Je, maneno na watu wa kibiblia kwenye Qurani ni Copypaste za kwenye Biblia?

Je, maneno na watu wa kibiblia kwenye Qurani ni Copypaste za kwenye Biblia?

Quran imetaja majina ya watu ambao tayari biblia ilishawataja zamani miaka zaidi ya 1000 kabla ya kuzaliwa mtume wa waislam.

Quran imetaja story zinazofanana na story za kwenye biblia au maandiko ya kiyahudi yaliyokuwepo miaka zaidi ya 2000 kabla ya kuzaliwa mtume wa waislam.

Nini chanzo cha hizi story kuonekana humo?. Najiuliza. Kama mwenyezi Mungu alisahau kitu huko nyumq kwa nini asingeleta story na mambo mapya ili yaonekane ni mbadala wa yale yaliyokuwepo?

Je hizi ni moja ya sababu?

1: Kwa sababu ukristo ulikuwepo uarabuni zaidi ya miaka 600 kabla ya kuzaliwa Mtume wa waislam, basi zilichanganywa ili kuvuta wafuasi.

2: Kwa sababu Mtume wa waislam alipotokewa na kitu asichokifahamu, mkewe mkubwa alimpeleka kwa mkristo ili amsaidia ndugu Waraqa. Na kazi ya huyu waraqa ilikuwa ni kutafsiri maandiko ya biblia kwa kiarabu, basi kuishi hapo ambapo alitabiriwa utume alipata ideas mbili tatu kuhusu mambo yaliyokuwemo kwenye maandiko ya wakristo na wayahudi.

3: Kile kilichomtokea pangoni ndio kilimpa hayo maagizo na kumpa tips zinazoendana na maandiko kabla yake ila zikiwa zimechanganywa ili kuleta utofauti.

4: Au yale yalikuwa ni maelekezo ya Allah ambayo hayatakiwi kuhojiwa wala kuzungumziwa wala kulinganishwa na chochote.

Wajuvi mtujuze sisi wenye akili viherehere tusiona mipaka kujifunza mambo.

Comments ziheshimu imani za watu.
Mpinga kristo!!!
 
Attachments

  • TAMU.mp4
    3.8 MB
Usikate tamaa unapotaka kujifunza kitu, iko hivi Mwenyezi Mungu ameilinda Quran isiharibiwe na watu kwa sababu Muhammad ni Mtume wa mwisho, yaani hakuna tena Mtume mwingine atakayekuja baada ya Muhammad mpaka mwisho wa dunia. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu ameahidi kuilinda Quran isiharibiwe na wanaadamu ili vizazi vyote vitakavyokuja vikute ujumbe ule upo vile vile bila kuharibiwa.

Na kuhusu vitabu vya Injili na Taurati Mwenyezi Mungu aliwaacha wanaadamu wafanye watakavyo kwani kwa wakati ule Mitume bado walikuwa wanaletwa kwa hivyo wale wanaokuja walikuwa wakisahihisha makosa yaliyofanywa na wafuasi wa Mitume waliopita.

Usifikiri Mwenyezi Mungu hataacha kuwaadhibu wale waliobadilisha maandiko Yake matakatifu, atawaadhibu tu siku ya Kiama.

Hebu cheki You Tube Kuna mama mmoja mmarekani mzungu anaitwa Nur Nasir (alitumia jina hili baada ya kusilimu) unaweza ukaangalia story yake ya conversion from Christian to Islam kwenye You Tube. Huyu mama amefanya utafiti mwenyewe kwa kutumia kitabu cha Biblia na mwisho wa utafiti wake akaona kuwa Yesu sio Mungu wala si mwana wa Mungu bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Baada ya kuthibitidha hili kupitia vitabu vyake mwenyewe yaani Gospel na Torah ndio akaamua kusoma Quran na mwisho akasilimu. Mwanzoni alikuwa haiamini kabisa Quran kwa hivyo hakuisoma kabisa mpaka alipofanya utafiti wake mwenyewe kupitia Bible.

Na kuna kijana mwingine from China ambaye alisilimu huko Singapore huyu yeye alimuomba Mwenyezi Mungu amuonyeshe kati ya Quran na Bible ipi ni kweli? Na Mwenyezi Mungu akamuonyesha. Akasilimu (ukienda You Tube angalia Chinese man convert to Islam in Singapore by the name Sherald.

Si kwamba vitabu vya Taurati na Injili ni havifai moja kwa moja hapana, ni maneno ya Mwenyezi Mungu na ni vitabu vyake isipokuwa wanaadamu wameharibu baadhi ya maandiko katika hivyo vitabu.

