Je, mita za LUKU zinawasilianaje na server za TANESCO?

Je, mita za LUKU zinawasilianaje na server za TANESCO?

Hapa kuna utata sana. Tukisema Tanesco wana mawasiliano na Luku, inakuwaje uingizwaji wa token za Luku ya Tanesco huwa hauleti usumbufu. Maana kama wana network ina maana iko stable balaa...

Mkuu Byanagandi ameeleza vzr sana namna luku inavyofanya kazi.
hakuna mawasiliano yoyote na server!, mawasiliano yapo wakat wa kuirejister kwenye system.
 
Majibu kwa wote..ndani ya hiyo meter ya luku kuna line (simcard) ya mtandao wa vodacom. Line hiyo ndo uwa inafanya mawasiliano na server ya vodacom kwenda tanesco.
 
Majibu kwa wote..ndani ya hiyo meter ya luku kuna line (simcard) ya mtandao wa vodacom. Line hiyo ndo uwa inafanya mawasiliano na server ya vodacom kwenda tanesco.

Kama hivi ndivyo kwanini basi haijawahi kutokea LUKU zikashindwa kuingia vocha hata kama kuna tatizo la mtandao wa vodacom?
 
NAOMBA NIKUJIBU KIUTAALAMU KIDOGO

katika nyaya za umeme zilizopo unaweza kutumia pia katika mawasiliano mbalimbali hii kitu inaitwa POWER LINE CARRIER wanachofanya ni kuinset signal zinazokua zina frequency tofauti na ile ya umeme mkubwa na pa kutokana na frequency kuwa tofauti basi na voltage power zinakua tofauti , nadhani umeme tunaotumia ni 50HZ ila wao kwa ajili ya mawasiliano wanaingiza frequency kubwa zaidi around MHZ kadhaa na kama unavyojua speed=frequency*wavelength so as frequency ikiongezeka na pia speed ya signal inaongezeka... na kwa kuwa hizi signal mbili zina frequency mbili tofauti inakua ni rahisi kuzitenganisha kabsa na kupata signal ya data na ya umeme tofauti....kitu kinachotumika hapa kuzitofautisha ni filters na couplers na pia kuna amplifier katikati ili kuzipa nguvu signal....
nadhani nimejitahidi kwa maelezo yangu machache maana hii kitu niliandikia project nikiwa first year miaka kadhaa iliyopita na kama wanavyosema elimu ni kile unachobaki nacho baada ya kusahau dessa zote so haypo ndio mafunyafunya niliyobaki nayo baada ya miaka kadhaa
 
Majibu kwa wote..ndani ya hiyo meter ya luku kuna line (simcard) ya mtandao wa vodacom. Line hiyo ndo uwa inafanya mawasiliano na server ya vodacom kwenda tanesco.
Kwa maana hiyo sehemu ambazo hazina network za simu, mita za LUKU zitakuwa haziwezi kuwa recharged?
 
mi binafsi nimeangalia kipindi maalum cha tanesco wakionyesha jinsi wanavyoweza kuaccess taarifa zako za matumizi ya umeme na hata kukukatia umeme wakiwa ofisini, ukiwa unachakachua wanafahamu, mechanism sifahamu, ila luku zinamifumo ya data, huamini uliza tanesco
 
We usipo nunua umeme wao wanaju mteja fulani mwezi huu akuja .hapo wanajua unachakachua ila ukilipa huku unachakachua awajui hawana network yoyote wale
 
Kwenye mita karibu zote kwenye ile screen display zinakuwa na symbol ya network kama zile za kwenye simu, kwa maana hiyo nadhani kutakuwa na mawasiliano na Tanesco. Na kama sio za network zina maanisha nini?

Weka picha.
 
Lol imenifurahisha discussion. Luku hazina mawasiliano yoyote, ila kadi au namba unayoingiza kwenye luku ina encrypted info ambayo inaiambia luku yako itoe units ngapi, that is all.

Kuhusu mahesabu ya matumizi kodi etc hayo yote yanafanywa kutokana na manumuzi yako ya units ambayo obviously yanahitaji kuwasiliana na server.

