Je, Magufuli amemfunika Nyerere kwa waombolezaji kwa sababu ya mtandao au ni kweli?

Je, Magufuli amemfunika Nyerere kwa waombolezaji kwa sababu ya mtandao au ni kweli?

Mazishi ya Rais Magufuli yanaweza kuweka historia ya kuhudhuriwa na watu wengi kuanzia kuaga hadi kesho atakapozikwa.

Kwa haraka haraka naona halaiki iliyomuaga na itakayomzika pamoja na matatizo ya corona, haijawahi kutokea.

Kwa hivyo, anaingia kwenye historia kama Mtanzania aliyezikwa na watu wengi ukiachia mbali kufautiliwa na wengi duniani.

Nini mawazo yako juu ya dhana hii?
Huwezi kufanya comparison ya viongozi ambao wamefariki katika vipindi tofauti na mzazingira tofauti! Tofauti ya miongo miwili siyo ndogo.

Nyerere alifariki akiwa ameshatoka madarakani kwa muda mrefu. Zaidi ya miaka 15.. kwa hiyo kuna watu wengi tu walikuwa wamezaliwa hata hawajui kama nyerere alikuwa raisi,walikuwa wanasikia tu.Lakini Magufuli amefariki akiwa madarakani. Tofautisha mazishi ya raisi na mustafu. Huwezi kufanya mlinganisho wa namna hiyo.

Halikadhalika,population ya wakati huo ilikuwa ndogo ukilinganisha na sasa.

Miundombinu ya mawasiliano ilikuwa duni. Hakuna barabara za lami na magari ya kutosha. Hakuna tv. Ilikuwepo ITV peke yake. Hakuna mitandao ya simu. Hakuna internet. Kwa hiyo upashanaji habari ulikuwa mgumu.

Kwa sababu hizo na nyingine nyingi, huwezi kufanya ulinganisho wa vitu ambavyo premise hazifanani! Hivyo Magufuli kupata waombolezaji wengi siyo kielelezo cha kwamba alipendwa kuliko Nyerere. Kumbuka hata Ruge na Mengi walipata waombolezaji wengi kuliko Nyerere. Je walipendwa kumzidi Nyerere! Hapana.
 
Kabla hujafanya ulinganishi wako unatakiwa kufahamu Mwalimu alifariki miaka 15 baada ya kuwa ameshatoka madarakani wakati JPM amefariki akiwa bado madarakani! Jiulize, JPM huyu angekuwa na status ipi miaka 15 ijayo! Lingine, inawezekana wakati Mwalimu anafariki ama bado ulikuwa mdogo au bado ulikuwa unafukuzana na ng'ombe kijijini kwenu!

Binafsi wakati Mwalimu anafariki nilikuwa naishi Chang'ombe, Sigara!! Unlike JPM ambae watu walienda kwa mihemuko na matokeo yake wakajazana kwa wakati mmoja, Mwalimu alijengewa kakibanda kabisa ka vioo na shughuli ya kumuaga iliendelea usiku kucha.

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, ile shughuli iliendelea 3 days in a row, na wakati wote wote bado kulikuwa na foleni ndefu za watu kwenda kumuaga Mwalimu.

Nakumbuka ingawaje nilikuwa naishi jirani lakini nilishindwa kwenda kumuaga kwa sababu sikuweza kuvumilia kusimama kwenye foleni ndefu kila nilipoenda.
Kumbukumbu zako ni nzuri kabisa. Nyerere alipendwa acha kabisa. Hata waliomchukia hawakufikia kiwango cha kufanya sherehe.
 
Mimi Nilishuhudia Umati Mkubwa sana kifo cha Mwalimu kwani nilikuwepo Mwili kila njia uliyopita ilifungamana Watu wengi sana sana na kwenye kuaga Mwili wake pale Taifa siku tatu lakini haikutosha japo ilikuwa 24/7 me sikufanikiwa kupata nafasi na wengi sana hawakuweza so ilibidi wawe wanasimama barabarani tu Uwanja wa Ndege tuliingia hadi ndani kule Termnal 1 tulikaa hadi ndege ikapaa na kupotea angani ndipo tuliondoka... Maraisi wa nchi nyingi sana walikuwepo hadi wa Nchi ya Finland Bonge Nyanya alikuwepo na Museven pia alikuwepo... Wa Magufuli hajaja! kapunguza Idadi tayari
Uko sahihi kabisa!
 
