Je, marais wa Afrika wameambizana kutumia magari ya Toyota kwenye safari zao?

Sio kuwa kila kiongozi alipakiwa na gari lake kwenye ndege
Basi itakuwa shughuli
Hilo huwa anafanya Rais wa US tena magari yanatangulia kitambo

Ila haya ni kodi zako na misaada ya bakuli letu
 
Viongozi wa nchi zilizopo kaskazini mwa jangwa la Sahara hawapo kwenye huu mkutano.
Hawakualikwa. Kwa muktadha wa Benki ya Dunia (wenye mkutano), nchi za Afrika ya Kaskazini hazihesabiwi kuwa Afrika bali eneo la Mediterranean. Afrika ni SSA (Sub-Saharan Africa). Hata EU na NGO kadhaa za kimataifa hutumia mgawanyo huo.
 
Wakati natazama ujio wa marais wa Afrika kwenye ukumbi wa JNICC nimegundua ya kuwa viongozi wengi waliowasili wametumia magari yanayofanana kimuundo na yote yametengenezwa na Toyota.
Watakuwa wamekodi sehemu moja
 
Uko nyuma sana ndugu.
Yale magari hawakutoka nayo huko kwao, yameandaliwa na serikali ya Tanzania kwaajili ya shughuli hiyo.
Tanzania kwenye suala la magari ya umma Toyota ndiyo chaguo nambari 1. Yawezekana Toyota wanawapa rushwa maafisa wa serikali na GPSA ili wapate upendeleo kwa kampuni ya Toyota kwenye manunuzi.
Kenya Nissan
 
Hawakualikwa. Kwa muktadha wa Benki ya Dunia (wenye mkutano), nchi za Afrika ya Kaskazini hazihesabiwi kuwa Afrika bali eneo la Mediterranean. Afrika ni SSA (Sub-Saharan Africa). Hata EU na NGO kadhaa za kimataifa hutumia mgawanyo huo.
Subsaharan africa ni sisi weusi,hao waarabu huko kaskazini ni waafrika ila hawana shida za umeme
 
Habari wakuu!

Wakati natazama ujio wa marais wa Afrika kwenye ukumbi wa JNICC nimegundua ya kuwa viongozi wengi waliowasili wametumia magari yanayofanana kimuundo na yote yametengenezwa na Toyota.

Kwa wale wajuvi wa mambo naomba mnieleze ni kwanini magari yao yanafanana na ni kwanini wanatumia ya kampuni ya Toyota?

Am just curious. Yangu ni hayo tu.
Kwani wote wakitumia gari za kampuni moja kuna tatizo gani au wewe unapungukiwa na nini. Cha msingi wafike eneo la mkutano hata kama wote wangetumia baiskeli za mbao za mninga wakifika eneo la mkutano salama haina shida.
 
Kwani kuna ubaya kuhoji kwanini wanatumia magari ya Toyota?
Kuuliza si ujinga.
 
Kuba watu hampaswi hata kuandika kitu humu sasa ww hujui kama magari ni ya serikali yetu mnatuchosha nyie darasa la 4 hv ww ukienda kusalimia kijijini unabeba na maji yako
Acha kejeli mkuu mi nimeuliza tu swali. Kama umeona la kipuuzi ungeachana nalo.
 
kutoka north korea,africa , India, north korea , Greece,indonesia,iran,iraq,palistan,philipnes,UAE, Syria,yemen wote hao wanatoyota kwenye convoy ya raisi na government kwenye baadhi ya taasisi pia.

Hizo nchi zote chache nilizozitaja .

Toyota is cheap and reliable.

Gari nyingine ni ghari sana kwenye maintainance na durability, huwezi chukua benz ukaiingiza ifakara huko zaidi ya toyota.
 
Uko nyuma sana ndugu.
Yale magari hawakutoka nayo huko kwao, yameandaliwa na serikali ya Tanzania kwaajili ya shughuli hiyo.
Tanzania kwenye suala la magari ya umma Toyota ndiyo chaguo nambari 1. Yawezekana Toyota wanawapa rushwa maafisa wa serikali na GPSA ili wapate upendeleo kwa kampuni ya Toyota kwenye manunuzi.
Mi pia niliwahi muuliza jamaa mmoja rafiki yangu,hivi ni kwanini serikali yetu wanapenda kutumia magari ya Toyota??,akanijibu kuwa serikali iliingia mkataba na kampuni hiyo tangu enzi hizoo,ambao ati uwezi kufutika kirahisi,lkn mi sikuridhika na jibu hilo,naomba nijue tena je kuna ukweli katika hilo??
 
Hakuna mkataba ,serikali inanunua gari toyota tanzania au wakala haijafungwa kununua toyota tu
 
🙇🙇🙇 ok asante. Mungu akusamehe sana na anisaidie kulipa mazur kwako kunitukania mzaz wang ambayo yy akukujibu ila n mm tu kweny kupeana mawazo mawili matatu
Kwa pamoja tujifunze kuchangia kwenye mitandao ya kijamii bila kufanya personal attack, hili ni ratizo kubwa kwa watz, hasa mtu anapohisi anajua zaidi kuliko muuliza swali au mtoa hoja.
Ukiiona mijadala ya nchi nyingine mfano Kenya, huwezi kuonà hilo, Ila utaona mizaha mingi na vituko, yaani swali na jibu haviendani, Ila hawamshambulii mtoa mada, sijui tatizo ni nini
 
Habari wakuu!

Wakati natazama ujio wa marais wa Afrika kwenye ukumbi wa JNICC nimegundua ya kuwa viongozi wengi waliowasili wametumia magari yanayofanana kimuundo na yote yametengenezwa na Toyota.

Kwa wale wajuvi wa mambo naomba mnieleze ni kwanini magari yao yanafanana na ni kwanini wanatumia ya kampuni ya Toyota?

Am just curious. Yangu ni hayo tu.
Bado UJINGA ni adui mkubwa wa taifa. Ndugu kwa akili yako ukajua marais wote walikuja na magari yao kwenye ule mkutano? Hujui kuwa yale ni magari ya serikali ya Tanzania yaliyotumika maalum kuhudumia hao wageni? Nimesikitika sana.
 
Back
Top Bottom