Je, Magufuli amemfunika Nyerere kwa waombolezaji kwa sababu ya mtandao au ni kweli?

Mimi Nilishuhudia Umati Mkubwa sana kifo cha Mwalimu kwani nilikuwepo Mwili kila njia uliyopita ilifungamana Watu wengi sana sana na kwenye kuaga Mwili wake pale Taifa siku tatu lakini haikutosha japo ilikuwa 24/7 me sikufanikiwa kupata nafasi na wengi sana hawakuweza so ilibidi wawe wanasimama barabarani tu Uwanja wa Ndege tuliingia hadi ndani kule Termnal 1 tulikaa hadi ndege ikapaa na kupotea angani ndipo tuliondoka... Maraisi wa nchi nyingi sana walikuwepo hadi wa Nchi ya Finland Bonge Nyanya alikuwepo na Museven pia alikuwepo... Wa Magufuli hajaja! kapunguza Idadi tayari
Ahsante sana, umethibitisha shaka yangu manake ndicho nimesema ingawaje sikuwa na kumbukumbu vizuri kama ilikuwa siku 3 au lah! Na kama ulivyosema, nakumbuka vema shughuli ya kuaga iliendelea usiku kucha, na watu hawakuwahi kupungua. Kwavile nilikuwa naishi jirani, nikasema wacha niende siku ya pili lakini nikakuta bonge la foleni! Nikasema wacha niende usiku lakini bado nikakuta bonge la foleni, kwahiyo nikashindwa ingawaje nilikuwa naishi jirani tu na shughuli ilienda 3 days in a row!!! Na hapo Mwalimu alishaondoka madarakani miaka 15 iliyopita!
 
Vitendo vip?

Vile vya kuwapeleka Uingereza Kina Kapten Maganga kujifunza Kuendesha na kutumia Vifaru vya kivita kuja kumtoa Iddy Amin Dada 1979?

Uwe Adui wa Mabeberu lakin muda wote Secretary wako binafsi ni Mzungu toka Ubeberuni Uingereza?

Uwe Mwiba wa Mabeberu lakin mfumo wako wote wa Ulinzi unapata mafunzo toka Israel?

Mwiba wa Mabeberu check up zako za Afya miaka yote unafanya Uingereza hata mwisho wako umefika ukiwa St Thomas Uingereza?

Kama Elimu yako ni ya Text books za 'Tanu yajenga Nchi' huwezi kufikiri nje ya wigo uliowekewa
Hivi upo objective au unaleta ushabiki?! Narudia, Mwingereza alikuja kumsaidia Mwalimu mwaka 1964 na yale hayakuwa MAPINDUZI bali MAASI! Na maasi yale yalifanyika MWAKA MMOJA TU baada ya uhuru!! Kwamba awe beberu wakati secretary wake ni mzungu hiyo ni hoja dhaifu kwa sababu ubeberu SIO rangi!!!! Kwamba eti aliwapelekea akina Maganda kujifunza kuendesha vifaru nayo ni HOJA DHAIFU kwa sababu hata JIWE mnayetaka kudanganya watu kwamba eti alikuwa anachukiwa na mabeberu bado mengi alikuwa anategemea huko huko!!!

Jiwe hajafanya lolote la maana la kuhitilafiana na mabeberu kama ilivyokuwa kwa Nyerere ambao walimkatia hadi misaada!! Ku-deal na Acacia huwezi kusema ali-deal na mabeberu kwa sababu Acacia ni wafanyabiashara tu, na Jiwe ana historia ya kutofautiana na Wafanyabiashara!!! Mwalimu alikuwa anawatunishia misuli TAASISI zenye nguvu kama World Bank, IMF, hadi Paris Club na sio individual business communities!!! Suala la eti alienda St Thomas nalo halina mashiko kwa sababu hata huyo Jiwe, hospitali aliyofia 99% ya vifaa vinatoka kwa mabeberu!!! Anatembea akisindikizwa na mavifaa ya kivita huku yote yakiwa yanatoka kwa mabeberu, lakini ukifika mwezi mchanga anawaadaa watu "hiyo chanjo inatoka kwa mabeberu" wakati misafara yake imejaa magari ya mabeberu!!!!

