Je, Mapambano ya Wanaharakati na Diamond yana faida kwa nchi?

Hajakatazwa kuwa mwanaccm , alichotakiwa kujiongeza nacho ni kupiga watu kurundikwa kwenye viroba na maiti kuokotwa ufukweni , watu kutekwa
Kama sijaona mtu aliyetekwa, utaniaminisha vipi kwamba watu wanatekwa. Vile vile Kuna uthibitisho wowote kwamba hayati Magufuli aliteka watu. Na kutekwa kwa watu Kuna uhusiano gani na fani yake ya mziki. Kwanini mlazimishe akili zifanane
 
ana elimu gani ? kwa sababu mafunzo huyapata wenye akili
Ana elimu ya form four lakini amewaajiri watu wengi wenye degree. Vile vile akili na elimu ni vitu viwili tofauti. Kwahiyo naweza kusema Mondi ana akili sana ndo maana amefanikiwa
 
Hao "wanaharakati" waliosimama upande wa haki ni akina nani? Wako wapi? Lissu alipoitisha maandamano hayo pichani walitokea? View attachment 1811498
Wanaharakati ni wale waliokua wanasema ATCL haina faida bali ina hasara,waliokua wanatupasha habari juu ya maiti zilikua zinaokotwa kwenye fujo za koko bichi zikiwa kwenye viroba,waliokua wanasema SHUJAA ni mgonjwa na nyie mkawa mnapinga hao ndio wanaharakati niliowakusudia


Kuhusu watanzania kutoitikia maandamano hilo ni suala la muda tu wala lisikutie shaka ipo siku miongoni mwa masiku litakuja tokea tu pengine ukiwa hai au wakati huo umetangulia mbele za haki
 
Hata firaauni PHARAOH aliijenga misri lakini alikua dhalimu
 
Ni jukumu la kila mtu
Tanzania watu 60M, ukimuondoa diamond na Magufuli watabaki 60M . Sasa Kuna haja gani kutaka kurudisha maendeleo ya mtu nyuma kisa tu mlitofautiana mitazamo. Kwa point kama hizi hayati Magufuli huwa anatumia kwa kusema wapinzani wanakwamisha maendeleo
 
Asante kwa maoni yako lakini kwa nini isiwe hasara iliyopatikana kutokana na matendo yake?

haya ni mambo mawili yasiyo fanana kabisa soma vizuri pingamizi lote kwa nini Diamond anashutumiwa.
Pingamizi dhidi ya diamond ni kwa sababu ya kutosimama upande wa haki kwa mujibu wa hao wanaharakati
 
Pingamizi dhidi ya diamond ni kwa sababu ya kutosimama upande wa haki kwa mujibu wa hao wanaharakati
Kuchagua au kuchaguliwa ni haki ya kila raia. Yeye kasimamia haki yake ya kuchagua upande anaoupenda. Hapo shida iko wapi
 
Tanzania watu 60M, ukimuondoa diamond na Magufuli watabaki 60M . Sasa Kuna haja gani kutaka kurudisha maendeleo ya mtu nyuma kisa tu mlitofautiana mitazamo. Kwa point kama hizi hayati Magufuli huwa anatumia kwa kusema wapinzani wanakwamisha maendeleo
Lakini yeye mwenyewe amesema hakuna wa kuweza kumshusha,means kwamba hakuna wa kumkwamisha mambo yake
 
Kumbe ukiwa msanii huruhusuwi kuwa mwanachama wa chama siasa?
 
Hoja ni kwamba anafatitiliwa na watu wengi sana. Hiyo 25000 ni watu na milioni 10 ni watu pia sasa 25000 wakikukataa wakati unakubalika na watu m. 10 huoni kama ni move ya kutafuta sehemu ya kutolea machungu. Kusaini kuna ugumu gani?
Sio wanakukataa Ila Wana ku disapprove hiyo ni kitu tofauti
 
Hajakatazwa kuwa mwanaccm , alichotakiwa kujiongeza nacho ni kupiga watu kurundikwa kwenye viroba na maiti kuokotwa ufukweni , watu kutekwa
Watu hawaelewi ishu ya kuvunja haki za binadamu ni mziki unao weza kumkosti mtu hadi dunia mzima ikamchukia
 
Sasa na wanaharakati wamechagua kuwasemea watu,sasa wakisema kwa BET kua msanii kwenye kinyang'anyiro chao ana support udhalimu Kuna shida gani
Watamtupa nje ya kinyang'anyilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…