Je, mahakama ya Tanzania inaweza kuendeshwa kama mechi ya Simba na Yanga?

Je, mahakama ya Tanzania inaweza kuendeshwa kama mechi ya Simba na Yanga?

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Inajulikana ndani ya mahakama kunakuwa na mchuano mkali wa hoja za ,utaratibu na ushahidi bila mihemuko.

Je ni sahihi kuwa na mashabiki wa pande mbili kila mmoja akivutia upande wake?

Wakati Yesu anahukumiwa pasipo haki pilato alisimama mbele ya wayahudi akawa anahoji baadhi ya maswali muhimu na akawa anapima upepo kwa kusikiliza sauti nyingi zinasemaje ,japo hakuona ushahidi wa kumhukumu Yesu ilimbidi tu amalize kesi pasipo haki kwa kuwa kelele zikikuwa nyingi na akatoa hukumu bila ushahidi wa dhahiri akamhukumu Yesu kutundikwa msalabani japo ilikuwa sio sawa.

Je, tuendeshe mahakama zetu kwa mfumo huo?

#logic
 
Back
Top Bottom