Iliwahi kuwa hivyo, hasa enzi zile za mipakani na madereva wa malori.
Hiyo ilikuwa enzi hizo, sidhani enzi hizi hilo linawezekana tena!
Taasisi kama Muhimbili ikubali kuchafuka kwa sababu tu za kisiasa? Ni vigumu kuamini.
Kwanza tafuta ni nani wanaopima, halafu wachunguze kwa makini. Ni nadra sana taasisi za aina hiyo kufanya mambo kinyume na taratibu za kitaaluma.
Kuna mengi yanayotokana na kujiharibia jina kimataifa kwa sababu za kijingajinga tu zinazosimamiwa kisiasa.
Kwa mfano: Maabara Muhimbili hawawezi kukata kona na kufanya vipimo kivingine mbali ya njia zinazotakiwa ili yapatikane matokeo wanayoyataka wanasiasa; na hawawezi kutoa cheti kinachoonyesha matokeo tofauti na yale yaliyoonyeshwa na vipimo vyao.
Kwa ufupi ni hivi: kutakuwa na mambo tusiyoyajua yaliyofanyika juu ya vipimo vya hao waliogundulika kuwa wana maambukizi. Ni maabara zipi zilizopima na kutoa majibu? Maabara hizi ziko 'certified' kufanya kazi hiyo na matokeo ya vipimo vyao kutambulika kimataifa?