Je, matatizo ya Mwanamke ni fursa kwa baadhi ya Wanaume?

Usiwe hivyo ss mtu akikutongoza chukua tuu km funny usiweke bifu wala usione km ni ishu kubwa mfanyie I
Ukaruni mpk ataacha mwenyewe km huna malengo nae
Nimesema sipendi kutongozwa hasa nikiwa na mahusiano naona kero

But sijasema najenga chuki usinilishe maneno
 
Nadhani tatizo lipo kwa baadhi ya watu wanaotumia nafasi, mamlaka au uwezo wao wa kifedha kutafuta kile wanachokitaka kutoka kwa mtu aliye kwenye mazingira magumu.

Mtu anapohitaji kazi, msaada wa kodi, au fursa yoyote, anapaswa kuhudumiwa kwa haki bila kuwekewa masharti ya kimapenzi. Tatizo si msaada wenyewe, bali pale msaada unapogeuzwa kuwa mtego wa kutimiza matamanio binafsi.

Hata hivyo, ukweli mwingine ni kwamba tabia hii haipo kwa wanaume pekee. Wapo pia wanawake wanaotumia nafasi zao kuwabana wanaume wanaohitaji ajira au fursa mbalimbali. Hivyo tatizo kubwa ni matumizi mabaya ya mamlaka, si jinsia.

Mtu mwenye maadili anaweza kusaidia bila kutarajia malipo ya kimapenzi. Na anayesaidia kwa lengo la kupata uhusiano, anapaswa kuwa mkweli tangu mwanzo badala ya kujificha nyuma ya huruma.

Kwa mtazamo wangu, matatizo ya mtu hayapaswi kuwa fursa ya kumdhalilisha, bali nafasi ya kuonyesha utu.
 
Una utu na utulivu sana
Mpka unavyoandika🥰🥰

Shukrani mkuu❤️
 
Back
Top Bottom