Hizi mambo bwana, ni za ajabu.
Nakumbuka mshua alipata sukari mwanzon kabisa mwa miaka ya 2000.
Akasema alikutana na mzee mmoja wa kiarabu kwenye stori stori, akampa dawa. Ni ya unga.
Alikua anaweka kwenye uji, ya kwamba ukichanganya na uji unabadilika rangi huo.uji unakua kama mweusi. Anakunywa.
Mdogo mdogo ndani ya miez 3 akapona kabisa na sindano na vidonge akaacha kutumia. Akawa fiti kabisa.
Na anakumbuka alilipia kwa bia mbili 2 Safari maana ndo huyo mzee aliziomba.
Miaka kama 3 yote hakuwahi kujua suala la kisukari wala dawa wala sindano.
After hizo 3 yrs akasema subiri amtafte tena hata wapige stori maana hajamuona kitambo.
Kufika maeneo yake na kumuulizia, wakamwambia mzee alishadedi kitambo na kama kawaida ya waislam.hakukua na stori mob, alikufa asubuh, jioni akala futi sita.
Ule mshtuko, dingi akarudi tena kwenye sukari. Mpaka leo hii yupo nayo.
So all in all, yawezekana hizi madawa zipo, lakini kumpata huyo ambae yake iko legit ndo kimbembe.
Na most times mtu atakaeweza kukupa dawa ya kienyeji ambayo inatibu kweli, gharama yake hua ni ndogo sana.