Na ninachokiona, ni wewe ndie unatumia siasa za "TANU yajenga nchi" huku ukiwa hujui hata historia yenyewe, na kama unajua basi umeamua kupotosha ili kumpaisha Mungu Mtu ambae PIGA UA, huwezi kumlinganisha na Nyerere hata robo!!!! Mtu kajenga hostel mnapiga kelele dunia mzima mnasahau watu wamejenga vyuo!! Mtu kajenga vipande vya reli, mnapiga kelele mnasahau watu wamejenga reli iliyokamilika!!! Mtu kanunua ndege na mnapiga mayowe kucha, huku mkisahau wengine walinunua ndege, magari, na matreni!! Mtu anafungua kiwanda cha Muhindi mnabaki kupiga yowe miaka kwa miaka huku mkisahau wengine walijenga viwanda na sio kufungua viwanda!!! Hivi mpo sawa kweli nyie watu?
 
Mazishi ya Rais Magufuli yanaweza kuweka historia ya kuhudhuriwa na watu wengi kuanzia kuaga hadi kesho atakapozikwa.

Kwa haraka haraka naona halaiki iliyomuaga na itakayomzika pamoja na matatizo ya corona, haijawahi kutokea.

Kwa hivyo, anaingia kwenye historia kama Mtanzania aliyezikwa na watu wengi ukiachia mbali kufautiliwa na wengi duniani.

Nini mawazo yako juu ya dhana hii?

Wenzetu waliotuzidi Akili na Kujitambua wanahangaika Kufafanisha Maendeleo yao ya Kiuchumi, kuzidi Kubuni Teknolojia mpya duniani huku wakipambana hivi sasa kutafuta Chanjo ya Janga baya la Corona ( Covid-19 ) Miswahili ( tena Kutwa inajitapa ni Misomi ) inakuja na Mlinganisho wa nani Kajaza Nyomi kati ya Hayati Nyerere na Hayati Magufuli.

Kuna Hoja ni za Kitoto halafu zinakera sana hata kama ukisema uzivumilie. Hivi ikiwa ni Nyerere au Magufuli Mmoja wapo amezikwa na Watu wengi hii Kiuchumi wa nchi na Maendeleo ya Mtanzania Mmoja Mmoja imeleta positive impact gani Kwao? Punguzeni Ujuha na Ushamba!!!
 
Simple
Nyerere alikufa akiwa rais mstaafu siku hiyo hata mimi nilienda msibani.
Magufuli amekufa akiwa kwenye kiti, si kawaida ndo mana Ataenziwa zaidi.
 
Mazishi ya Rais Magufuli yanaweza kuweka historia ya kuhudhuriwa na watu wengi kuanzia kuaga hadi kesho atakapozikwa.

Kwa haraka haraka naona halaiki iliyomuaga na itakayomzika pamoja na matatizo ya corona, haijawahi kutokea.

Kwa hivyo, anaingia kwenye historia kama Mtanzania aliyezikwa na watu wengi ukiachia mbali kufautiliwa na wengi duniani.

Nini mawazo yako juu ya dhana hii?
Technolojia imechangia ila chema chajiuza pia...
 
Kwo siku hizi misiba nimashindano ?? Ndo mana watu wanatwanga mbege safari namziki kwasababu mnefiwa badala yamhuzunike mnatafuta viewers namafolowaziii 😂😂😂turudi kwenye hoja idadi yawatu kipindi hicho nasaizi nitofaut,, ufatiliaji wakipnd hicho nasaiz nitofaut usingeweza kukusanya data za idadi yawatu wakati wanasikiliza wanaskiliza redio af TV kwa mjumbe siku hizi ukipost unaona waliokufata kiurahisi
 
Mazishi ya Rais Magufuli yanaweza kuweka historia ya kuhudhuriwa na watu wengi kuanzia kuaga hadi kesho atakapozikwa.