Kama ukitaka kujihakikishia nenda kanunue umeme mwingi kisha usiutumie kwenye luku yako utaona bado kodi yako itaenda kwrnye level ya mtumiaji mkubwa bila kuhali kama uliutumia huo umeme.
 
mi binafsi nimeangalia kipindi maalum cha tanesco wakionyesha jinsi wanavyoweza kuaccess taarifa zako za matumizi ya umeme na hata kukukatia umeme wakiwa ofisini, ukiwa unachakachua wanafahamu, mechanism sifahamu, ila luku zinamifumo ya data, huamini uliza tanesco

Kama kweli waliongea hivyo walikuwa wanatishia nyau ili raia wa kawaida waogope. Tanesco hawana teknolojia hiyo kwa sasa.
 
Kwenye mita karibu zote kwenye ile screen display zinakuwa na symbol ya network kama zile za kwenye simu, kwa maana hiyo nadhani kutakuwa na mawasiliano na Tanesco. Na kama sio za network zina maanisha nini?
Mkuu sijakuelewa! Sidhani kama symbol zinazo onekana kwenye screen zina uhusiano wowote na Wireless/wired network. Labda nizumgumzie kidogo kuhusu screen diplay generally, ni hivi Screen zote kuanzia za computer za kawaida, mobilephone, instrumentation (LUKU) zinawekwa pale kukusaidia wewe mtumiaji ujuwe kinacho endelea, lakini vifaa hivyo havielewi lugha ya alphanumerical character (alfabeti, namba, space, linefeed, formfeed nk) vifaa/mashine hivyo vinaelewa lugha ya ki-digitali tu {binari(0 na 1) na hexadesimali(0 - 16 na hizo ubadirishwa kwenye binari)} Kubadirisha text na namba ambazo binadamu anazielewa na kuziweka kwenye lugha ambayo mashines zinaielewa wanapashwa kutumia code ya kubadirisha text na namba na kuziweka kwenye lugha ya kidijiti kwa kutumia ASCII code kama nakumbuka vizuri, na si lazima mashine kutumia code ( ambayo hiko very popular) kuna code nyingine chungu zima cha muhimi hapa ni kubarisha text 2 binary. Back to the point narudia kusema binafsi sijawahi kuona LUKU inayo onyesha symbol za network, sikatai kwamba mita za nama hizo zipo duniani lakini kwa Tanzania sijawahi kuziona. Luku za hapa kwetu - kinacho onekana pale ni kWh, kuonyesha umeme uliobaki kadri unavyo tumia, kuonyesha zero wakati umeme unapokwisha, kuonyesha namba wakati una-topup, kuonyesha kama token imekubaliwa au la, kufuta namba na kuhingiza upya kama ulingiza kwa makosa nk.
 
mi binafsi nimeangalia kipindi maalum cha tanesco wakionyesha jinsi wanavyoweza kuaccess taarifa zako za matumizi ya umeme na hata kukukatia umeme wakiwa ofisini, ukiwa unachakachua wanafahamu, mechanism sifahamu, ila luku zinamifumo ya data, huamini uliza tanesco
Mkuu nafikiri walikuwa wanazungumzia LUKU zilizofungwa viwandani i.e watumiaji wakubwa nafikili siku hizi hizo mita zinafungwa kwenye nguzo mbali kidogo na kiwanda husika hawazifungi ndani ya kiwanda tena, LUKU za viwandani ndio zilizo wekwa mfumo wa kuwa monitored matumizi kutoka ofisi kwao na kufanya lolote wapendalo, sio LUKU za majumbani. Katika kubainisha uchakachuaji wa umeme wa majumbani nadhani wanangalia tred ya matumizi yako ya kila mwezi unapokwenda kununua umeme kutoka kwa wakala wao - hapo ndio wanaweza kugundua kama unachukua muda mrefu sana kabla hujanunua umeme wakilinganisha na historia yako siku za nyuma, kama kungekuwa na mawasiliano ya LUKU za majumbani na Tanesco kusingekuwa na ulazima wa Wafanyakazi wa Tanesco kutumwa ku-disconnect umeme nyumbani kwako wange disable mita wakiwa ofisini. narudia kusema kwamba kihunganishi cha wateja wa majumbani na Tanesco ni wakati unapo kwenda kununua umeme kutoka kwa Wakala wao ukiwa na mita namba yako - mashine za wakala ndio zinawasiliana na Database Servers za Tanesco kwaku-invoke track record yako na kufanya marekebisho fulani mfano malipo ya VAT, madeni kama unadaiwa na fixed costs collected kila mwisho wa mwezi, baada ya kumaliza zoezi hili ndio zitatolewa namba/code zenye information ya kiasi cha umeme ulionunua unapewa ili uzingize kwenye mita manually - kama mita hizo zingekuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na Tanesco kuna haja gani ya mteja kununua token na kuzihingiza manually kwenye mita yake, kwa nini hafanyiki automatically kutoka ofisi za Tanesco baada ya kununua umeme.
 
