Je, mita za LUKU zinawasilianaje na server za TANESCO?

Nadhani msingi wa swali upo hapo kwenye bold. Una maana kila kiasi cha units tunazonunua kina corresponding numeral arrangement?

Mmmh mkuu ni kweli lakini ni "a unique corresponding numeral arrangement" ambayo haitaweza kujirudia wakati wa manunuzi mengine mapya...(kama utakuwa ushawahi kusoma Pure Maths, kumbuka topic ya probability kwenye sub topic ya permutations).
 
Kama haina mawasiliano na Tanesco, vipi kuhusu ukataji wa ile asilimia ya service charge na makato mengine ya kila mwezi, inatambuaje na kuyakata?

Tanesco wanafahamu kuwa wewe unatumia kiasi gani cha umeme kwa mwezi kwa kupitia jinsi ununuavyo umeme kwa mwezi.

Katika server za tanesco kila mteja wa tanesco ana akaunti yake ambayo katika layman language tuifananishe na jedwali la attendence ya shule ambapo kila uhudhuriapo hujazwa kuwa umehudhuria na mwisho wa mwezi mahesabu ya kuwa umehudhuria siku ngapo hupigwa.

Tukirudi kwa tanesco, hesabu za kuwa unatumia unit ngapi kwa mwezi hupigwa automatically na utambuzi wa kuwa wewe ni mteja mkubwa ama mdogo hufanywa kwa kuangalia wastani wa unit unazotumia kwa siku.
 

Nashukuru kwa ufafanuzi, sijuhi kama hapa Tanzania full duplex trasmission inatumika kwenye media za waya za Tanesco i.e kwa wateja, ingekuwa hivyo basi wateja wasingekuwa na sababu ya kwenda kununua vocha/kadi, mita zao zingekuwa set remotely baada ya malipo - sasa zoezi la wateje kwenda kwa wakala kununua umeme ina maana teknolojia hiyo haja hota mizizi hapa Tanzania, teknolojia hiyo niliona kwa wenzetu wanao tumia HT wires kupitishia mawasiliano ya Video na internet nk. Tukija kwenye METER za LUKU kinacho fanyika pale ni count down inapofikia zero basi umeme unakatika kwa hiyo saula la ku-reset alipo unless sijui maana ya ku-reset - samahani lakini. Najua kuna meters za Wateja wakumbwa sinasomwa na Tanesco remotely - nina hakika pale wanatumia aidha GSM au Wi-Fi sio waya za Tanesco.
 
...
Tukirudi kwa tanesco, hesabu za kuwa unatumia unit ngapi kwa mwezi hupigwa automatically na utambuzi wa kuwa wewe ni mteja mkubwa ama mdogo hufanywa kwa kuangalia wastani wa unit unazotumia kwa siku.
Wanajuaje huo wastani wakati ni 'pre-paid'? Unaingizwaje kwenye tariff ya watumiaji wakubwa au wadogo wakati wewe ni pre-paid, yaani unalipa kabla ya kutumia? Watajuaje kama utatumia kiasi kikubwa au kidogo?
 

Tanesco wanatumia hii teknolojia ya kupitisha data kwenye nyaya za umeme kwa matumizi yao binafsi na si kwa ajili ya wateja. Wanatumia hii teknolojia katika mawasiliano ya wao kwa wao. And mostly ni kutoka katika HEP power plants na remote office za Tanesco.
 

Pamoja mkuu, thanks 4 the info - mkuu hivi si Tanesco walikuwa na Fiber Optics cables siku nyingi tu, hizo zilikuwa zinatumika kwenye nini hasa!!
 
Wanajuaje huo wastani wakati ni 'pre-paid'? Unaingizwaje kwenye tariff ya watumiaji wakubwa au wadogo wakati wewe ni pre-paid, yaani unalipa kabla ya kutumia? Watajuaje kama utatumia kiasi kikubwa au kidogo?

Records zako za manunuzi ya umeme kwa mwezi zinabakia katika database ya tanesco. Hivyo kujua wastani wa matumizi yako ni kwamba mwisho wa mwezi watachukua jumla ya UNIT walizokuuzia, watagawanya zimelast kwa muda gani mpaka wewe ulipoenda kununua tena umeme.
 
Hujanielewa mahali fulani. Kwa mfano ninanunua umeme wa unit 40 tarehe 3/10/2013. Sasa kwa nini wananiuzia kwa tariff ya watumiaji wadogo wakati hawajui labda baada ya siku nne nitakuwa nimeumaliza na hivyo kukosa sifa za mtumiaji mdogo huku nikiwa tayari nimeununua kwa tariff ya watumiaji wadogo? Msingi wa swali langu ni kwamba huo wastani wanaukokotoa baada ya matumizi au kabla ya matumizi? Kama ni baada ya matumizi, ilikuwaje waniuzie kwa bei ya tariff ya watumiaji wadogo? Kama ni kabla, watajuaje kama nataka nizitumie hizo units kwa siku chache au nyingi?
 

