Je, milioni 35 nizi-invest katika biashara ipi kati ya hizi?

Pharmacy inalipa ila ni biashara ambayo kila.mtu anaweza kuifanya na kukufanya kila siku usiwe na uhakika wa income yako.

Pharmacy Pia ina matumizi mengi sana, kwa upande wangu mimi ningeshauri upite na Idea yako no. 8


Lakini usi ifanye kama ulivyoandika "vituo saba vya uwakala mobile money" utakua unajidanganya.

Vituo 7 ukimaanisha kila kituo ukipe Mtaji wa 5M si eti? Kuna maswali ya kujiuliza

1.Ofisi unazo (kodi umelipia)?
2.Ukarabati Ndani nnje?
3.Vitendea kazi (mashine + line za uwakala)?

Hizi biashara usizichukulie poa watu wengi sana huona 5m ni hela nyingi, ukweli ni kwamba 5m ni pesa mingi kwa asie nazo lakini ni kijisent kwa vibopa.

Hivi unajua hii biashara anaweza akaja mteja mmoja tu anataka kutoa Mil 2 akaenda mishe zake akarudi baada ya lisaa li 1 akataka kutoa tena mil 1 akaondoka baaada ya 3 hrs anarudi anataka 2m

Unahisi ukiwa na ofisi ya mtaji wa 5m mteja wa namna hyo utamuweza?

Ukweli ni kwamba mkuu idea yako no.8 ni bora kwa upande wangu kama Pesa yote ikifungua OFISI 1 tu sio saba kama usemavyo.

Fungua ofisi 1 utakayoweza hudumia wateja wenye miamala mizito mizito uhakika wa 3m to 4m per month ni jambo la kawaida.

Miezi ya pesa kugusa 5M kwa mwezi ni kawaida tu BOSS lakini ili ucheze humo kwenye faida za haya maandishi yangu Atleast ucheze na capital isiyopungua 50M.

So kwa 35M utaanza biashara then utakua unaongeza mtaji up to 50M baada ya hapo anza kula Maisha.

fungua Asubuhi saa 2 kufunga saa 3Usiku Kwa mwezi 5M hiii hapa.

Make sure hukosei LOCATION usione tabu kulipia frem 1M kwa mwezi USIOGOPE yani wewe Mwanzo hakikisha una invest kupata FREM iliyo mdomoni kwa gharama zozote zile The more frem yako inakua mdomoni uhakika wakuvuka 5m kwa mwezi ni mkubwa.

Frem ikizidi kukaa mdomoni Mtaji wako ukawa stable basi Faida utazokua unapiga si za kuandika hapa.. siri zingine za Kambi tuziache tu ila nakusisitiza Mkuu kama una passion na hiyo no 8 Aseee zama mzima mzima.

Ingia kichwa miguu usiache kiungo chako nnje ya Box Biashara yenye Risk Free 91% hizi 9% hasara ni uzembe binafsi tofauti na hapo ni moja ya Biashara Zangu BORA kwa wakati wote maishani mwangu.

Assume una biashara za 50m za namna hiyo 4 kila wilaya kwa kila mkoa then kwa mikoa mikubwa yote zisambaze.

Halafu uniambie ukipata 200m utaenda kutungua Coaster uzisambaze road ufe kwa mapresha? aseee naomba niishie hapa ila mkuu chambua hiyo no.8 kimya kimyaàaa.
 
Nice.....
 
Ahsante mtu wangu umenifungua macho kikubwa
 
Ahsante pia kwa kuchukua muda kwa kudadavua kwa ukubwa..umesaidia wengi
 
Ile thread niliitafuta sana kipindi fulani ili nifanye reference, sikuipata , jamaa alielezea vizuri sana mambo ya mobile money na faida anayopata
Mkuu kama unaikumbuka link yake , iweke hapa kwa manufaa ya wote
 
Ile thread niliitafuta sana kipindi fulani ili nifanye reference, sikuipata , jamaa alielezea vizuri sana mambo ya mobile money na faida anayopata
Mkuu kama unaikumbuka link yake , iweke hapa kwa manufaa ya wote
Ila 300,000 kwa mwezi..bado haujalipa mfanya kazi..kodi ya pango ..wewe bado..
 
Ila mkuu naogopa gharama ya undeshaji kumlipa pharmacist, vibali..dispenser...au mauzo ya pharmacy yanalipa kupelekea ku- cover costs za undeshaji
Shida ipo hapa. Famasi ndio changamoto kubwa ipo hapo.

Ondoa wazo la pharmacy.

Weka Hardware, angalia vitu vinavyotoka anza na hivyo. Kwa kuwa mtaji sio mkubwa sana wewe cheza na mahitaji ya wateja wako chamganya umeme sementi misimari nk.

Baada ya muda uje unishukuru
 
Nimeumia sana
 
Shukrani boss
 
Maelezo zaidi itakuwa poa ndugu yangu..
Mkuu pharmacy zimeharibiwa Sana na maduka yanayouza Dawa baridi za mitaani. Dawa ambazo inabidi ziuzwe na pharmacy Kuna watu sio waaminifu kwenye hayo maduka wanaziuza pia. Kuna mengi ya kuandika unaweza kutafuta Uzi wa biashara ya pharmacy uko humu. Sio kwamba ni biashara mbovu inalipa ila jipe miaka kuanzia 3-5 uanze kuona faida nzuri.

Ushauri wangu kwa kuwa ndio unaanza biashara fanya biashara ambayo ni rahisi kuwa managed. Isiwe na Mambo mengi unapoisimamia. Do your own analysis.

Ushauri wangu fanya biashara yoyote ya chakula kwa Bei za kitanzania.

Fungua saloon.

Spare parts au hardware. Point kubwa ni location location. Poteza muda wako kutafuta maeneo yenye muingiliano wa watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…