Kwa haraka haraka naona halaiki iliyomuaga na itakayomzika pamoja na matatizo ya corona, haijawahi kutokea.

Kwa hivyo, anaingia kwenye historia kama Mtanzania aliyezikwa na watu wengi ukiachia mbali kufautiliwa na wengi duniani.

Nini mawazo yako juu ya dhana hii?
Wanyonge mbona mnatapatapa sana, hata kwenye msiba mnaleta siasa!
 
Unapolinganisha vitu, vilinganishe kiusawa.

Nyerere alipofariki mwaka 2000, Tanzania ilikuwa na idadi ya watu takriban milioni 33.

Mwaka huu 2021 aliofariki Magufuli, idadi ya Wtanzania imeongezeka karibu mara mbili, makadirio ya worldometrters.info yanatuweka kwenye zaidi ya watu milioni 61.

Unapolinganisha idadi ya watu waliotokea kwenye tukio la kitaifa miaka ya nyuma na sasa inafaa uangalie ongezeko hii la watu.
Bila kusahau technology...
 
Technolojia imechangia ila chema chajiuza pia...
Tukizungumza suala la Chema, hapo Julius atapewa 100% kwa sababu Julius hakuwa na kundi la watu wa "kumuuza" kama ilivyo sasa lakini alijiuza mwenyewe!! Na wala sikumbuki kuoneshwa mavyuo, madaraja, mabwawa ya umeme, mashule, na mavitu kadhaa wa kadhaa alivyojenga! Wakati wa msiba wa Mwalimu zilitawala sana hotuba zake kuliko alivyojenga!! Kaseti za hotuba zake ziliuzwa sana bila kuambiwa kwamba ndie mjenzi wa UDSM, SUA, Mzumbe, CBE, na kadhalika, na kadhalika!!!
 
Nyerere anafaidika na enzi za utawala wake hakukua na uwazi, mitandao ya kijamii haikuwapo, watu wengi hawakua na exposure na vitu vingi hata wengi wao pia walikua na ufinyu wa kufikiria nje ya boks...
Nyerere kwa nyakati hizi angepata wapinzani wengi sana kwa staili aloyoitumia. Ni kama JPM...
 
Na pia kuangalia tofauti ya kiteknolojia, kwa sasa mawasiliano na vyombo vya habari vimeongezeka sana hivyo kuvutia watazamaji wengi zaidi ya 1999. Kwa hali ya kawaida Magufuli hawezi kumfunika Nyerere kwa njia yoyote ile.
Ila Mataga /Wanyonge wana tia hasira sana, yaani wanamlinganisha Nyerere na Jiwe 😠😠😠
 
Wasukuma kuweni wapole tu kufananisha inasaidia nini Nyerere alishang'atuka madarakani muongo mmoja ulishapita,,any ways jeuri yenu mjini kwishney
 
Hivi upo objective au unaleta ushabiki?! Narudia, Mwingereza alikuja kumsaidia Mwalimu mwaka 1964 na yale hayakuwa MAPINDUZI bali MAASI! Na maasi yale yalifanyika MWAKA MMOJA TU baada ya uhuru!! Kwamba awe beberu wakati secretary wake ni mzungu hiyo ni hoja dhaifu kwa sababu ubeberu SIO rangi!!!! Kwamba eti aliwapelekea akina Maganda kujifunza kuendesha vifaru nayo ni HOJA DHAIFU kwa sababu hata JIWE mnayetaka kudanganya watu kwamba eti alikuwa anachukiwa na mabeberu bado mengi alikuwa anategemea huko huko!!!