Kama una nia ya kuutafuta ukweli basi muombe Mwenyezi Mungu akuongoze katika njia sahihi, muulize Mwenyezi Mungu ukweli ni upi na Yeye atakuonyesha. Itabidi ujitose katika kusoma kwa bidii na kumuomba Mungu na Yeye atakuonyesha njia sahihi.
Una kifungu chochote kuwa quran isiharibiwe kwa sababu Muhammad ni mtume wa mwisho.

Vitabu vyote vya mwenyezi Mungu kabla ya mtume viharibiwe hadi atakapokuja mtume.

Umeandika uongo mkubwa sana ambao hata mtume akisimama na wewe mbele ya kiti cha hukumu cha Yesu atakukana.

Wakati mtume anatokewa na jibril pangoni alipelekwa kwa Waraqa. Hadith sahih Bukhari imeweka wazi kuwa huyu Waraqa alikuwa anatafsiri injil. Maana take hadi mtume anapata huo unaoitwa utume injil ilikuwepo.

Katika nguzo za uislam, zinawataka waamini vitabu vya mwenyezi Mungu yaani Injil, Zabur na taurat. Sasa mnanguzo ya uongo. Maana Imani chanzo chake ni kusikia neno la Mungu, sasa utasikiaje kitu ambacho hakipo.

Umeandika contradictions
 
Sio kweli,ingekuwa Qur'an imecoppy Biblia.Ingekubaliansa moja kwa moja na
1.Kusulubiwa kwa Yesu,QUR'AN imekataa kama Yesu kasulubiwa.
2.Kuuwawa kwa Yesu,Qur'an imekataa kama Yesu kauwawa.
3.Kufa kwa Yesu,Qur'an imekataa kama kufa.Inasema hakufa,yuko hai,mbinguni
4.Kuzikwa kwa Yesu,Qur'an inakataa kuzikwa kwa Yesu,inasema hakuuwawa,hakuzikwa,yuko hai,mbingumi.
Na mengine mengi,yapo yanaotofautiana
1.Kama habari za Paulo,hazimo kwenye Qur'an
2.Kuolewa na fundi seremala kwa Mama wa Yesu,na Yoseph hazimo kwenye Qur'an
3.Ibada za kiislamu zipo tofauti kabisa na za ndani ya biblia,hazifanani kabisa.
4.Mtoto wa kiislamu,akizaliwa anakuwa muislamu,moja moja,lakini kwenye biblia,mpaka mtoto abatizwe.
5.Katika nyumba za ibada za waislamu,kiongozi wa ibada,anafanya ibada kama wengine,anaowaongoza,wakati katika biblia kongozi,anafanya ibada tofauti na anaowaongoza.
6.Quran imebaki katika lugha ya asili,ilitafsiriwa inahesabiks ni tafsiri sio Qur'an wenyewe.Lakini biblia,tafsiri inahesabika ndio biblia yenyewe.
7.Qur'an ukianza kuisoma,ni lazima umlani shetani,wakati biblia ukiiosoma,humlani shetani,unasoma moja kwa moja tu.
8.Nk
Imekopi mambo mengi kimakosa inaonekana lengo ni kukifanya kionekane kitabu hicho kinauhusiano na Mungu wa kwenye agano la kale na jipya ili kiwe na sura ya udini. Vibginevyo kingekuwa kama vitabu vya kihindu.

Lengo kuu inaonekana ni kumuhafifisha Yesu na wokovu aliouleta, ili wanaoufuata uislam wakose matumaini maana hata wanaomfuata hana uhakika na hatma yake.

Kile kitabu kimekaa kimtego sana, inahitaji akili kubwa kujua kinaweza kuwa kimefunga watu mamilioni wasione mpango wa Mungu wa kumrejeza mwanadamu katika hadhi aliyomkusudia kabla ya kudanganywa eden.
 
ALAH alishusha vitabu 4.

TORATI-- --MUSA
ZABURI --DAUDI.
INJILI--ISSA(YESU)
FURQAN --MUHAMAMAD(SAW).

Tofauti ya ukiristo na uislam Ni vitu 2 tu.

--YESU sio MINGU.
--YESU hakusulubiwa msalabani.

--ALAH(MUNGU) --Hana mtoto,,Hana mke,wala hakuzaa wala hakuzaliwa.

Ukiangalia mengine yote yanafanana.

Hata YESU pia alisema kwenye INJILI KWAMBA,,,,
SIKUJA KUTENGUA TORATI BALI KUITIMILIZA.

means MUNGU huyo huyo wa MUSA ndy wa YESU,
MUNGU wa MUSA ndy MUNGU wa MUHAMMAD (SAW).
amri Kumi ya TORATI ya MUSA ndy amri Kumi za MUNGU WA MUHAMMAD..