Mazishi ya Rais Magufuli yanaweza kuweka historia ya kuhudhuriwa na watu wengi kuanzia kuaga hadi kesho atakapozikwa.

Kwa haraka haraka naona halaiki iliyomuaga na itakayomzika pamoja na matatizo ya corona, haijawahi kutokea.

Kwa hivyo, anaingia kwenye historia kama Mtanzania aliyezikwa na watu wengi ukiachia mbali kufautiliwa na wengi duniani.

Nini mawazo yako juu ya dhana hii?
Kwa hiyo amefufuka?
 
Mazishi ya Rais Magufuli yanaweza kuweka historia ya kuhudhuriwa na watu wengi kuanzia kuaga hadi kesho atakapozikwa.

Kwa haraka haraka naona halaiki iliyomuaga na itakayomzika pamoja na matatizo ya corona, haijawahi kutokea.

Kwa hivyo, anaingia kwenye historia kama Mtanzania aliyezikwa na watu wengi ukiachia mbali kufautiliwa na wengi duniani.

Nini mawazo yako juu ya dhana hii?
Nyerere hakuzungushwa mikoa kadhaa.Watu walilia machozi hayakuonwa na Instagram et al.
 
Nyerere akasome babaa, Magu ni kipenzi cha watu.
Acha mizaha yako.

Naamini Nyerere ameongoza wewe hujazaliwa,hivyo hakuna unachojua!

Nyerere was a great leader. Siyo Tanzania tu,bali Afrika na Dunia kwa ujumla.Legacy ya Nyerere ni ya kipekee. Kuna maeneo sehemu mbalimbali duniani yamepewa jina lake mpaka Uingereza kwa mama Elizabeth.
 
Mitandao,

Ongezeko la watu,

Kutembezwa vituo vingi

Mwisho Nyerere alikufa baada ya miaka 15 hivyo alishaanza kusahaulika.
 
Wenzetu waliotuzidi Akili na Kujitambua wanahangaika Kufafanisha Maendeleo yao ya Kiuchumi, kuzidi Kubuni Teknolojia mpya duniani huku wakipambana hivi sasa kutafuta Chanjo ya Janga baya la Corona ( Covid-19 ) Miswahili ( tena Kutwa inajitapa ni Misomi ) inakuja na Mlinganisho wa nani Kajaza Nyomi kati ya Hayati Nyerere na Hayati Magufuli.

Kuna Hoja ni za Kitoto halafu zinakera sana hata kama ukisema uzivumilie. Hivi ikiwa ni Nyerere au Magufuli Mmoja wapo amezikwa na Watu wengi hii Kiuchumi wa nchi na Maendeleo ya Mtanzania Mmoja Mmoja imeleta positive impact gani Kwao? Punguzeni Ujuha na Ushamba!!!
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
 
Tukizungumza suala la Chema, hapo Julius atapewa 100% kwa sababu Julius hakuwa na kundi la watu wa "kumuuza" kama ilivyo sasa lakini alijiuza mwenyewe!! Na wala sikumbuki kuoneshwa mavyuo, madaraja, mabwawa ya umeme, mashule, na mavitu kadhaa wa kadhaa alivyojenga! Wakati wa msiba wa Mwalimu zilitawala sana hotuba zake kuliko alivyojenga!! Kaseti za hotuba zake ziliuzwa sana bila kuambiwa kwamba ndie mjenzi wa UDSM, SUA, Mzumbe, CBE, na kadhalika, na kadhalika!!!
Halafu vingine vinavyoonyeshwa amejenga ni vile vilivyojengwa awamu ya mtangulizi wake yeye akaenda kuzindua mf. Daraja la Kigamboni,JNIA TERMINAL III, Hospital ya Mloganzila,nk
 
Hakuna msiba uliokuwa mzito kama wa Nyerere, hata nyimbo za maombolezo zilitayarishwa kwa weredi sana, hizi za Maghu ni wabana pua watupu, wanajiita all star wakati wapo watano tu.