Jiwe hajafanya lolote la maana la kuhitilafiana na mabeberu kama ilivyokuwa kwa Nyerere ambao walimkatia hadi misaada!! Ku-deal na Acacia huwezi kusema ali-deal na mabeberu kwa sababu Acacia ni wafanyabiashara tu, na Jiwe ana historia ya kutofautiana na Wafanyabiashara!!! Mwalimu alikuwa anawatunishia misuli TAASISI zenye nguvu kama World Bank, IMF, hadi Paris Club na sio individual business communities!!! Suala la eti alienda St Thomas nalo halina mashiko kwa sababu hata huyo Jiwe, hospitali aliyofia 99% ya vifaa vinatoka kwa mabeberu!!! Anatembea akisindikizwa na mavifaa ya kivita huku yote yakiwa yanatoka kwa mabeberu, lakini ukifika mwezi mchanga anawaadaa watu "hiyo chanjo inatoka kwa mabeberu" wakati misafara yake imejaa magari ya mabeberu!!!!

Na ninachokiona, ni wewe ndie unatumia siasa za "TANU yajenga nchi" huku ukiwa hujui hata historia yenyewe, na kama unajua basi umeamua kupotosha ili kumpaisha Mungu Mtu ambae PIGA UA, huwezi kumlinganisha na Nyerere hata robo!!!! Mtu kajenga hostel mnapiga kelele dunia mzima mnasahau watu wamejenga vyuo!! Mtu kajenga vipande vya reli, mnapiga kelele mnasahau watu wamejenga reli iliyokamilika!!! Mtu kanunua ndege na mnapiga mayowe kucha, huku mkisahau wengine walinunua ndege, magari, na matreni!! Mtu anafungua kiwanda cha Muhindi mnabaki kupiga yowe miaka kwa miaka huku mkisahau wengine walijenga viwanda na sio kufungua viwanda!!! Hivi mpo sawa kweli nyie watu?
We fikiri hali yakifeza iliyokuwepo kipind hicho lakini mhuni katandaza mataaluma dsm to tunduma,,,lakini jamaa kipande kidogo tu cha reli wanamfagilia kama majaabu flan,,,
 
Nyerere anafaidika na enzi za utawala wake hakukua na uwazi, mitandao ya kijamii haikuwapo, watu wengi hawakua na exposure na vitu vingi hata wengi wao pia walikua na ufinyu wa kufikiria nje ya boks...
Nyerere kwa nyakati hizi angepata wapinzani wengi sana kwa staili aloyoitumia. Ni kama JPM...
Suala sio kupata wapinzani na ndo maana sijagusia popote suala la upinzani unless kama unamaanisha wakosoaji!! Kama issue ya uwazi na upinzani, rais pekee anayeweza kujigamba hivyo ni JK na ndo maana maufisadi maufisadi na maovu ya utawala wake YOTE yalifahamika wakati akiwa bado madarakani, na kwavile kulikuwa na uwazi, mengi kama sio yote yalifahamika wakati bado yupo Ikulu, na wapinzani walikuwa huru! Lile sakata la Lugola na Andengenye lingejadiliwa bungeni wazi wazi; lakini je, hivi hata wewe nikikuuliza hapo suala la Lugola na Andengenye limefikia wapi; unaweza kuwa na jibu? Hivi sasa huo upinzani upo wapi? Huo uwazi upo wapi? Lakini kubwa zaidi, hata kama Julius hakuwa na upinzani bado hiyo isingezuia watu kumpamba kwa sababu by 1999 tayari tulishakuwa na tv and radio stations kibao, na ambacho kilikosekana na internet "kwa wengi"!!
 
Kutazamwa na watu 3.9 billion siyo kitu cha kawaida,

Magufuli alikuwa kipenzi cha watu [emoji848]
Acha uongo! Source ya hizo data ni magumashi. Watazamaji 3.9 wa kiswahili unawapata wapi? Mbona mnapenda sifa za kishamba?
 
Back
Top Bottom