DINI Ni moja Ila imeingiliwa na binadamu wakaichafua ndy utofauti wa uislam na ukristo..

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
Kati ya Biblia na Quran ipi ilianza?
Acha kupotosha watu ndugu.
 
Sio kweli,ingekuwa Qur'an imecoppy Biblia.Ingekubaliansa moja kwa moja na
1.Kusulubiwa kwa Yesu,QUR'AN imekataa kama Yesu kasulubiwa.
2.Kuuwawa kwa Yesu,Qur'an imekataa kama Yesu kauwawa.
3.Kufa kwa Yesu,Qur'an imekataa kama kufa.Inasema hakufa,yuko hai,mbinguni
4.Kuzikwa kwa Yesu,Qur'an inakataa kuzikwa kwa Yesu,inasema hakuuwawa,hakuzikwa,yuko hai,mbingumi.
Na mengine mengi,yapo yanaotofautiana
1.Kama habari za Paulo,hazimo kwenye Qur'an
2.Kuolewa na fundi seremala kwa Mama wa Yesu,na Yoseph hazimo kwenye Qur'an
3.Ibada za kiislamu zipo tofauti kabisa na za ndani ya biblia,hazifanani kabisa.
4.Mtoto wa kiislamu,akizaliwa anakuwa muislamu,moja moja,lakini kwenye biblia,mpaka mtoto abatizwe.
5.Katika nyumba za ibada za waislamu,kiongozi wa ibada,anafanya ibada kama wengine,anaowaongoza,wakati katika biblia kongozi,anafanya ibada tofauti na anaowaongoza.
6.Quran imebaki katika lugha ya asili,ilitafsiriwa inahesabiks ni tafsiri sio Qur'an wenyewe.Lakini biblia,tafsiri inahesabika ndio biblia yenyewe.
7.Qur'an ukianza kuisoma,ni lazima umlani shetani,wakati biblia ukiiosoma,humlani shetani,unasoma moja kwa moja tu.
8.Nk
Wakristo hawamtumbui Issa bali wanamtambua Yesu kristo aliyesurubiwa msalabani na siku ya tatu akafufuka na hana uhusiano wowote na Issa.
Ila waislamu wanamtambua Issa wakimaanisha Yesu. Ukimuuliza muislam yoyote kuhusu Issa atakuambia ndiye Yesu wa kwenye Biblia.
Quran imenukuu kutoka kwenye biblia
 
Una kifungu chochote kuwa quran isiharibiwe kwa sababu Muhammad ni mtume wa mwisho.

Vitabu vyote vya mwenyezi Mungu kabla ya mtume viharibiwe hadi atakapokuja mtume.

Umeandika uongo mkubwa sana ambao hata mtume akisimama na wewe mbele ya kiti cha hukumu cha Yesu atakukana.

Wakati mtume anatokewa na jibril pangoni alipelekwa kwa Waraqa. Hadith sahih Bukhari imeweka wazi kuwa huyu Waraqa alikuwa anatafsiri injil. Maana take hadi mtume anapata huo unaoitwa utume injil ilikuwepo.

Katika nguzo za uislam, zinawataka waamini vitabu vya mwenyezi Mungu yaani Injil, Zabur na taurat. Sasa mnanguzo ya uongo. Maana Imani chanzo chake ni kusikia neno la Mungu, sasa utasikiaje kitu ambacho hakipo.

Umeandika contradictions

Ni kweli sisi waislamu tunaamini Injili, Zaburi na Taurati ni vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyoteremshwa kwa Mitume tofauti kwa zama zao, ila sasa kuna kitabu cha nne ambacho ni Quran kilicho teremshwa kwa Mtume wa sasa ambaye ni wa mwisho ambaye ni Muhammad (SAW).

Hivyo vitabu vyote vilivyotangulia kama mikono ya waandishi haikuharibu maneno yao yangekuwa sawa sawa na Quran tu kwa sababu vitabu vyote vimeteremshwa na Mungu huyo huyo mmoja. Hizi tofauti zimeletwa na wafuasi wa Mitume waliopita ambao ndio walibadilisha baadhi ya maneno kwenye vitabu vya zamani.

Quran haijawahi na haiwezi kubadilishwa mpaka mwisho wa dahari. Ni ahadi ambayo Mwenyezi you ameahidi na ndio mana hadi leo miaka 1400 bado ipo vile vile.
 