Wanajuaje huo wastani wakati ni 'pre-paid'? Unaingizwaje kwenye tariff ya watumiaji wakubwa au wadogo wakati wewe ni pre-paid, yaani unalipa kabla ya kutumia? Watajuaje kama utatumia kiasi kikubwa au kidogo?
Hivi unafahamu kuwa tumewekwa kwenye tarif tofauti tofauti kutegemeana na umepeleka mchoro wenye items ngapi wakati wa kuomba umeme?
 
Nadhani luku inayo programme ambayo inahifadhi matumizi ya umeme tangu mwanzo wa mwezi. Matumizi yakivuka low tariff rate, programme ina adjust salio la units kulingana na next tariff rate. Mawazo yangu.
 
Hivi unafahamu kuwa tumewekwa kwenye tarif tofauti tofauti kutegemeana na umepeleka mchoro wenye items ngapi wakati wa kuomba umeme?
Mkuu, wangekuwa wanafuata mambo ya mchoro wa kuombea umeme mbona wangeshafilisika mapema zaidi kuliko walipo sasa!
Mimi nadhani zile taarifa za maombi kwenye kadi ni za awali tu kwaajili ya kuprocess upataji wa service line, lakini taarifa zako za ukweli zinakuja kujulikana kwa jinsi mwenyewe unavyohudhuria kwa vendor.

Imagine mtu anaomba umeme wa domestic use, lakini kumbe anakuja kuutumia kuchomea mageti.
 
We usipo nunua umeme wao wanaju mteja fulani mwezi huu akuja .hapo wanajua unachakachua ila ukilipa huku unachakachua awajui hawana network yoyote wale

details za mita zipo kwenye database zao wanajua when was the last time ulirecharge.
 
So zile code unazopewa baada ya kununua units zinaenda kutafsiriwa na luku ni units ngapi, na si kwamba unapo ziingiza zile code zinatumwa Tanesco kuwa verfied
Kwamaana hiyo LUKU haiwasiliani na server za Tanesco
...wala LUKU haijui TANESCO ipo coordinate gani!
 
Majibu sahihi ni haya. Mita za LUKU za kawaida za majumbani hazina mawasiliano yoyote na Tanesco. Mita zinazofungwa kwenye nguzo na zenye remote zina mawasiliano ya moja kwa moja na Tanesco. Units za kuanzia unazopewa bure wakati mita yako ikisajiliwa ndizo zinazotoa majibu uwekwe kwenye kundi la wateja wadogo au wakubwa. Unaweza kubadilishwa kundi muda wowote kutegemea matumizi yako. Tanesco wanauwezo wa kuona line zote za umeme wakiwa ofisini kwa kutumia waya huo huo uliobeba umeme.
 
Mita za Tanesco wadau zinamawasiliano na server za Tanesco kabisa. Isipokuwa zimewekewa mfumo wa kugenerate units kutokana na namba za vocha utakazonunua. Mf. kwenye mita za sasa za Luku kuna Camera maalum ambazo zinadetect mtu anayeichezea mita na kupiga picha then kutuma kwenye server ya Tanesco ambapo wao watajua eneo ilipomita hiyo na kuja haraka. Afisa Uhusiano wa Tanesco Badra Masud alilisema pia hili huko nyuma na niukweli. Uncle wng ni Afisa wa Tanesco.
 
Back
Top Bottom