Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Nafasi ya Waziri Mkuu Tanzania imekuwa mwiba mchungu kwa miaka mingi dhidi ya Marais waliopo Madarakani.
Pamoja na kwamba Marais ushiriki kupendezekaza jina la Waziri Mkuu; wengi uwaona kama watu wenye nguvu na ambao usipokaa nao kwa akili wanaweza kukuoutsmart.
Kati ya mawaziri wakuu waliowahi kuwepo ni wawili tu ndio waliokosa uwezo na ushawishi wa kutishia nafasi ya Rais aliyepo na anayekuja. Mzee Pinda by nature hakuwahi kuwa tishio kwa JK same as Frederick Sumaye kwa Mkapa.
Mawaziri wakuu waliobaki wamejipambanua kwa umahiri na hivyo kuwafanya waonekane kama wanauwezo mkubwa kuliko Marais.
Mfano mmoja ulio wazi ni nguvu ya Kisiasa aliyokuwa nayo Lowasa; kwa nguvu aliyokuwa nayo ilimfanya JK na baadaye JPM baada tu yakuingia madarakani kuhamisha majukumu ya tawala za mikoa na serikali za mitaa kwenda ofisini kwake kwa lengo la kumpunguzia nguvu Waziri Mkuu.Kumbuka huyu ni mteule wake lakini nafasi hiyo ilionekana tishio kwa JPM na akaona arejeshe serikali za mitaa kwake na Serikali kuu Pia.
SSH kama alivyofanya mtangulizi wake siyo tu kwamba anasimamia tawala za mikoa bali anasimamia pia Serikali kuu ila ameweka Makamu Waziri Mkuu si kwa lengo jingine bali kuionyesha nafasi ya Uwaziri Mkuu kwamba siyo nafasi nzuri sana kiutawala kwa sababu inakuexpose kuliko aliyekuteua.
Kasimu Majaliwa na Mama Samia awana ugomvi wowote. Bali nafasi ya Urais na Uwaziri Mkuu zina ugomvi mkubwa na wa muda mrefu. Ugomvi wa nafasi hizi mbili unawezalinganishwa na ugomvi wa nafasi ya Urais na Makamu wa Rais huko Kenya kwa sasa.
Ugomvi mkubwa uliopo katika nafasi ya Waziri Mkuu ni kwamba, kama ambavyo Rais anapokuwa mwenyekiti wa chama anaweza kusema hakuna fomu zaidi ya ile ya mwenyekiti katika kugombea Urais basi Waziri Mkuu naye anaweza akatamka au wapambe wake wakatamka kwamba yeye ndiye mrithi wa Rais ajaye na mchezo unaishia hapo. Hali hii imepelekea Rais aliyepo kupewa vitisho na maneno mengi yanayomfanya wakati wote aishi akiogopa kivuli cha kiti cha Waziri Mkuu.
Lakini pia hata Makazi ya viongozi hawa na mgawanyo wa majukumu yamekuwa na kizungumkuti. Haya yote ufanyika na wataalam wa siasa kumfanya Rais asiwe rafiki wa kiti cha waziri Mkuu ila awe Rafiki wa Waziri Mkuu. Kwa maana nyingine, wanaowaza kuwa warithi wa kiti cha Urais wamekuwa na nguvu kubwa yakupambana na kukidhoofisha kiti cha Waziri Mkuu kuliko nafasi nyingine yoyote. Nataka kusema nini! Watu wanaotaka kugombea Urais au wanaoandaliwa wapo kwenye risk sana wakipewa nafasi ya waziri Mkuu. Kama unataka Urais kwa mfumo huu wa vita kati ya viti hivi viwili bora ubaki kama waziri wa kawaida au uwe nje ya siasa za juu.
Hata hivyo, kwa kuwa nafasi ya Waziri Mkuu ni moja, na ili kuondoa fikra zakuzuia wagombea urais wengi kwamba waziri Mkuu ni tishio napendekeza iwe wazi kwamba ukishika nafasi ya Waziri Mkuu utakuwa umepoteza sifa ya kugombea Urais.
Tukiweka mazingira haya yakawa ya kitamaduni au kisheria itamsaidia RAIS aliyepo kuwa na amani na Waziri Mkuu kama nafasi ya uongozi sambamba na Waziri Mkuu kwa personality. Lakini pia itasaidia mteule kwenye nafasi hii awe the most competent person ambaye hatakuwa na fikra za kushika nafasi ya juu zaidi.
Kinyume na hapo Waziri Mkuu wa Tanzania ataendelea kuandamwa na vita ya madaraka kutoka juu, chini, mashariki na Magharibi na hivyo kukosa uhuru wa kumsaidia Rais na kuwasaidia wananchi. Namwona Kasimu Majaliwa akiwa na malengo makubwa kumsaidia Rais lakini mfumo unamkataza kufanya hivyo. Anachoweza kufanya kutamka kwa dhati ya moyo wake kwamba hana mpango wa kugombea Uraisi; hii itampunguzia kupigwa vita na kumfanya asifanye kwa viwango vile.
Wanafalsafa na wanataaluma sijui kama nimewaza sahihi ila ukweli ni kwamba vita ya viti hivi ni kubwa zaidi. Tusaidie mawazo ya kutatua vita hii ambayo hata kikiingia chama kingine lazima tu viti hivi viwili vitaendelea kugombana.
Kiti cha Makamu wa Rais hakina vita kwa sababu kimenyamazishwa kwenye muundo wa Muungano. Kwamba utaangaika na Muungano na Mazingira and that Y Mzee wa Kigoma katika macho ya nje siyo threat ; ila Waziri Mkuu anapotakwa kuwa ndiye Msimamizi wa shughuli za serikali na anakaa muda Mwingine na Wabunge na kwa kuzingatia wabunge ndio wanaochora michango ya kupata kura........this vita will never end.
Let us fight hii vita kwa kumpiga marufuku waziri Mkuu ajaye asiwe na maono ya Urais ili awe uru kuhudumia wananchi kwa vipawa alivyojaaliwa.
Food for thought from Sato Land to My Mama Tanzania