Understood
 
So zile code unazopewa baada ya kununua units zinaenda kutafsiriwa na luku ni units ngapi, na si kwamba unapo ziingiza zile code zinatumwa Tanesco kuwa verfied
Kwamaana hiyo LUKU haiwasiliani na server za Tanesco
Luku yoyote kabla yakufungiwa mteja inakuwa programed na imeingizwa kwenye database system ya tanesco ndiyo maana mwanzo ilikuwa vigumu kununu nje ya wilaya yako ila kwa sasa unanunua hata mkoani kwakuwa wamecentraliz hivyo ukiingiza no ta luku jwa venda kutokana na software waliyomuwekea yenye data za luku zote Ikiingizwa no ya luku inagenerate unit kwakuwa inadata za luku yako iko programed
 
Hujaitendea haki post yako kaka
 

inawezekana uliponunua mara ya kwanza ulinunua kwa tariff ya wadogo lakini baada ya miezi mitambo inaonyesha wewe ni mtumiaji mkubwa kwa kurecod matumizi makubwa ya units kwa mwezi ndio maana ukabadilishiwa tariff
 
inawezekana uliponunua mara ya kwanza ulinunua kwa tariff ya wadogo lakini baada ya miezi mitambo inaonyesha wewe ni mtumiaji mkubwa kwa kurecod matumizi makubwa ya units kwa mwezi ndio maana ukabadilishiwa tariff
Kwa hiyo nikiendelea na matumizi madogo kama awali watanibadilishia tena? Hapa naona tunahitaji mtu wa Tanesco
 

Nimekuelewa swali lako, kimsingi previous usage yako ya umeme ndiyo inakuhumumh wewe wakuuzie vipi umeme utakaponunua umeme kwa mara nyingine. Kuliwezesha hili ndio maana mwanzo wanapokufungia luku mpya wanakupa na unit za kuanzia, zile unit za kuanzia kimsingi hawakupatii bure kwani kama ni mchunguzi utagundua kuwa huwa wanakata pesa yake pindi utakapoenda kununua umeme mara ya kwanza ukiwa kama mteja mpya wa Tanesco.

Wanachofanya wanakupatia unit za kuanzia ili kukukadiria matumizi yako pindi utakapoenda kununua umeme kwa mara ya kwanza wakuuziaje. So kwa mara ya kwanza utumiaji wa unit za mwanzo wanazokupatia ndio zinaamua wakuweke katika kundi gani la wateja wao.

Kwa mfano tarehe 1/10 umenunua umeme na wakakupatia unit 60, kufika tarehe 15/10 server zao zikapokea request ya wewe kununua umeme na wakakupatia unit 60 then umeme huo unakaa mpaka tarehe 1 ndio unaisha. Hapo simply ni kuwa umetumia unit 110 kwa mwezi ambapo roughly ni wastani wa unit 3 na point kwa siku.

Na ikumbukwe Tanesco wanakudiscourage wewe mteja usitumie umeme sana. Kwani kwa sababu za kiuchumi, wanataka umeme nchini utumike kwa kiwango kidogo iwezenanavyo. So kama unatumia kidogo, utalipa bei kidogo per unit vice versa kama unatumia sana. Hiyo ndiyo sera ya tanesco..!
 

Tuko pamoja mkuu, ila mimi nadhani unaponunua/kufungiwa meter ya LUKU, wana isajili kwenye database yao ilikua na taarifa muhimu za mmiliki wa hicho chombo, na kwa kesi hii meter namba ndio inakua ID yako. Na baada ya hapo manunuzi yote unayofanya yanakua yanahusishwa na hiyo ID yako, lakini hakuna mawasiliano ya moja kwa moja na servers za TANESCO.

Ndio maana hata ukiokota receipt ya LUKU ambayo haijatumika huwezi kuitumia kwenye meter nyingine.
 
Na kwa evidence ndogo ambayo inaonekana kuhusu LUKU kutokuwa na mawasiliano na server za Tanesco ni hii, sidhani kama kuna hata mmoja wetu amewahi shindwa ingiza umeme kwa sababu ya ishu ya mtandao ( kama tanesco wasemavyo katika case mbalimbali za ununuzi wa umeme). Kwani ununuzi wa umeme ndio hutegemea direct comm na server za tanesco kwa sababh zilizotajwa na wadau wengine hapo juu.
 

Kitu kinachonifanya nifikirie kwamba matumizi yangu ya umeme hayahusiki sana na makadirio ya tariff nnayopangiwa na TANESCO ila wanaangalia nahudhuria mara ngapi kwenye vituo vya mauzo!
 
Kwenye mita karibu zote kwenye ile screen display zinakuwa na symbol ya network kama zile za kwenye simu, kwa maana hiyo nadhani kutakuwa na mawasiliano na Tanesco. Na kama sio za network zina maanisha nini?
 
Hapa kuna utata sana. Tukisema Tanesco wana mawasiliano na Luku, inakuwaje uingizwaji wa token za Luku ya Tanesco huwa hauleti usumbufu. Maana kama wana network ina maana iko stable balaa...
 
Wadau,mita za luku haziwasiliani na server. Mita za AmR ndo pekee zina chip ya mawasiliano na mita hyo authorized staf anaweza kukata na kuunga umeme remotely. mita hz kwa saśa zipo Tanesco na zimewashika watu kibao! mita ukifungua hata mlango inaalarm kwenye pc center huko!,Mita za kisasa zaidi,na zipo za 3phase tu tanesco.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…