Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Hizi tuhuma zimekuwepo kwa muda mrefu kuwa watanzanzania au raia wa nje wanapotaka kwenda nje hutakiwa kupima Covid-19 na kupatiwa cheti kuonyesha kuwa hawana maambukizi.
Lakini kumekuwa na na tetezi zinazogaa mitandaoni kuwa mamlaka husika hapa Tanzania hazitoi majibu sahihi. Na mara zote watu wakipima wanaambiwa hawana maambukizi. Ila wakienda nje ya nchi wanapopimwa wanakutwa na maambukizi.
Hivi mamlaka husika mnaficha ili iweje? Kwamba Tanzania kutokuwa na maambukizi ndio sifa?
Leo hii kuna watanzania watatu huko Angola wameonekana na maambukizi,ina maana hapo maabara kwenu hamkugundua? Au mnataka kusema maabukizi wameyapata huko Angola?
Mnadhani UK ilikosea bahati mbaya kupiga marufuku watanzania kuingia huko kwao?
Kuweni wakweli maana mmeanza kuaibika.