Kifo Cha sokoine 1984, watu walikufa kwa mshituko, waliokufa kwa Maghu ni utaratibu mbaya tu hsukupangwa, watu wakakanyagana.
Ma MC wote walikuwa vilaza, Yule Mama hata kiswahili hajui vizuri, alikuwa anskosea hata majina ya viongozi, Uhuru Muigai Kenyata, akasema Mungai Kenyata, Tena akarudia mara tatu.

Shughuri nzima ilipingwa hovyo.

Kwanini hawakutumia watangazaji wa TBC, kama ma MC, wakaokoteza mijitu, isiyojua kitu.

Hata msiba wa Ruge na Mengi uliendeshwa vizuri.
watangazaji wa TBC waligoma kiaina mara nauguliwa mara niko safari nk

Jk nyerere weee thubutu mpaka leo wastani wa watu 100 kila siku wanaenda mwitongo kuhiji.
 
Acha mizaha yako.

Naamini Nyerere ameongoza wewe hujazaliwa,hivyo hakuna unachojua!

Nyerere was a great leader. Siyo Tanzania tu,bali Afrika na Dunia kwa ujumla.Legacy ya Nyerere ni ya kipekee. Kuna maeneo sehemu mbalimbali duniani yamepewa jina lake mpaka Uingereza kwa mama Elizabeth.

Hayo ni maono yako wala sikupingi


Magufuli âś”
Babu ❌
 
Unapolinganisha vitu, vilinganishe kiusawa.

Nyerere alipofariki mwaka 2000, Tanzania ilikuwa na idadi ya watu takriban milioni 33.

Mwaka huu 2021 aliofariki Magufuli, idadi ya Wtanzania imeongezeka karibu mara mbili, makadirio ya worldometrters.info yanatuweka kwenye zaidi ya watu milioni 61.

Unapolinganisha idadi ya watu waliotokea kwenye tukio la kitaifa miaka ya nyuma na sasa inafaa uangalie ongezeko hii la watu.
Na kuongezea nyama, mwili wa Nyerere uliagwa Dsm pekee, haukuzungushwa mikoani kama mbio za Mwenge. ..
 
Wangempelekea na mikoa kama singida, mbeya, arusha, songwe afu mngeleta hizo siasa zenu

Katika mikoa ambayo haikutegemewa kwa Marehemu kujizolea kura nyingi moja wapo kanda ya ZIWA/MWANZA. Nani alitegemea hayo??? Huko Arusha hatuhitaji kura zao, tunawajua kitambo tu, wengi wao wabinafsi na lichama lao.
 
Na kuongezea nyama, mwili wa Nyerere uliagwa Dsm pekee, haukuzungushwa mikoani kama mbio za Mwenge. ..
Ile habari ya kuizungusha maiti mikoani kama a circus show ni jambo la aibu sana.
 
MaCCM majinga mpaka yanaleta kichefuchefu maana mtu mwenye akili unawezaje kulinganisha Mlima Kilimanjaro na kichuguu cha Chato, kwanza Nyerere alifariki zaidi ya miaka 20 kabla ya kichuguu na pili alifariki akiwa Mstaafu karibu miaka 20 kichuguu amefariki akiwa madarakani. Nyerere maiti yake ilikuwa inalala palepale Uwanjani na haikuzungushwa kama bidhaa inatafuta wanunuzi bali iliagwa Dar na Butiama tu na mipango ilikuwa mizuri sana hakuna aliyekufa wala kujeruhiwa licha ya umati mkubwa wa waombolezaji waliofurika usiku na mchana. Nyerere ni Baba wa Taifa!
Mkuu punguza ukali wa maneno.
 
Back
Top Bottom