Je, Magufuli amemfunika Nyerere kwa waombolezaji kwa sababu ya mtandao au ni kweli?

Je, Magufuli amemfunika Nyerere kwa waombolezaji kwa sababu ya mtandao au ni kweli?

Dah wenye mahaba niue na marehemu wamechanganyikiwa mno na wanateseka sana,wanaisifia mpaka maiti
 
Mazishi ya Rais Magufuli yanaweza kuweka historia ya kuhudhuriwa na watu wengi kuanzia kuaga hadi kesho atakapozikwa.

Kwa haraka haraka naona haraiki iliyomuaga na itakayomzika pamoja na matatizo ya corona, haijawahi kutokea.

Kwa hivyo, anaingia kwenye historia kama mtanzania aliyezikwa na watu wengi ukiachia mbali kufautiliwa na wengi duniani.

Nini mawazo yako juu ya dhana hii?
Nyerere kwanza kifo chake watu walichanganyikiwa sidhani ata kutembea Walisema.
Msiba wa Nyerere haukufanyiwa siasa kama hii. Haukuwa show hizi.
Pili Nyerere alikuwa mstaafu wakati anafariki tofauti na huyu amefariki akiwa madarakani .
kulikuwa hamna social media na Magufuli was anti vaccine huku USA almost half of Americans ni anti vaccine na alikuwa kama trump mambo yake .Very controversial and colorful na watu wanapenda watu kama dictator
 
Mazishi ya Rais Magufuli yanaweza kuweka historia ya kuhudhuriwa na watu wengi kuanzia kuaga hadi kesho atakapozikwa.

Kwa haraka haraka naona haraiki iliyomuaga na itakayomzika pamoja na matatizo ya corona, haijawahi kutokea.

Kwa hivyo, anaingia kwenye historia kama mtanzania aliyezikwa na watu wengi ukiachia mbali kufautiliwa na wengi duniani.

Nini mawazo yako juu ya dhana hii?

B3E48349-113C-486C-ADAE-775A50EE2294.jpeg


9D1D7C0B-94C2-4B00-9971-B6EEA963F3D8.jpeg
 
Mazishi ya Rais Magufuli yanaweza kuweka historia ya kuhudhuriwa na watu wengi kuanzia kuaga hadi kesho atakapozikwa.

Kwa haraka haraka naona haraiki iliyomuaga na itakayomzika pamoja na matatizo ya corona, haijawahi kutokea.

Kwa hivyo, anaingia kwenye historia kama mtanzania aliyezikwa na watu wengi ukiachia mbali kufautiliwa na wengi duniani.

Nini mawazo yako juu ya dhana hii?

Nyerere akasome babaa, Magu ni kipenzi cha watu.
 
Ni kosa kubwa kufananjsha msiba wa Nyerere na Magufuli,,kumbuka Nyerere alikufa kipindi TV ipo Moja mtaa mzima,Nyerere alikufa kipindi kumiliki simu na TV ni anasa..Nyerere alikufa enzi ya ujinga uliokubuhu na hakukua na utandawazi hapa Tanzania na miundo mbinu ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine ni ishu..pia Nyerere hakutembezwa mikoa yote hiyo,,Msiba wa Magufuli kinachofanyika kila anapokuwepo basi viongozi na wafanyakazi wengine wa serikali karibu wote wanahamia eneo hilo ,,,Tazama chato kuna magari mpaka yanatangaza nauli kwenda huko...

Mwisho usisahau huu msiba..hiyo ratiba na matukio mengi yamepangwa kiustadi ili kuwaprove wapinzani wa kisiasa wa Magufuli kuonesha kua alikua anakubalika...na pia sisi watanzania bila kujali mtu alikuaje ila unapokufa lazima tukuhurumie iwe mwema au mbaya..


Apumzike panapostahili Mh Rais Hayati Magufuli
MaCCM majinga mpaka yanaleta kichefuchefu maana mtu mwenye akili unawezaje kulinganisha Mlima Kilimanjaro na kichuguu cha Chato, kwanza Nyerere alifariki zaidi ya miaka 20 kabla ya kichuguu na pili alifariki akiwa Mstaafu karibu miaka 20 kichuguu amefariki akiwa madarakani. Nyerere maiti yake ilikuwa inalala palepale Uwanjani na haikuzungushwa kama bidhaa inatafuta wanunuzi bali iliagwa Dar na Butiama tu na mipango ilikuwa mizuri sana hakuna aliyekufa wala kujeruhiwa licha ya umati mkubwa wa waombolezaji waliofurika usiku na mchana. Nyerere ni Baba wa Taifa!
 
Waombolezaji wa maigizo kuzimia huku mifuko , chupa za juice hawaangushi ? Kuzimia gani huko? Hata aibu hamna .
 
Hajawahi kutokea mtu kama nyerere TANZANIA, usidanganywe na ccm hawa wa magufuli, yan nyerere umfananishe na magu ? jaman
Ni upumbavu kumfananisha Nyerere na Magufuli .Nyerere ni founder wa nchi unafanya mchezo kuchukuwa nchi kutoka kwa mkoloni nini .
 
NAJIULIZA TU MWENYEWE.

Mwaka 1999 Tanzania Ilikua Na Watu Wa Ngapi?.

Mwaka 2021 Tanzania Ina Watu Wa Ngapi?.

Vyombo Vya Habari Kati Ya Mwaka 1999 Na 2021 Je hesabu Zinalingana?.

Uelewa Wa Mambo Kwa Wananchi Ulikuaje mwaka 1999 Hivi Ni Sawa Na Mwaka 2021?

Mwaka 1999 Barabara zetu zilikua Ninamuwezesha Mwananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kushiriki au kushuhudia tukio na kurejera kwake kwa haraka?

Vyombo Vya Usafiri Vilivyotumika na Njia Za Kupashana Habari za Nyakati Hizo Zilikua Rafiki Kama Ilivyo sasa?

MAJIBU NI SIRI YANGU•
 
Back
Top Bottom