chochote

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Mazishi ya Rais Magufuli yanaweza kuweka historia ya kuhudhuriwa na watu wengi kuanzia kuaga hadi kesho atakapozikwa...
Kwani mwalimu nyerere alitembezwa kama bizaa?

Elewa kwamba umaarufu wa mtu upo katika pande mbili. Waweza kuwa chanya au hasi.

Leo hii ukimleta osama anaweza kuwa maarufu kuliko yeyote duniani, why kila mtu anataka amshuhudie kwamba ni yule Osama mtesi kweli au kiini macho? Vivyo hivyo kwa Magu.

Kamwe kamwe familia ya mtu kama Mawazo, Azory, Kanguye Ben saa8 nk wk kama hao hawawezi kusikia kuwa Magu kafa na maiti yake ipo mjini kwao wasitoke kwenda kushuhudia.
 
1) Hawakupendwa na Mabeberu
2) Walipendwa Mno nchini mwao na Wanyonge
3) Walileta maendeleo sana kwa muda mfupi
Hivi mnatumia vigezo gani kusema "hakupendwa na mabeberu"?! Tanzania iliwahi kukatiwa hadi misaada wakati wa Mwalimu! Huyo JPM lini alikatiwa misaada?! Acheni hizi porojo za kumpaisha kwa kumpa sifa zisizo zake!! Hivi Jiwe angekuwa hapendwi na mabeberu hata hiyo mikopo ya mabeberu angepata?! Kwa mara nyingine, umetumia kigezo gani kusema alikuwa hapendwi na mabeberu?!
 
Jibu ni fupi,sababu za hayo yote ni
1.Magufuli ameaga dunia akiwa bado madarakani (hivyo alikuwa bado na mvuto), wakati Nyerere alikuwa tayari ameshastaafu.

2.Wakati Nyerere anafariki idadi ya watu ilikuwa ndogo, wakati Kipindi hiki ambacho Magufuli ameaga dunia watu ni wengi(kuna ongezeko la watu).

3.Mifumo ya mawasiliano Wakati Nyerere anafariki ilikuwa bado duni Sana, wakati huu ambapo Magufuli amefariki mifumo ya mawasiliano ipo ktk ubora wa hali ya juu.
 
Mazishi ya Rais Magufuli yanaweza kuweka historia ya kuhudhuriwa na watu wengi kuanzia kuaga hadi kesho atakapozikwa...
Unaelewa tofauti ya Rais kufariki akiwa madarakani na akiwa amestaafu?

Unaweza kulinganisha vitu viwili tofauti kwa mzani ule ule? JKN (Rais Mstaafu, Baba wa Taifa) JPM ( Rais aliyekua madarakani)

Pia inategemea unaongelea kufunika kwa maana ipi, ikiwa no wingi was watu, JKN alizungushwa mikoa mingapi?

Kuna vitu kama legacy n.k hivyo ndio vya muhimu zaidi.
Katika hawa wawili, kila mmoja alikua na umaarufu na ubora wa namna yake, mapungufu vile vile.
 
Miaka 6 aliyofanya ni zaid ya waliokaa madarakan miaka10 nanukiunganisha wote
 
Acheni matusi ninyi Yaani mimi japo sio mwana sisiemu ila kumlinganisha Nyerere na huyu mpima mapapai na mafenesi kama yana korona ni kituko cha karne ya 22.Halafu korona ikamfyekelea mbaali mamaaaamee.
 
In addition to that, social media wakati wa Nyerere was almost nonexistent. Pia wengi walishapata taarifa kuhusu “kupotea kwake”, Na pia kuhusu yeye kuwa “COVID-19 denier”
 
Nyerere hakufariki mwaka 2000
 
Mimi Nilishuhudia Umati Mkubwa sana kifo cha Mwalimu kwani nilikuwepo Mwili kila njia uliyopita ilifungamana Watu wengi sana sana na kwenye kuaga Mwili wake pale Taifa siku tatu lakini haikutosha japo ilikuwa 24/7 me sikufanikiwa kupata nafasi na wengi sana hawakuweza so ilibidi wawe wanasimama barabarani tu Uwanja wa Ndege tuliingia hadi ndani kule Termnal 1 tulikaa hadi ndege ikapaa na kupotea angani ndipo tuliondoka... Maraisi wa nchi nyingi sana walikuwepo hadi wa Nchi ya Finland Bonge Nyanya alikuwepo na Museven pia alikuwepo... Wa Magufuli hajaja! kapunguza Idadi tayari
 
yapata bilioni nne kwa mujibu wa taarifa za serikali na vyombo mbali mbali vya habari.Pia kama ulikuwepo 1999 linganisha uliyoona juzi na jana na yale ya mwaka tajwa utapata jibu bila kuhitaji msaada wangu mwanangu. SIyo kila kitu lazima usaidiwe.
Msiba wa Nyerere haukufanyiwa siasa kama hii. Haukuwa show hizi.
Pili Nyerere alikuwa mstaafu wakati anafariki tofauti na huyu amefariki akiwa madarakani .
 
Tofautisha nyakati chalii
 
Nyerere kwanza kifo chake watu walichanganyikiwa sidhani ata kutembea Walisema.
3.9 billion cmchezo R I P JPM.
3.9 billion cmchezo R I P JPM.
Kuna uzushi duniani ameuliwa cause alikuwa anti vaccine.Na dunia nzima kuna covid na asilimia nyingi kubwa hawataki vaccine .Halafu alikuwa kama trump very controversial na strong man dictator wanna be na mara nyingi sana watu wanapenda watu wa aina hii .Magufuli nick name yake Africa Trump like
 
Nilishangaa hata dikteta wa urusi Stallin aliagwa kwa maelfu,baada ya hapo sishituki na uwingi wa watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…