Je, marais wa Afrika wameambizana kutumia magari ya Toyota kwenye safari zao?

Je, marais wa Afrika wameambizana kutumia magari ya Toyota kwenye safari zao?

Dede 01

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2024
Posts
1,182
Reaction score
2,248
Habari wakuu!

Wakati natazama ujio wa marais wa Afrika kwenye ukumbi wa JNICC nimegundua ya kuwa viongozi wengi waliowasili wametumia magari yanayofanana kimuundo na yote yametengenezwa na Toyota.

Kwa wale wajuvi wa mambo naomba mnieleze ni kwanini magari yao yanafanana na ni kwanini wanatumia ya kampuni ya Toyota?

Am just curious. Yangu ni hayo tu.
 
Uko nyuma sana ndugu.
Yale magari hawakutoka nayo huko kwao, yameandaliwa na serikali ya Tanzania kwaajili ya shughuli hiyo.
Tanzania kwenye suala la magari ya umma Toyota ndiyo chaguo nambari 1. Yawezekana Toyota wanawapa rushwa maafisa wa serikali na GPSA ili wapate upendeleo kwa kampuni ya Toyota kwenye manunuzi.
 
Labda kampuni ya Toyota wameamua kutumia mkutano huu kama fursa ya kutangaza biashara yao. I'm just thinking..
Mkuu ukichunguza hata mikutano ya SADC marais wanaenda kwa kutumia magari ya Toyota.
 
Hatimaye,
Rais wa Somalia kaingia na BMW.
 
Ninachokijua mpaka sasa ni ule mkutano wa chadema kuzuiliwa kwa nguvu na polisi,kumbe kwani kuna mkutano tena.
 
Uko nyuma sana ndugu.
Yale magari hawakutoka nayo huko kwao, yameandaliwa na serikali ya Tanzania kwaajili ya shughuli hiyo.
Tanzania kwenye suala la magari ya umma Toyota ndiyo chaguo nambari 1. Yawezekana Toyota wanawapa rushwa maafisa wa serikali na GPSA ili wapate upendeleo kwa kampuni ya Toyota kwenye manunuzi.
Mbona Mimi nimetumia Benz AU hukuniona?
 
Viongozi wa nchi zilizopo kaskazini mwa jangwa la Sahara hawapo kwenye huu mkutano.
 
Hilo swali ungeuliza serikali yako maana ndio waliondaa hayo magari.

Waalikwa wamekuja na ndege zao tu ambazo zimepaki Airport.
Mbona rais wa Somalia na Djibout wametumia magari tofauti? Na mbona nchi wanachama za SADC marais wao wanatumia Toyota?
 
Back
Top Bottom