Hivyo vitabu vyote vilivyotangulia kama mikono ya waandishi haikuharibu maneno yao yangekuwa sawa sawa na Quran tu kwa sababu vitabu vyote vimeteremshwa na Mungu huyo huyo mmoja.
Allah alikuwa wapi waandishi wakiharibu vitabu vyake ?

Na toka kitabu chake Cha mwisho kiharibiwe ilimchukua mda gani kuleta kingine?
 
Ni kweli sisi waislamu tunaamini Injili, Zaburi na Taurati ni vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyoteremshwa kwa Mitume tofauti kwa zama zao, ila sasa kuna kitabu cha nne ambacho ni Quran kilicho teremshwa kwa Mtume wa sasa ambaye ni wa mwisho ambaye ni Muhammad (SAW).

Hivyo vitabu vyote vilivyotangulia kama mikono ya waandishi haikuharibu maneno yao yangekuwa sawa sawa na Quran tu kwa sababu vitabu vyote vimeteremshwa na Mungu huyo huyo mmoja. Hizi tofauti zimeletwa na wafuasi wa Mitume waliopita ambao ndio walibadilisha baadhi ya maneno kwenye vitabu vya zamani.

Quran haijawahi na haiwezi kubadilishwa mpaka mwisho wa dahari. Ni ahadi ambayo Mwenyezi you ameahidi na ndio mana hadi leo miaka 1400 bado ipo vile vile.
Kwa nini vitabu vyoote vipqkaziwe kuharibiwa na waandishi, wakati mfumo wa Mungu kabla ya quran alikuwa anawaagiza watu wake waandike.

Mungu huyu Allah yeye inaonekana ni mpya maana haamini katika kuandika (permanent storage).
1: Hakuwahi Kuagiza kitabu cha Quran kiandikwe.
2: Hata Mohammad mwenyewe hakuwahi kumuagiza mtu yeyote aandike hicho kitabu.
3: Aliagiza watu wakariri. Wakitunze kichwani (Temporary storage) inaonekana hayo maneno yalikuwa ninya muda mfupi tu, alafu yale ya mitume na manabii kabla ya huyu unayemtetea ndio yalikuwa yakudumu ndio maana yapo hadi kesho licha ya kupakaziwa kuchakachuliwa.

Nani aliagiza Quran au Mushaf uandikwe.
1: Ni kiongozi wa Kisiasa rafiki yake mtume Caliph Uthman.

Lini?
Karibu miaka 20 baada ya kifo cha Mohammad mwaka 650BK.

Calif abubakar hakufanya hivyo.
Calif Umar hakufanya hivyo.
Hii inakifanya kuwa kitabu cha kutiliwa shaka sana kuliko vitabu vyote vya kidini maana baada ya kufanya hivyo kinyume na maagizo ya Allah wala Mohammed aliagiza manuscripts ambazo zilitumika kukitengeneza (Yale magombo waliyokuwa wanatumia kuandika ili wakariri) aliagiza yachomwe moto.

Quran ndio kitabu pekee cha kidini ambacho huwezi kwenda uarabuni ukafanya excavation ukakutana na ushahidi hata wa ngozi au jiwe au kipande cha katatasi za zamani ambazo ukizisoma zinamaneno yanafanana angalau na hicho kilichomo kwenye hii compilation ya Kiongozi wa wa kisiasa na kidini Caliph Umar wa Islamic Calphate ya wakati wake.

Wakati makusanyo ya kitabu vya biblia, Juzijuzi tu wamekuta kwenye vyungu katika kuchimba kuna karatasi za karne ya kwanza zenye makusanyo karibu yote ya hiki tunachokiita agano jipya leo (Sinai Manuscripts).
Dead sea scrolls nyingi za kale zanachimbuliwa kila leo wanakutana na magombo ya kale hata kabla ya Yesu yenye maandishi ambayo ukifungua kwenye biblia inayotumika leo unayakuta yanafanana.

Mkuu haya mambo nje ya JF huwezi kuyasikia msikitini.

Ndio maana ili kuficha hizi siri, Quran imewekwa katika mfumo wa viapo. Kila sentensi ni kama kiapo havina ushahidi na hauhitaji kuhoji.
 
Wapo wanazuoni wanadai Wakatoliki ndio waliounzisha uislam kupitia watawa wa kiJesuit,lengo kuu ni kuwaweka waarabu under one control sababu ilikua ni vigumu kuwacontrol sababu walikuwa wakiabudu masanamu.
Ndio unaona huo mfanano wa Quran kukopi maandiko ya Biblia.
dini zote Dunia ni branch ya ukatoliki ikiwemo uislam.Ndo maana ya church and churches.
Kwanini waliamua kuanzisha uislam badala ya kusambaza injili?
 
Back
Top Bottom